Wanamuziki wa Congo(DRC) na vituko na mikasa yao. Akina Defao, Madilu,Franco Luambo

Huu uzi ulikua mzuri sana ila majigambo ya baadhi ya wachangiaji umesababisha tukose vitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wanapenda ujuaji usio na mantiki yeyote. Hawa wasanii kila mmoja anauzuri na madhaifu yake. Napenda sana Sauti ya Jb Mpiana, sikiliza omba au papito, ila jamaa ni mbinafsi sana ndio maana hakuna artist wakali 5th gen waliotokea kwa Mpiana. Juzi Migon kaeleza kupewa nafasi ya kuingiza nyimbo solo ili usikike ni ngumu. Werrason ni mbahili na halipi vizuri, ila anatoa sana nafasi na uhuru kwa artist wake ndio maana kina ferre, fabregras, watanabe, celeo scram wamehit wote ni Werrasonique. Koffi ni tapeli na mfitini sana. Kwa ushirikina wote ni washirikina.
 
Mtaalam Genta, kuna ngoma moja ya kikongo. Wanaimba halafu kuna kajamaa kanaimba dunguru dunguru du wenzake wanajibu BASUPA. Naomba uniambie hiyo ngoma inaitwaje na ni ya kundi gani. Nitashukuru brother, kwa sababu hiyo ngoma ninaikubali sana.
Huo wimbo unaitwa PONDERATION 8 wa Blaise Bulla
 
Back
Top Bottom