Serikali ya Sudan kuikimbia mji Mkuu Khartoum na kuhamia Port Sudan

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,232
6,479
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Generali El Burhan, amesema serikali kuu na Jeshi zinajiandaa kuhamia Port Sudan mji wa mashariki mwa Sudan.

Hatua hii imekuja baada ya wanamgambo wa RSF kushikilia maeneo yote nyeti ya mji Mkuu Khartoum.
Kiongozi wa RSF Generali Mohamed Daglo, ameionya hatua ya kuihamisha mjii Mkuu wa utawala kwenda Port Sudan ni kuigawa nchi na sio kuunganisha.

Amesema hilo likitokea ataunda serikali yake na yeye yenye makao makuu Khartoum. Hata hivyo kasema yupo tayari kwa mazungumzo ya amani sambamba na kurejeshwa kwa serikali ya kidemokrasia chini ya uongozi wa kiraia.

Kiongozi wa Kijeshi wa Sudan El Burhan anadaiwa hataki mazungumzo. Vita vya Sudan viliibuka April 15 mwaka huu huku serikali ikiahidi kuwamaliza wanamgambo ndani ya wiki mbili tu.

Source: BBC
 
Wote ni majenerali wajinga wajinga fulani hivi. Wanaangalia madaraka na maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
Burhani alitaka daglo na kikosi chake waingie/wawe chini ya jeshi la nchi,daglo akaona atakua mdogo,hapo daglo ndiyo mpumbavu,Hana uzalendo,huwezi kuwa na majeshi mawili ndani ya nchi
 
Back
Top Bottom