Wanajihad waviteka visiwa vingine viwili Msumbiji

Sergei Lavrov

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
6,873
2,000
Wanajihad kaskazini mwa Msumbiji waliviteka visiwa viwili vidogo vya bahari hindi na kutishia usafiri wa baharini katika eneo hilo ambapo mradi wa gesi yenye thamani ya mabilioni ya madola unajengwa kulingana na wakaazi.

Hatua hiyo ndio ya hivi karibuni katika mkoa huo wa Cabo Delgado katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.

Inajiri mwezi mmoja baada ya Wanajihad hao wanaohusishwa na kundi la Islamic State kuteka mji wa bandari ya kimkakati ya Mocimboa da Pria, ambayo ilitumika kusafirisha mizigo ya ujensi wa mradi huo wa gesi.

Mashahidi waliambia chombo cha habari cha AFP kwamba wapiganaji hao waliteka kisiwa cha Mecungo na Vamisse siku ya Jumatano usiku.

''Waliwasili usiku wakiwa katika boti ndogo ya kuvulia samaki . walitoa watu katika nyumba zao na kuzichoma'', alisema mkaazi mmoja ambaye alikuwa ametoroka katika kisiwa cha Mocimboa da Pria.

Jeshi la Tanzania lakana kujihusisha na mzozo unaoendelea Msumbiji
Viongozi wa nchi jirani wajitolea kusaidia Msumbiji kukabiliana na ugaidi
Msumbiji yapigania kukomboa bandari iliyotekwa na IS
''Hawakumdhuru yeyote , walitoa maagizo ya watu kuondoka katika kisiwa hicho'', alisema kwa njia ya simu , akiongezea kwamba ameelekea ndani zaidi ya mji huo wa madini wa Montepuez baada ya kuvuka hadi kisiwani humo kwa kutumia boti na baadaye kusafiri kwa basi hadi Montepuez.

Visiwa hivyo vilikuwa vikiishi watu waliopoteza makaazi yao waliotoroka vijiji vya eneo la bara ambalo mashambulizi yameongezeka.

Shahidi mwengine anasema kwamba kabla ya nyumba hizo kuchomwa , Wanajihad hao walifanya mkutano na wakaazi na kuwaagiza kuondoka katika kijiji hicho.

''Walitukusanya pamoja na kutuambia kutoroka iwapo tunataka kuishi. Nadhani kila mtu aliondoka katika kisiwa hicho'' , mtu mmoja ambaye hakutaka kutambulika alisema.

Wapiganaji hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio tangu 2017, na kuwawacha watu 250,000 bila makao huku wakiwaua watu 1500.

Vikosi vya serikali bado vinakabiliana na wapiganaji hao ili kuikomboa bandari ya Mocimboa da Pria tangu Agosti 12.

Mashambulio ya wapiganaji hao katika Cabo Delgado yamesababisha uharibifu mkubwa wa barabara kati ya mji mkuu wa mkoa huo Pemba na eneo lenye utajiri wa gesi la Palma kutopitika.

Usafiri wa baharini ndio uliokuwa umesalia kwa mizigo kupita.

Lakini kampuni ya mafuta ya Ufaransa Total , ambayo inawekeza dola bilioni 23 katika mradi wa uchimbaji wa gesi ilisema kwamba haitegemei tena bandari ya Mocimboa da Praia kama eneo la kimkakati na kwamba sasa imejenga vifaa vyake baharini , Total ilisema katika barua pepe ya maswali.

Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamekataa kuzungumzia kuhusu kutekwa kwa kisiwa hicho.

BBC swahili
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,234
2,000
In
Wanawazembea sana hao vibaka! Wakiendelea kupata nguvu watakuja kuwa tanzi hata kwa nchi yetu
Inaelakea kuna baadhi ya wanajeshi wa Msumbiji wana support kwa kificho harakati za magaidi hao - Jeshi la Msumbiji linashindwaje kumaliza/kukomesha ujinga huu, mpaka wafikie hatua ya kuomba msaada kutoka kwa majeshi ya SADC - wao wapo wapo tu wanasubiri kuhatarisha maisha ya wanajeshi wetu.

Binafsi siamini sana jeshi la Msumbiji,LEO watakwambia wamefanikiwa kuwa fyeka magadi, kesho unambiwa magaidi walifanikiwa kutumia speed boats na kwenda kuteka visiwa wakahitisha mkutano na kuwambia wakazi wahame ili wasije dhulika - inakuwaje magaidi waji amini kupita kiasi mpaka kufikia hatua ya kutumia boats za mwendo kasi, wakusanye wakazi wa visiwani na kuwahutubia kwa masaa -hivi inaigia akili kwamba Jeshi la Msumbiji lilikuwa halijui kinacho endelea kwa muda wote huo, je, jeshi la Msumbiji halina Helicopters gunships, fast military patrol boats na jet fighters vitu ambavyo ni vyenye umuhimu wa kipekee kukabiliana na magaidi kwa haraka.

Jeshi la Msumbiji linijichunguze kwanza na kuchukua hatua ya kinidhamu kabla hawaja chelewa, mambo yanavyo onekana ni dhahili kuna baadhi ya wanajeshi wana support vurugu zinazo endelea kaskazini mwa Mikoa ya Msumbiji yenye utajiri mkubwa wa gesi, binafsi siamini kama waasi hao ni wa kikundi cha Wasilaam wenye itikadi kali, madai hayo ni ulaghai mtupu - sio siri kwamba kundi hilo linakuwa funded na western Intel agencies ndio maana mwaka Jana alikatwa mzungu kutoka Afrika kusini aliye kuwa anawalipa mishahara waasi hao na kuwapatia silaha.

One more thing, kama kampuni za Merikani ndio zingekubaliwa kuchimba gesi ya Msumbuji nawahakikisheni kwamba wala tusingesikia kujitokeza magaidi wa kuchonga tu i.e wa uongo na kweli - lakini kwa kuwa kampuni iliyo fanikiwa ni ya Kifaransa (Total) basi the so called magaidi wata hakikisha Wafaransa hawafanikiwi katika Project ya gesi kwa kuwakosesha amani ili wakate tamaa.
 
Kobane

New Member
Sep 15, 2020
1
45
Wengi wenu hamjui tunayayacomment kwan musiwazarau jeshi la msumbiji kushindwa kuwa zuia kwan mbona Kuna majeshi Bora Kama yanashindwa kuwazuia Sinai huko au jeshi la Nigeria mbona wameshindwa Tz tunaona Kama jeshi letu ni imara hao wakivamia kambi ya jeshi wenyew wanakimbia jeshi hao sio masihara sikieni tyu
 
ngulukizi

JF-Expert Member
Oct 10, 2018
245
1,000
Mimi jeshi la Musumbiji nililidharau baada kuja kuokoteza wale wamakonde wanaoishi site kule mbezi na kuwafanya wanajeshi kutoka hapo niliona kuna watu wanacheza na maisha ya watu
 
rommy shabby

JF-Expert Member
Jun 26, 2017
694
1,000
Point
Wengi wenu hamjui tunayayacomment kwan musiwazarau jeshi la msumbiji kushindwa kuwa zuia kwan mbona Kuna majeshi Bora Kama yanashindwa kuwazuia Sinai huko au jeshi la Nigeria mbona wameshindwa Tz tunaona Kama jeshi letu ni imara hao wakivamia kambi ya jeshi wenyew wanakimbia jeshi hao sio masihara sikieni tyu
 
Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
1,968
2,000
View attachment 1570148
Wanajeshi wenyewe ndio hawa chini wamevaa ndala,kuna siku hao magaidi watafika Maputo akili ndio zitawakaa vizuri.

