Wanamuziki wa Congo(DRC) na vituko na mikasa yao. Akina Defao, Madilu,Franco Luambo

Siyo ' Solora ' no ' Solola ' Mkuu. Halafu Album ya Kwanza ya Werrason ya kumjibu JB Mpiana na Album yake ya Titanic haikuwa hiyo ya ' Solola Bien ' bali ilikuwa ni ya ' Force Intervation Rapide ' ikimaanisha kwamba ni ' Kikosi Maalum cha Uvamizi ' alichokuwepo na Waimbaji akina Adolphe Dominguez na Aimelia Byakodile.

Kila la kheri.
=Kikosi maalum cha Uokoaji
 
Kaka nenda nae Taratibu atakuelewa tu, jina la BCBG alikuanza baada ya bendi kuparanganyika, hilo jina lilikuwepo hata wakati bendi haijavunjika

Urafiki wa Koffi na Werrason haukuanza wakati wakiwa wamesambaratika, ni urafiki wa Muda mrefu tu, wakati huo JB akiwa karibu sana na Papa Wemba na hao Koffi na Ppa Wemba ndio miongoni mwa waliosababisha bendi hiyo ya Wenge Musica kuvunjika
Fact
 
Kama shida yako ni Nyimbo tu za JB Mpiana ambazo Gitaa la Solo limepigwa vyema na lazima tu utalifurahia ni hizi zifuatazo:
  1. Eve Sukari ( katika Album ya Kine Bouger ) hapa Solo alipiga ' Fundi ' mwenyewe Alain Makaba ' Prense '
  2. Filandu ( katika Album ya Pentagone ) hapa Solo alipiga ' Mwalimu ' mwenyewe Ficarre Mwamba
  3. Masuwa ( katika Album ya Ndombolo ya Solo ) hapa Solo alipiga tena ' Fundi ' mwenyewe Alain Makaba ' Prense '
  4. Liberation ( katika Album ya Titanic ) hapa Solo alipiga ' Mtaalam ' mwenyewe Burkinafaso Mbokaliya
  5. Decision ( katika Album ya Anti Terror ) hapa Solo alipiga ' Mwalimu ' mwenyewe Ficarre Mwamba
  6. Mohammed Kaniansy ( katika Album ya Toujur Humble ) hapa Solo alipiga ' Kifaa ' mwenyewe Patrick Moleso
  7. Le Tenant Du Titre ( katika Album ya Internet ) hapa Solo alipiga ' Kifaa ' mwenyewe Patrick Moleso
Nakuomba uzitafute hizo nyimbo kisha zisikilize kisha uje unipe ' mrejesho ' wako Mkuu.

Kila la kheri.
Mkuu tupia audio ya masuwa, eve sukari na filandu nimezitafuta sana hizi ngoma sijazipata
 
GENERAL DEFAO
mara ya kwanza nasikiliza album ya Defao (Defao Matumona) ilikuwa inaitwa General and Big Stars mwaka 1993 nlipenda saut ya huyu jamaa alikuwa naimba kw autulivu flani ingawa sikuwa najua maana ya nyimbo zake. kuanzia hapo nilikuwa napata nafasi ya kusikiliza kila album yake.kipindi hicho alikuw ana mwonekano mzuri hakuwa amejichubua sana kiasi hiki cha mwisho ambapo alikuwa mpaka anaonekana kama vile ni ghost.

ana album nyingi sana lakini Sala Noki 1998 ni album ambayo binafsi nliikubali sana pamoja na Amour Interdit 1996. nyuma ya hapo zilikuwepo album kama Big Stars Du general Defao ya mwaka 1992 ,Famille Kikuta 1997 na zile akiwa na Choc Stars. alikuw ani muimbaji mzuri sana na style yake ya kucheza haikuwa ukitumia nguvu sana pale anapochangamka baada ya kulalamika. miaka ile ya africa moto,mpaka chamukwale...ni mtaalamu mzuri wa rhumba,ndombolo na soukous.

jambo la kusikitisha lilikuwa huyu jamaa inasemekana analiwa jicho.alikuwa si riziki... hili lilikuja kufahamiaka baadaye na hata alipokuja dar kuna watu inasemakana walipata nafasi ya kumla jamaa. na ukija kumwangalia jamaa kwa kweli alijichubua sana pamoja na kuwa wakongo wanaupenda sana weupe ila huyu jamaa alifikia mpaka kuonekana kama ni lijimama flani shangingi hivi. alikuwa amejichubua na alipenda kuvaa vito mikononi na shingoni. defao hakuwahi kukanusha jambo hili kuwa watu wanamla nyota.

MADILU SYSTEM

Jean de Dieu Makiese aka Madilu Multi System....huyu jamaa alikuw amuimbaji mzuri sana hawa wa rhumba toka miaka akiimbia TP OK Jazz na akina Simaro kiambukuta, akiimba na akina Franco Luambo Makiadi. toka miaka ya 1970 mpaka 2007 alipofariki. aliibuka TP OK Jazz na kibao cha Mamou ndo kilimuinua akaanza kusikika. Franco et le T.P. OK Jazz Presents Madilu System mwaka 1985. album hii utamsikia kwa mara za mwanzoni kabisa akiimba kwa utulivu. sauti alikuwa nayo nzuri sana. umewahi usikiliza wimbo wa frere duardo? akicheka? au ya Jean.. jamaa alikuwa akiimba kwa utulivu sana isikilie Frère Edouard 1996. mimi binafsi nilianza kumsikia miaka ya nyuma sana toka 1990 akiwa na TP ok Jazz. albuma yake ya Pouvoir 2000, na nyingine kadha wa kadhaa....

Madilu inasemakana alikuwa ni mshirikina sana. alikuwa mshirikina kiasi kwamba wanasema ilikuwa ili kupata pesa aliwahi kwenda kwa mganga ambako alitengenezwa ikawa kila baada ya muda flani inabidi afe... alikuwa na chumba maalum ambacho ilikuwa ikitokea ameenda kwenye kile chumba anatakiwa akae siku kadhaa ambapo huko atakufa na kuoza. ndani ya siku kadhaa mkewe inabidi aende akazoea wale funza akawaweke kwenye mifuko mikubwa ambayo ndo zilikuwa zinakuwa pesa.

inasemekana ilikuwa ni siri ambayo anaijua mkewe tu na hakutakiwa alie ikitokea hali hiyo.then baada ya siku kadhaa anazinduka akiwa kama binadamu na wanaendelea na maisha yao. suala hili lilikuja kuzungumzwa sababu duniani hamna siri.

shutuma hizi za ushirikina kwa wanamuziki wa kongo ni za zamani sana toka miaka ya akina Franco Luambo Makiadi, akina Pepe Kalle n.k wamekuwa na tabia hii ya kuamini sana ushirikina.

Lawama na shutuma za namna hii zimekuwepo hata kwao wenyewe kwa wenyewe. Mara kadhaa koffi olomide amekuwa akisema kuwa mwanamuzi fally ipupa alitoa sadaka wazazi.koffi anasema lacoste ni muimbaj mzuri sana kuliko fabregas.lakini kwa kuwa fabregas anatoa saba sadaka amekuwa maarufu na anapendwa sana.

Alipofariki kiongozo wa zaico langa langa dv moanda kulikuwa na ukakasi mkubwa nani achukue nafasi yake hasa kutokana na majukumu aliyokuwa nayo kishirikina kulisaidia kundi.

Imekuwa kawaida sana kwa wanamuziki wa kongo kuua wazazi,wake,watoto au wenyewe kwa wenyewe wanapotaka kutoa album au mara baada ya kutoa ili kuweza kuuza sana.lakini masharti mengine yamekuwa ya mwanamuzik kufanya mapenzi na mama yake mzazi ili aweze kuwa maarufu.ukiacha hayo wamekuwa wakirogana sana na kuharibiana kupitia wanawake n.k
Ila muziki wa Congo mtamu tangu mwaka 1988 nasilikiliza sana nyimbo za hao magwiji kwangu nimejaza nyimbo zao,
Ushirikina siyo Congo tu GU Dume hili ni suala la jamii zote duniani, fikiria waganga wote waliopo Bagamoyo, Tanga, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Shy, Simiyu, Geita, Lindi, Mtwara, Njombe, Ruvuma nk kwahiyo katika maisha wengine wanaamini bila kupitia kwa waganga hawawezi kupata mafanikio
 
maswali mengine ya ki wacky kweli
Kumbe unataka maswali tu Mkuu sawa yanakuja. Haya naomba kujua yafuatayo tafadhali kwani hata Mimi ni Mgeni mno katika miziki hii ya Kikongo hasa ihusuyo Bendi ya Wenge BCBG
  1. Naomba unitajie ' Lead Singers ' Watano tu wa Wenge BCBG
  2. Ukishanitajia naomba unitajie na aina za Sauti zao ambazo huwa wanaziimba kati ya zile Kuu Nne ( 4 )
  3. Atalaku / Mghani / Rapa / Animateur mpya wa Wenge anaitwa nani na alitokea Bendi ya Msanii gani Congo DR?
  4. Huyo atalaku ameletwa hapo Wenge BCBG kuziba pengo la nani na kumsaidia nani aliyepo kwa sasa?
  5. Ni Wimbo gani ambao kila mara Wenge BCBG inapopiga ' Live Shows ' zake popote pale duniani ni lazima waanze nao na ni upi ni lazima wamalize nao?
  6. Ni kwanini katika Bendi nzima ya Wenge BCBG ' Wanamuziki ' wake hawatakiwi kushika ' mic ' zao kwa mkono wa kushoto bali wanatakiwa kuishika kwa mkono wa kulia tu pale wanapokuwa wanaimba iwe stejini au mazoezini?
  7. Naomba unitajie ni Mcheza Show gani wa Kike wa Wenge BCBG amepewa jina la Mchezaji mpira wa Italia aitwae Zambrotta? Naomba jina lake tu tafadhali.
Umetaka maswali nami nimekupa hayo juu hivyo hangaika nayo tafadhali kisha unipe majibu na nakuruhusu pia uombe msaada kokote kule ambako utaona kunafaa tafadhali. Unaweza ukanijibu sasa hivi kwani Saa 5 Kamili na log out humu au pale nitakaporudi humu tena mnamo Saa 8 na Robo mchana.

Akhsante.

Cc: asrams

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom