Pande zinazopigana zalaumiana kukosa uaminifu wa kusitisha mapigano Nchini Sudan

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Licha ya kuwepo kwa mazungumzo ya kusitisha vita baina ya pande mbili zinazogombea madaraka kumeibuka lawama huku kila upande ukilaumu

Jeshi la Sudan na wapiganaji wa Vikosi vya RSF wameendelea kutishia utulivu hasa katika Mji Mkuu wa Khartoum na hivyo kuwa na uwezekano wa kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki moja yaliyosimamiwa na Jamii ya Kimataifa.

RSF inayoongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Daglo, imemlaumu Mkuu wa Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan kuwa chanzo cha kukiukwa kwa usitishwaji wa mapigano wakati jeshi nalo limedai limezuia shambulizi lililofanywa na RSF, hali inayoonesha wanakiuka makubaliano.
 
Back
Top Bottom