Unajua ukitaka kujua kiini cha tatizo ni lazima uende kwenye mzizi,
1. Kwa mara ya kwanza wa-Congo wapiga muziki, waliaza kuletwa Tanzania na Batengas, mfanya biashara maarufu sana zamani aliyekuwa rafiki mkubwa sana wa Mwalimu.
2. Batengas alikuwa akimilki club moja kubwa sana ya muziki pale mahali ambapo sasa kipo kituo cha Tazara, alianza na Nova success ambayo ilikuwa na kina Baba Gaston, Emmy, na Kabila Kabanze hii ilikuwa ni in the 60s, kipindi hiki hakuna aliyejali kama hawa wa-Congo, ana vibali vya kuishi nchini kwetu kwa sababu hakukuwa na competition na Batengas alikuwa ni mtu mwenye big political influence, hakuna aliyeweza kumgusa na hili swali.
3. Siasa zetu za taifa zilipoanza kubadilika, hawa wa-Congo, wakaanza kuhamia Nairobi, na wengine wapya wakazidi kuingia kuanzia in the 70s, wakaja Marquis, Banangenge, na Boma Liwanza, yaani kina Chinyama Chiyanzi, Fataki Masumbuko ya dunia, Nsilu wa Bansilu, Mbuya Makonga, Wabangoi.
- Hapa ndio kwa mara ya kwanza Batengas, akaaanza kushindana na wengine kama kina Hugo Kisima, kwenye hii field ya wanamuziki wa ki-Congo, ndipo kwa mara ya kwanza katika hii competition mpya, maswali ya vibali vya hawa wanamuziki kuwepo nchini hapa yaaanza, yaani kutoka kwa competitors wa Batengas, hatimaye Batengas alioonahawezi tena ku-deal na competition, akaamu kujitoa kwenye hii biashara na ugomvi ukaanza kwa waliobaki kwenye field na neno kubwa likawa vibali vya hawa wanamuziki.
4. Mpaka hapa local wetu, kina Mbaraka Mwinshehe ( Moro Jazz/Super Volcano), Balisidya (Dar Jazz/Afro 70), Wema Abdallah (Tabora Jazz/Western Jazz), Kassim Mapiri (Tabora Jazz), Wilson Peter (Simba Wa Nyika), Ahmed Kipande (Atomic Jazz), Juma Mrisho (Kilwa Jazz), Butiama Jazz, Marijani Rajabu (Saffari Trippers/ Dar International), Juma Ubao (Biashara Jazz), Shaban Dede (Bima Jazz), Salum Abdallah (Cuban Marimba), Gurumo (Msondo Ngoma), Juma Kilaza (Subi Subi), na wengineo walikuwa na fair share kibiashara ya market ya muziki nchini na hawa wa-Congo.
5. Lakini in the 80s, mambo yakabadilika kabisaa, kilikua ni kiipindi cha kuanza kwa matatizo makubwa ya kiuchumi, bendi zetu zikaanza kukosa vyombo vizuri vya muziki, huku wa-Congo wakisaidiwa na their former colonial masters, yaani wa-Faransa na Wa-Belgiji, walianza kurudi kwao na wakaingia kwenye kuu-promote muziki wa wa-Congo, Nairobi nayo kawa mwiba mkubwa sana kwetu kwa sababu kwa mara ya kwanza ikawa very clear kuwa wa-Congo, wana vipaji superior vya muziki kuliko sisi santuri zao zikaanza kutawala sehemu zote za starehe nchini, na nyingi zilikuwa zinatoka Nairobi,
-Mbaraka Mwinshehe ambaye kwa kawaida, alikuwa in the same league na Lwambo Makiadi, maana huko Congo Kinshasa kwenye radio zao na club za starehe miziki ya Mbaraka ilikuwa ikipigwa kwa usawa na ya Lwambo, lakini sasa ikaanza kushuka thamani kwa sababu bendi zetu bongo hazikuwa na vyombo vya kisasa, in fact hata Mbaraka alifariki akiwa anahangaika kutafuta vyombo vya kisasa, kwa sababu ukiangalia muziki wa Albamu ya mwisho ya Mbaraka, yaani "Shida", utaona tofauti kubwa kabisa na muziki wake wa zamani maana huu wa mwisho ulikuwa ni mzuri na uliotengenezwa kifundi kwa kutumia vyombo vya kisasa.
- Mfano mwingine ni Simba Wa Nyika, wao pia walihamia Nairobi na kufanikiwa sana kimziki, kwa kuwa na vyombo vizuri pmaoja na kuhsirikiana sana na wanamuziki wa Kio-Congo.
5. Haya mabadiliko makubwa kimziki kuanzia Nairobi, Congo Kinshasa, mpaka Brusells na Paris, yakaishia kuwapa the edge wanamuziki wa Ki-Congo, yaani sasa iikiiitwa Zaire, hapa bongo bendi za ki-Zaire zikaanza kutawala soko lote la muziki Tanzania, ni bendi mbili tu local yaani Msondo Ngoma, na Urafiki Jazz, ukiacha Tabora Jazz kwa mikoani ndio walioweza kusimama imara na kujaribu kushindana na hawa wa-Zaire, lakini ukweli bado ulikuwa wazi kuwa wa-Zaire wanawazidi sana kwa kupata watu,
-Ndio sasa vibali vya wanamuziki wa Zaire, ukaanza kuwa ishu kubwa sasa, kwa sababu sasa ndio hasa rushwa ilikaza mizizi nchini kwa kushirikiana na wafanya biashara wanamiliki hizo bendi za muziki, ndipo maofisa wachache wa uhamiaji wakagundua hazina kubwa ya hela za rushwa za kirahisi sana huku kwenye hii field ya wanamuziki wa ki-Zaire nchini, ndio maana wale wote waliofanikiwa kimuziki yaani wa-Zaire kama Kiki, Nguza, Chinyama (RIP), Mbuya Makonga (RIP), Assosa, Wabangoi, Massiya Radi (RIP), Kassongo Mpinda, Ndala Kasheba (RIP), Remmy, Makassy, Ilunga Lubaba, Bobo Sukari, Kasaloo Kyanga na wnegineo usingewza kusikia hata siku moja wana matatizo ya vibali vya muziki, ni kwa sababu walikuwa na uwezo mkubwa kipesa kutoa rushwa nzito, ni wale tu waliokuwa na uwezo mdogo kipesa ndio waliokuwa na matatizo ya vibali.
6. Sasa hili tatizo limekuwa too complicated kwa sababu soko la muziki wa dansi nchini, linatawaliwa na marafiki wawili yaani Msilwa (Twanga Pepeta), na Martin (FM Academia), ambao wamesoma pamoja Mlimani na walikuwa wakiishi chumba kimoja pale Mlimani, na ambao originally ndio walioanzisha ile bendi iliyokuwa maarufu sana zamani iliyokuwa pale New African Hotel ya Kassongo Mpinda, lakini baadaye waliachana na kwenda njia tofauti.
7. Martin alianzisha FM Academia, Msilwa akaanzisha Twanga Pepeta, John Komba akaanzisha Achigo Sound akishirikiana na Mundhiri na Nguza.
(a.) Twanga wakaamua kuwa hawataki wa-Zaire kwenye bendi zao ambazo sasa zilikuwa ni Twanga ya Ali Choki na Revolution ya Muumini Muniri na Badi Bakule zikiwa ni bendi zenye wanamuziki wazawa tu.
(b). FM Academia, ikawa ni bendi yenye wa-Zaire tu kina Nyoshi El-Sadat, Jose Mara, na Kitokololo, hawa wakapata mafanikio makubwa sana na ndio wanaotawala soko zima la muziki Dar na hatimaye wameanzisha bendi mpya ya Akudo.
(C). Kuona hivi Twanga Pepeta, ambao hawakuwa na soko zuri sana la biashara wakaanza nao kutafuta wa-Zaire kina Soko la Mandondo Diof, sasa ndio competiton tena imeanza kati ya Martin na Msilwa, kuona hivi dada wa Msilwa akaamia kujitosa kwenye NEC, kutafuta kinga na ubavu wa kupata vibali vya wanamuziki wa ki-Zaire kwenye bendi za kaka yake, huku upande wa pili Martin mzee wa Academia, yeye ni mzee wa system kwa hiyo hana tatizo sana na access ya vibali, lakini ni katika hivi vita vya hawa wapinzani wawili ambao sasa umehamia kwenye wanamuziki wenyewe, yaani hawa wa-Zaire, ndio unapata tatizo hili la vibali vyao vya kuishi hapa na kupiga muziki,
kwa sababu sasa wamefika mahali wanachongeana wenyewe kwa wenyewe, kutokana na kuoneana wivu, kabla ya hapo hakukuwa na tatizo kwa sababu hakukuwa na tatizo la mashindano ni mpaka majuzi tu Twanga, walioamua kuajiri wa-Zaire, sasa m-Zaire akitoka Twanga akaingia Academia tu, basi Twanga ni kwenda kumchongea kuwa hana papers na vice versa,
Kwa maoni yangu ni kwamba:-
Ukweli ni kwamba wengi wao ni watu wa Kigoma, kwa sababu kama umewahi kuishi huko utajua ninachokisema, lakini kwa sababu soko la muziki Dar linataka Wa-Zaire hijfanya wa-Zaire, sasa mpaka ofisa wa uhamiaji aje athibitishe hilo huwa jamaa ameshkaa ndani kwa mwezi mzima na magazeti yamesharipoti yetu uchwara yamesha ripoti bila na uhakika wa habari,
Wanamuziki wa kweli wa-Zaire, wengi wao huwa hawawezi ku-take hiyo risk ya kuja bongo kupiga bila kibali kwa sababu kwa kawaida wao huwa wako transit tu, siku zote wanatafuta kwenda kwenye masoko makubwa ya muziki wao, kama Paris na Brussells, au Nairobi ambako wanajua kuwa hawawezi kwenda huko bila makaratasi, na pia hawa huwa wana masoko hata kwao Zaire, kwa hiyo ni wajibu wa mfanya biashara anayewataka kuwatafutia makaratasi yanayotakiwa, maana hawawezi kukubali kuja bila papers kamili.
Now ni kweli kuwa wapo wachache sana wasiokuwa na makaratasi kabisa, kama na sisi wabongo huko nje, tunachofanya sasa ni kuwaa-abuse pale tu wanapohama bendi moja ya mwenye nguvu kwenda ya asiyekuwa na nguvu, sheria za taifa haziwezi kutumiwa kama kinga kwa baadhi ya wafanya biashara, kama nia na madhumuni ni wote wawe na vibali, basi ifanyike operation kubwa nchini wa-aire wote wapiga muziki wahakikishwe kuwa wana the right papers!
Samahani kwa kuwachosha, lakini nilitaka tu kuiweka hii sawa kidogo!
Ahsante Wakuu!