Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,092
- 43,265
Ni matumaini yangu wenye hekima watatawala katika kuamua kuua au kuacha vitu viharibiwe tu ikibidi. Kama bado wanafikiria kutetea mali na kuua miili basi wafikirie tena. Dunia haijawahi kufanya kumbukumbu ya mali zilizoharibiwa, majumba au ofisi zilizochomwa moto. Hakuna minara ya kumbukumbu za majengo yaliyoharibiwa katika vurugu nchi yoyote! Tutaona kama ndugu zetu hawa somo hili wanalielewa au bado wanaendelea kulinganisha uhai wa watu na mabasi ya mwendo kasi...
Lakini, vyovyote ilivyo wao waendelee kupanga wanachopanga, na sisi tunaendelea kupanga tunachopanga...