Wanamuziki wa extra musica

Mkuu inatajwa kuwa kundi la G7(Impressions Des As) lilianzishwa ili kupambana na hawa jamaa, lakini lilishindwa, je madai haya yana ukweli wowote?
Kama utausikiliza wimbo wa G7 uitwao Flueve Du Mal(Impressions Des As Album) utasikia sauti za moja wa watu kama kutoka Extra Musica.
 
G7 hawajawahi kuwa na muimbaji toka Extra Musica, G7 (Impressions Des As) album yao iliitwa Prenez vite !!! yenye nyimbo kama Ca va aller na Fleuve du mall. Ili wapate umaarufu, G7 walitumia muda mwingi kuwashambulia extra musica kwa maneno japo extra walikuwa kimya, hali hii ilifanya kundi hili kupoteza mvuto na kufanya album yao ya pili iitwayo A qui la faute na yatatu kutofanya vizuri sokoni na kupelekea kundi la G7 kupotea. Kumbuka Congo-Brazaville kuna makundi na wanamuziki wengi sana kama Mbuta Likassu, Arlus Mabelee, Alain Konkou, nk
 
Rogaroga kwema ? kule penye uzi wa tafsiri naona pamepwaya .
 
Mkuu Rogaroga nakushukuru sana kwa ufafanuzi. Ila G7 album hiyo walijitahidi sana. Fleuve du Mall naupenda sana.

Leo umenitoa matongotongo sikuwa na ufahamu kuwa Alain Konkou, Aurlus Mabele(I hope ni yule wa Loketo Group) Mbuta Likasu ni kutoka Congo Brazzavile! Hivi Tchico Tchikaya,Marehemu Jean Baron wanatoka Congo Kinshasa au Congo Brazzaville?
Taarifa nilizo nazo ni kuwa Aurlus Mabele(Groupe Loketo) alipata stroke, sijui kwa sasa afya yake ikoje maana ni muda mrefu kidogo tangu nisikie hivyo!

Ubarikiwe sana Roga roga.
 
Tchico Tchicaya, Ballu Canta, Zitani Nell, Pierre Belcos, Lucien Bokilo hawa wanatoka Brazaville. Kuhusu Arlus Mabelee nalifanyia kazi swala lako.

Ona mfanano huu wa Congo Brazzaville na Congo Kinshasa

Congo Brazaville
Official language: French
Recognised languages: Kikongo, Lingala
Main ethnic groups: Kongo, Sangha, M'Bochi, Teke


Congo Kinshasa

Official language: French
National languages: Kikongo, Lingala, Kingwana (Swahili), Tshiluba
Main ethnic groups: Kongo,Mongo, Luba, Mangbetu-Azande


The two closest capital cities between two sovereign countries are Kinshasa, Democratic Republic of the Congo, and Brazzaville, Republic of the Congo, which are about 1.6 km (0.99 mi) apart, one upstream from the other on different banks of the Congo River (the distance between the middle points is about 10 km)
 
Mkuu ahsante sana. Kuna uzi unazungumzia wanamuziki wa Congo, karibu watu wanashusha nondo kule balaa. Tunategemea mchango wako. Watu wamezungumzia Amida Shatur kumsaliti mumewe na kuolewa na Didi Kinuani, na baadae JB mpiana kukubalina kurudiana nae, hadi picha ya mtoto wa Amida aliyezaa na Kinuani ipo tena mtoto kamshika Mpiana
 
Ngoja niutafute nije na nondo huko
 
Kwa
Kwa hiyo mkuu huyu kindoki wa yanga ni ndumba?
 
Nipo naanda story kuhusu Loketo group, keep wait
Ok mkuu,tunasubiri kwa hamu.
Hivi JB Mpiana yuko wapi? Mbona hana nyimbo zinazobamba kama zile za zamani mfano wa zile Album kali za
Titanic,Toujours Humble,Internet. Alipotoa Ant-Terror haikufanya vizuri sana na tangu hapo sijasikia Album nyingine kuzizid hizo 3
 
Yupo, ana albamu nyingi tu mfano ni Kipé Ya Yo (2007), Quel Est Ton Probleme n.k Tatizo albu hizi kizazi kikubwa cha wenge kama wakina Titina, Aimelia, Alain mpella walikuwa wameshajitoa kwa JB Mpiana na JB kwa kiasi fulani anaangushwa na Serguin Mignon ambaye ndiye drummer wake
 
Nipo naanda story kuhusu Loketo group, keep wait
Mkuu ile nyimbo ya Extra Musica niliokuwa naisema Oxygene ni Cri du coeur (oxygene) ambayo ipo kwenye album ya etat major
Tafazal nitupie kiongozi
Pia hizi zifuatazo
[emoji673] Chagrin plus plus
[emoji673] Amie ravens
[emoji673] Losambo
[emoji673] Na ko bala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…