WanaJF naomba msaada wa busara toka kwenu tafadhali!!

Follow your way!! Even though siijui bcoz u ddnt mention it. Jiamn laana haipat sku iz ondoa izo fikra potofu

I have cried b'se of yur comment,, sio kwamba uko in my favour lkn umenikumbusha mengi sana
 
Pole sana,,my hubby aliwahi kutofautiana na mlezi wake aliyemlea kuhusu professional ohooooo.... Haikuwa kazi rahisi! Ila ukimya Wa kiasi.. Neno" nisamehe nimekosea* kusalimia bila kuchoka yamekuwa msaada sana hadi alipofanikiwa... Sasa yy ndiye shujaa na anawashauri wadogo zake( watoto) Wa mlezi wake.... Ila haikuwa kazi rahisi

Thanks sana sana Ms mol,, may God bless you..!! umenivusha hatua moja mbele
 
Umeandika kitu ambacho kimenigusa Sana Sana,Nimepitia ayo maisha yakuchaguliwa Kitu
cha kusoma, kufata upande ambao mlezi wangu alihitaji niufate kutokana na yeye kuona kwake ni sawa,kiukweli upande wangu sikuwa najinsi,Sababu aliniambia kuwa nisipomfata basi mimi na yeye tumemaliza na sikuwa na njia au mtu yeyote wakuweza kunisaidia kwa kipindi kile..

Ila leo Naweza sema amenivusha sana na amenisaidia sana kwa upande mkubwa sababu nilifata alichohitaji akanisaidia kwa moyo wote japo kwa maneno maneno,Ila alinishika mkono akanivuta mpka sehemu ivi..Baada ya apo nilijishika,nikajishika mpaka apa ambapo leo nipo,Nashukulu Mola kwa hilo ila ilianzia kwake..

Kwa upande wako ni,Kama unaona unaweza jisimamia,unaweza kusimama peke yako bila kuwa na msaada wake,kwangu mi naona ufate ndoto zako,Sisemi kuwa na uanze kumuoneshea jeuri Hapana muheshimu mpaka mwisho wa maisha yako,Sababu bado utahitaji ata msaada wa mawazo yake,Fata ndoto zako ufanye vizuri, ata yeye mwisho wa siku aone ni kweli alikuwa anakuzuia kitu bora kwako...Ila usisahau kumuheshimu na Kumtakia Mema kwa Mola..

"Thanks for your trust" as your signature says...
 
"Thanks for your trust" as your signature says...
Karibu, Karibu Sanaaa, Mi huwa nawapenda wazazi au walezi wale ambao wanapenda sapoti vizazi vyao, Chochote utakachohitaji ye yupo pale kukupa Msaada wake bega kwa bega na hawa ndo hutengeneza Kujiamini kwa Watoto wao, Trust Me Mzazi au Mlezi ndo huwa chanzo cha Mafanikio ya kujiamini kwa vijana wao.....Leo apo wewe unaona unakosa Kujiamin yote sababu ya Mlezi wako Kushindwa kukubari Unachotaka fanya....Inaumiza sana Yaani
 
Nimepitia uzi wote na baadhi ya ushauri uliopewa nikajifunza mengi sana. ..shukrani kwa kuleta huu uzi....kiasi umenigusa/unanihusu.

Kwa mtazamo wangu...mlezi wako anaishi maisha yake kwenye kivuli chako. ...anapata faraja kuona unafanikiwa, pengine ni maisha aliyataka lakini hakuweza kufanikisha sasa anaona kuyafanikisha kupitia kwako.

Ukimfuatilia anachosema utakuwa unaishi kwenye ndoto zake na sio zako, huko mbeleni na wewe utakuja kurudia kosa la kutaka kizazi chako kumalizia ndoto zako ambazo hukupewa nafasi ya kuzikamilisha. ...

Simamia msimamo wako, ongea naye vizuri, maana naamini bado utamuhitaji katika maisha ya kukamilisha ndoto zako.

Kutokana na maelezo yako hapo juu ya ufaulu wako na kiwango chako cha elimu, naamini unajielewa na ushafikiria hasi na chanya zote za kukamilisha ndoto zako na ukaona uwezekano wakufanikiwa upo.

Maisha yakuishi kukamilsha ndoto za wazazi/walezi yameshapita. ..niwakati sasa watoto waruhusiwe ku kamilisha ndoto zao. ...ile dhana baba ni Dr lazima na mtoto awe Dr...imepitwa. ...kuna mambo mengi yakujaribu. ...

Simamia ndoto zako....naamini ipo siku utafanikiwa na watajifunza mengi toka kwako.

"Don't believe your doubters, prove them wrong"
 
Hujakosea kaka na ndicho kilichonifanya kuandika niloyaandika..!!!
Ushaur wako ni wa thamani sana kwangu,, thankx a lot...!!
 
Experience imenifunza kitu kimoja kikubwa mno, unapoamua kufanya yako especially baada ya kushauriwa na kukataa ushauri uliopewa kwa sababu unaamini 100% maamuzi unayofanya ni sahihi utafuatiliwa sana na wengine kukutakia mabaya. Wapo wengi wanaamua kufanya yao na wanaibuka on top, lakini mambo yakikiendea kombo na hauna moyo mgumu utatamani uhamie mars kama sio pluto.

Kama una moyo mgumu endelea na mipango yako ikikwama you will most probably be on your own na wengi watajitapa walikuambia. Cha muhimu sana hakikisha una mpango mwingine, plan B kama ikitokea unachofikiria sasa hakitafanikiwa.
 
Hahah,, thnkx kaka,, nacheka kama mazuri vile,, Lakini ujumbe umeniingia na nimekuelewa,,, Asante sana kwa mchango wako..!! Mungu akubariki
 
Just thanks kwa kupotea tyme yako kucomment hapa..!!

Kama ndo vile ulivyomaanisha kule chini kwenye ufafanuzi basI jitahidi tu uwe unatumia kiswahili maana ulichofafanua na ulichoandika mwanzo vinamkanganyo na makakasi kidogo

Ushauri pekee ni kwamba
Fanya kile ambacho kipo ndani yako maana ndo kinachoweza kustawi na kina misingi imara

Hakuna akujuae zaidi ya wewe mwenyewe
Watu wengi tunakoseaga familia au watu wanaotuzunguka mara nyingi wanatuelekezaga vyema na muda mwingine wanatupotosha maana wanadhania wanatujua zaida ya tujijuavyo. Simamia ndoto zako umri unakuruhusu na pia wakati wa kujenga future yako ni sasa aisee

Ukitaka kufanikiwa jitahidi kujiondoa karibu na watu uwapendao au ambao hautaki kuwaumiza hisia zao maana usipofanya hivyo utajikuta hausogei wala haukuzi ndoto zako

Na kurekebisha kidogo
Ukifanya jambo upendalo toka moyoni mwako sio tu unakamilisha ndoto zako bala unatimiza kusudi la MUNGU alilikuwekea ndani yako
Ukifanya kitu ambacho moyo wako unapenda inaonyesha dhaili kwamba unafanya kusudi uliloletwa duniani

MUNGU akusimamie na akupe hekima katika hali uliyonayo sasa ili usijekufanya maamuzi yoyote ambayo yatakuja kufanya ujutie baadae

Barikiwa sana

By shedymwai
 
Back
Top Bottom