Jeshi lipo kama kikundi cha mgambo,naona hata mishahara na posho zao wana zipata kwa tabu.
Kuna ile clip ina trend wanamuua mwanamke kwa kumhisi kuwa ni jihadist very unfair hili Jeshi kwa kweli image linayo potray kwa Jamii ni mbaya sana, inaonekana ni Kikosi cha wahuni tu Jeshi ovyo kabisa ilo
 
Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
1,968
2,000
Wengi wenu hamjui tunayayacomment kwan musiwazarau jeshi la msumbiji kushindwa kuwa zuia kwan mbona Kuna majeshi Bora Kama yanashindwa kuwazuia Sinai huko au jeshi la Nigeria mbona wameshindwa Tz tunaona Kama jeshi letu ni imara hao wakivamia kambi ya jeshi wenyew wanakimbia jeshi hao sio masihara sikieni tyu
Tanzania Jeshi letu ni imara sana ndio mana unaona hata Mkiru pamekuwa cleared mapema tu na Kambi ilijengwa kabisa, Sisi tuna assets sana Haswa upande wa rasilimali watu na vifaa, Nigeria wana lack rasilimali watu na jeshi lao limekaa kisiasa sana ndio mana unaona hata pirates tu wanawatesa

Tanzania People Defence Force(TPDF) au Jeshi la wananchi liko imara sana na ni miongoni mwa jeshi bora kabisa barani
 
uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
5,097
2,000
Wanajihad kaskazini mwa Msumbiji waliviteka visiwa viwili vidogo vya bahari hindi na kutishia usafiri wa baharini katika eneo hilo ambapo mradi wa gesi yenye thamani ya mabilioni ya madola unajengwa kulingana na wakaazi.

Hatua hiyo ndio ya hivi karibuni katika mkoa huo wa Cabo Delgado katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.

Inajiri mwezi mmoja baada ya Wanajihad hao wanaohusishwa na kundi la Islamic State kuteka mji wa bandari ya kimkakati ya Mocimboa da Pria, ambayo ilitumika kusafirisha mizigo ya ujensi wa mradi huo wa gesi.

Mashahidi waliambia chombo cha habari cha AFP kwamba wapiganaji hao waliteka kisiwa cha Mecungo na Vamisse siku ya Jumatano usiku.

''Waliwasili usiku wakiwa katika boti ndogo ya kuvulia samaki . walitoa watu katika nyumba zao na kuzichoma'', alisema mkaazi mmoja ambaye alikuwa ametoroka katika kisiwa cha Mocimboa da Pria.

Jeshi la Tanzania lakana kujihusisha na mzozo unaoendelea Msumbiji
Viongozi wa nchi jirani wajitolea kusaidia Msumbiji kukabiliana na ugaidi
Msumbiji yapigania kukomboa bandari iliyotekwa na IS
''Hawakumdhuru yeyote , walitoa maagizo ya watu kuondoka katika kisiwa hicho'', alisema kwa njia ya simu , akiongezea kwamba ameelekea ndani zaidi ya mji huo wa madini wa Montepuez baada ya kuvuka hadi kisiwani humo kwa kutumia boti na baadaye kusafiri kwa basi hadi Montepuez.

Visiwa hivyo vilikuwa vikiishi watu waliopoteza makaazi yao waliotoroka vijiji vya eneo la bara ambalo mashambulizi yameongezeka.

Shahidi mwengine anasema kwamba kabla ya nyumba hizo kuchomwa , Wanajihad hao walifanya mkutano na wakaazi na kuwaagiza kuondoka katika kijiji hicho.

''Walitukusanya pamoja na kutuambia kutoroka iwapo tunataka kuishi. Nadhani kila mtu aliondoka katika kisiwa hicho'' , mtu mmoja ambaye hakutaka kutambulika alisema.

Wapiganaji hao wamekuwa wakitekeleza mashambulio tangu 2017, na kuwawacha watu 250,000 bila makao huku wakiwaua watu 1500.

Vikosi vya serikali bado vinakabiliana na wapiganaji hao ili kuikomboa bandari ya Mocimboa da Pria tangu Agosti 12.

Mashambulio ya wapiganaji hao katika Cabo Delgado yamesababisha uharibifu mkubwa wa barabara kati ya mji mkuu wa mkoa huo Pemba na eneo lenye utajiri wa gesi la Palma kutopitika.

