Wanamtwara mmesahau kuliwa na Simba?

Wanamtwara mmesahau kuliwa na Simba?

Yaani kwa wanamtwara sio Makongoro tu kwa Wana Mtwara CCM ni tatizo ni janga inapaswa wasiisahau,ni juzijuzi tu wameonja shida wameishi kama wapo enzi za ukoloni wa Mjerumani,Mtwara kulikuwa hakuna uhuru,hakuna kukaa katika vikundi vya mijadala kwa kweli nakusapoti Asilimia mia Moja wakiona mtu yeyote wa CCM inabidi wapaze sauti kubwa ya kumkataaa.wana Mtwara Say No to CCM

Soma vizuri mada, uelewe nani aliwalisha kwa simba wana Mtwara, usirushe.
 
Umenikumbusha hadithi ya "simba karatasi". Wananchi wa ntwala....hahahaa!

Muwe na maamuzi bora mchague kiongozi anayeweza kuwatoa point A kwenda B.
 
Siku zote tunakuona wewe tu. Nani vile huwa unasema? Punguwani Wahedi au Punguani Wahedi?

JF + Ajuza FF + Nyerere = You make my day. Long live JF na Ajuza. Bahati mbaya Nyerere ni Hayati.

Mada umeiona lakini kwenye post namba moja? au wewe umeniona mimi tu?
 
Waliuliwa na Simba au waliliwa na Simba? Ulikuwapo wakati wanaliwa? Na kama ulikuwepo, ulifanya nini ili kuwasaidia?

Prof. Kazilahabi kwenye kitabu chake cha Gamba la nyoka anasema "hilo zoezi lilikuwa kama kukamua usaha."

Ukiuacha, unauma na ukiukamua, unalea maumivu. Ukichema nchale, ukimumunya nchale, ufanye nini?

Leo hii Gas inapatikana, itakuwa rahisi kupata huduma vijijini kuliko wangeliachwa waishi kama Wamongolia.

Ukisikia kiongozi lazima awe na uwezo wa kuamua majukumu magumu, ndiyo alikuwa Nyerere.

Kwamba walikuwepo watu fulani Mataahira na wazembe kama Mzee Ruksa aliyeanza kuuwa vikongwe huko Shinyanga, hilo ni swala jingine. Kwenye operation kubwa kama hizo, makosa lazima yatokee. Vijiji vilianza na tumesoma wengi wetu humu ndani. Nyie mmeanzia shule za kata, hahahahaaa shule za kata.

IMG_3819.JPG

Barbarosa
 
Last edited by a moderator:

Mbona sikuelewi hoja yako ni nini haswa ya kwamba unapinga kwa Wanamtwara hawakudhuriwa na Simba kwenye hivyo vijiji walikosombewa ambavyo havikutayarishwa kuishi binadamu?
 
Mwenye macho haambiwi TAZAMA. Kama unashindwa kuelewa hicho nilichoandika, utamuelewa Nyerere kweli wakati unasimuliwa tu ya nini kilichotokea wakati ule? Utamu wa mtungi anaujua kata. Wewe potezea tu.

Pouwa!

chuki dhidi ya nyerere haitawafikisha popote.....mpende msipende ndo baba wa taifa la Tanzania period...kwani simba alikuwa anawatuma yeye..mbona maeneo mengi ya tanzania watu wanaliwa na simba hadi leo...na nyerere hayupo...acheni chuki...
 
Watu walilidhuriwa na simba kwa sababu walihamishwa kutoka nyumbani kwao na kupelekwa sehemu nyingine au vijiji vya ujamaa ambavyo vilikuwa havijatayarishwa vizuri matokeo yake ni kwamba watu wengi waliliwa na Simba na mambo mengine mengi na ndio maana mambo ya kuliwa na Simba yako huko huko Mtwara tu, hivyo hapa siyo swala la kuwa na chuki na Mlm.Nyerere (,,Apumzike kwa Amani") bali ni swala la ukweli, na ukweli ni kwamba Watu waliliwa na Simba kwa sababu ya maamuzi ya Mlm.Nyerere!!
 
Kwan sera ya villagilization ilikuwa mbaya kuwen waungwana..nyerere asingefanya ivo tanganyika ya leo ingekuwa vipande vipande

Kama haukiliwa na Simba ni rahisi kusema kwamba kilikuwa kitu kizuri lakini ukiwaliza watu ambao waliona live ndugu zao wakiliwa na Simba nafikifiri watakuwa na jibu lingine!
 
Kumbe hata aggression huna? Samahani Mkuu, kumbe hata Makuu huna. Mambo yako hivi:

Kuhamisha watu kwenye vijiji vya Ujamaa ilikuwa lazima na ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na faida yake ilionekana baada ya muda mfupi kwani mwaka kama sikosei 1975, asilimia 94 ya Watanzania walijua kusoma na kuandika.
YES, walijua kusoma na kuandika na shangazi yangu ambaye hakusoma utotoni, nilishuhudia akianza kusoma na kuandika kanisani ambapo zamani alikuwa akiimba nyimbo kwa kuzikumbuka tu.

Katika hiyo operation, kuna makosa mengi yalitokea pia. Mfano unaofahamika sana ni kuuawa kwa Wazee wenye macho mekundu huko Shinyanga. Unajua sisi Wanyamwezi, tunawasha moto ndani na usiku pia ili kupata mwanga. Matokeo yake wale Wazee wanakuwa na macho mekundu na vijana wa Mwinyi wakawa wanajua ni Wachawi. Basi ukaanza msako na Wazee wakawa wanauawa. Mwinyi kama Waziri wa mambo ya ndani akajiuzuru.

Vijiji vingine vilipangwa kwa kukomoana na hilo nakukubalia ingawa ukweli ni kuwa vingi viliwekwa sehemu ambazo barabara zitapita na wakati huo wengine walichukulia kama wametupwa sehemu zenye Simba.
Ule uzembe wa watu kuchelewa kuhama kama ilivyo leo sehemu za mabondeni hata wakati ule ulikuwepo. Watu waliombwa mara kadhaa wafungashe tayari kuhama ila wao waligoma. Hapa ndipo wanakuja wale vijana Wakorofi na wanajeshi ambao waliwabeba na kwenda kuwatupa mbali na kwao ili wasiweze kurudi tena kwenye nyumba zao na nyumba hizo zilichomwa moto. Wengine badi walirudi.

Kama ukiniuliza mimi leo hii, bado ntakubaliana na mpango wa Nyerere ila tu labda ingelibidi kujenga walau sehemu za kufikia watu kabla hawajaanza kujenga nyumba zao, walau mashuleni.
Huku SIKONGE, vijijini vingi ambavyo leo hii vinafanya vizuri kwa shule, kilomo na maisha kwa Wanakijiji ni vile vijiji vya Nyerere ambavyo vilianzishwa kipindi hicho.

Ni rahisi sana leo kulaumu yaliyotokea wakati ule. Nyerere kama RAIS anabeba lawama zote ila alifanya hivyo kwa nia nzuri kabisa. Kule chini kuna watu walichemsha. Hilo ni lazima utegemee litokee. Kumbuka wakati huo, usafri, barabara na mawasiliano kwa Tanzania ilikuwa kama miujiza.

Kama hii ndiyo sehemu Rais anapiga kura, huko mikoani kulikuwaje? Eti hapa ni Urambo mwaka 1951.

ck3.jpg
1-30.jpg

Pouwa!

Mwaka huu mtafukua makaburi yote maccm
 
Kwan sera ya villagilization ilikuwa mbaya kuwen waungwana..nyerere asingefanya ivo tanganyika ya leo ingekuwa vipande vipande

Sera hiyo sijawahi kuisikia.

Sera ya kwenda kuwafanya watu chakula cha Simba unaiona ni nzuri? au kwa kuwa hukuwepo? mleta mada kayasema ya simba tu, lakini kuna waliogomgwa na nyoka, kuna waliokosa matibau ya kawaida na wakafa hovyo, kuna walikufa kwa njaa huko maporini na kula matunda na majani yaliyowadhuru, kuna wengi sana waliopoteza maisha yao wakati huo na si Mtwara pekee - kumbuka hilo.
 
Hayo angesema FaizaFoxy angeambiwa "mdini" analeta "udini".
Unajua kusema kweli linapokujaga
suala la dini,tunatakiwa kuwa makini kwenye kuchangia,

Mjadala wa huyu jamaa unaona uko neutral
ni wa kitaifa zaidi,lakini angesema ''Nyerere alisababisha
waislam wa mtwara waliwe na simba''
tungemnanga na tungesema ni mdini.
Sasa pitia mijadala yote uliyochangia ukaitwa mdini
ipitie mara mbili-mbili utakuta element za udini
na hizo kila mtanzania aliyeiva lazima azipige vita.

Lakini sehemu nyingine mbona unachangia vizuri
na watu wanakupa LIKE?
 
Barbarosa

Jana kwenye TV niliwaona wanamtwara wanamtaka Mh.Halima awaombe msamaha eti amewazalilisha
wanasema ardhi yao wameitoa kwa kuridhia na si kwamba wamenyanganywa.

Nimesikitika kuona viongozi wa mtwara hawajui
kuwa watu wanaongezeka ila ardhi,iko palepale
unapotoa maelfu ya heka kwa kuangalia leo
kesho watoto au wajukuu zako watapata shida.

Mi naona afadhali ya Nyerere alikuwa anafanya
jambo kwa kumaanisha na hata lilipoleta
negative effects zilikuwa si za kukusudia.
kwa sasa watawala wanajua wanachokifanya
na kwa ufinyo wa elimu,raia wanaona ni sawa
kesho utakuta wanataka kuandamana.
 
Last edited by a moderator:
Unajua kusema kweli linapokujaga
suala la dini,tunatakiwa kuwa makini kwenye kuchangia,

Mjadala wa huyu jamaa unaona uko neutral
ni wa kitaifa zaidi,lakini angesema ''Nyerere alisababisha
waislam wa mtwara waliwe na simba''
tungemnanga na tungesema ni mdini.
Sasa pitia mijadala yote uliyochangia ukaitwa mdini
ipitie mara mbili-mbili utakuta element za udini
na hizo kila mtanzania aliyeiva lazima azipige vita.

Lakini sehemu nyingine mbona unachangia vizuri
na watu wanakupa LIKE?

Weka ushahidi wacha porojo, huwa sikisii.

Mkikosa hoja na ya kuwaingia ndiyo mnakuja na kauli mbiu ya "mdini".

Ukishindwa kuweka ushahidi basi wewe utakuwa ndiyo mdini na fataani na muongo juu.

Nnasubiri.
 
Back
Top Bottom