Usafiri wa baharini ndio uliokuwa umesalia kwa mizigo kupita.

Lakini kampuni ya mafuta ya Ufaransa Total , ambayo inawekeza dola bilioni 23 katika mradi wa uchimbaji wa gesi ilisema kwamba haitegemei tena bandari ya Mocimboa da Praia kama eneo la kimkakati na kwamba sasa imejenga vifaa vyake baharini , Total ilisema katika barua pepe ya maswali.

Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamekataa kuzungumzia kuhusu kutekwa kwa kisiwa hicho.

BBC swahili
Hao wanajeshi wa hiyo nchi wanamuua a helpless Woman kwenye ile video, kweli ni aibu sana! Wacha watekwe tu!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,013
2,000
In

Inaelakea kuna baadhi ya wanajeshi wa Msumbiji wana support kwa kificho harakati za magaidi hao - Jeshi la Msumbiji linashindwaje kumaliza/kukomesha ujinga huu, mpaka wafikie hatua ya kuomba msaada kutoka kwa majeshi ya SADC - wao wapo wapo tu wanasubiri kuhatarisha maisha ya wanajeshi wetu.

Binafsi siamini sana jeshi la Msumbiji,LEO watakwambia wamefanikiwa kuwa fyeka magadi, kesho unambiwa magaidi walifanikiwa kutumia speed boats na kwenda kuteka visiwa wakahitisha mkutano na kuwambia wakazi wahame ili wasije dhulika - inakuwaje magaidi waji amini kupita kiasi mpaka kufikia hatua ya kutumia boats za mwendo kasi, wakusanye wakazi wa visiwani na kuwahutubia kwa masaa -hivi inaigia akili kwamba Jeshi la Msumbiji lilikuwa halijui kinacho endelea kwa muda wote huo, je, jeshi la Msumbiji halina Helicopters gunships, fast military patrol boats na jet fighters vitu ambavyo ni vyenye umuhimu wa kipekee kukabiliana na magaidi kwa haraka.

Jeshi la Msumbiji linijichunguze kwanza na kuchukua hatua ya kinidhamu kabla hawaja chelewa, mambo yanavyo onekana ni dhahili kuna baadhi ya wanajeshi wana support vurugu zinazo endelea kaskazini mwa Mikoa ya Msumbiji yenye utajiri mkubwa wa gesi, binafsi siamini kama waasi hao ni wa kikundi cha Wasilaam wenye itikadi kali, madai hayo ni ulaghai mtupu - sio siri kwamba kundi hilo linakuwa funded na western Intel agencies ndio maana mwaka Jana alikatwa mzungu kutoka Afrika kusini aliye kuwa anawalipa mishahara waasi hao na kuwapatia silaha.

One more thing, kama kampuni za Merikani ndio zingekubaliwa kuchimba gesi ya Msumbuji nawahakikisheni kwamba wala tusingesikia kujitokeza magaidi wa kuchonga tu i.e wa uongo na kweli - lakini kwa kuwa kampuni iliyo fanikiwa ni ya Kifaransa (Total) basi the so called magaidi wata hakikisha Wafaransa hawafanikiwi katika Project ya gesi kwa kuwakosesha amani ili wakate tamaa.
Paragraph yako ya mwisho ndiyo ilitakiwa iwe mchango wako pekee. Hawa siyo waasi au sijui magaidi wa kawaida. Wangekuwa wapiganaji wa kawaida mbona ni rahisi kabisa kuwamaliza? Tena jeshi la Msumbiji lina uzoefu na mambo ya vita. Wangekuwa wapiganaji wa kawaida mbona hata askari 2000 wakiongozwa na mizinga, vifaru na silaha ndogo ndogo wangewavurumisha kwa muda wa wiki moja tu? kuna nchi kubwa kabisa inawapa mafunzo na zana. Tatizo ni mali iliyoko chini. Nchi nyingi za dunia ya tatu zilizogundua kuwa raslimali zimeishia kuwa kama zimelaanika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom