WanaJF naomba msaada wa busara toka kwenu tafadhali!!

SHAMAC

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
1,343
3,561
Mimi ni kijana wa kitanzania, umri wangu ni kati ya miaka 24. Historia yangu ya maisha ni complex na rough kidogo lakini namshukuru Mungu bado naendelea kufaidi pumzi ya bure bila malipo,,...!!

Mwaka 2010 nilimaliza elimu yangu ya secondary na nashukuru nilifanya vizuri kabixa ( daraja la kwanza kwa point za juu mno.) na nikaendelea na high school nako nikafanya vizur pia ( daraja la pili la mwanzo.) 2013.

Siku zote huwa najiona katika kundi la watu wenye ndoto kubwa sana maishani, na sijawahi hata sku moja kuishawishi akili na moyo wangu kwamba haiwezekani.,,

Sio kwa sababu nimeweza kukariri maandishi then nikaulizwa swali na Necta nikajibu, Ndalichako akaona naweza.. HAPANA!!! hiyo haijawahi kunipa kiburi ht cku moja na kunifanya nikajiona niko tofauti na fulani...!!

Uwezo wa angalau kujiona naweza, ku imagine my future na kuishape future yangu namna nnavotaka iwe, cku zote ndo imekua motisha ya mimi kujiona NAWEZA... Bila hata kuhusisha hii miscellaneous education tunayoitokea Jasho miaka zaidi 17 hapa TZ.,

Nina mlezi aliyenifikisha nilipo ingawa si ndugu yangu na wala hatuhusiani kwa damu kwa vyovyote..!! kama msamaria mwema aliamua kunilea km mwanae, akanilisha, kanivika, kanilaza, kanipa elimu bora anayoamini ingeweza nisaidia..!!

Si nia yangu kueleza kwa undani sana mzazi/wazazi wangu walikua wapi all the way back..!! Sababu ya mimi kuja hapa kuomba busara zenu ni kwamba AM DOOMED RIGHT NOW,, Moyo wangu una huzuni kiasi kwamba nashidwa kujua lipi nifanye,,

Kwa sababu ya historia yangu nyuma cku zote nimekuwa mtu wa kufanikisha lolote lile ninaloamini lina manufaa kwangu. Hakuna mtu au kitu kilichoweza kusimama katikati ya njia niloamini inaweza kunifikisha mbali na hakuna aliyewahi kunisukuma nifanye kitu chenye manufaa kwangu mwenyewe..!!!..!!! Nilikua sterling na hero wa maisha yangu mwenyewe,,!!

Mkanganyiko unakuja pale mtu ninayemwamini, na aliyenifikisha hapa nilipo kujaribu kuweka kizuizi kwenye njia ninayoamini ni sahihi kunivusha next step.,, Tumetofautiana kimtazamo, hiyo ndo shida kubwa,,!! anataka na ananilazimisha niwe mtu wa aina flani na mimi mwenyewe nataka niwe flani tofauti na matakwa yake...!!

Njia hizi mbili ( yake na yangu) ni tofauti kabixa, ni sawa na kusema moja inaenda kushoto nyingine kulia..!! na zinatengeneza watu wawili tofauti kabixa, Ni njia ambazo ukiamua kuifuata moja bas utaiacha nyingine maisha yako yote, Na ukiamua kuchagua moja na ukaiishi huwezi kuwa opposite kwa vyovyote vile...!!

Kwa kifupi anataka niishi katika ndoto zake yeye..!! ( not to live in ma dreamz ), And thats one thing i can't allow it to happen NEVER,,!! Even once in a lifetime...!! "Kutoa msaada wa kumlea mtu haimaanishi umemnunua" ndicho nnachoamini..!! sijui kama niko wrong hapo..!! Still atakua independent person in all the means...

Tumefikia hatua mbaya sana na huyu mlezi wangu,, kiasi cha kutoongea mwaka mzima,,kiasi cha kuvualiana nguo na kupeana laana,, yani kwa kifupi ni stage mbaya sana nashindwa niiweke vip mnielewe...!!

Sina Amani kabixa na maisha nnayoishi sasa, sipendi kuishi niishivyo nataka Amani ya moyo, nataka furaha ya maisha.., Maamuzi yangu yananichapa viboko ss.,, Sio kwa sababu ni mabaya kwangu lkn kwa sabab hayajaafikiwa na mtu aliyekubeba kwa muda flan akakufikisha mahali, bado anataka akubebe lakini wew unataka utembee kwa miguu yako...!!

Wanadamu huwa ni watu wanaojudge wanachokiona na sio uhalisia jinsi ulivyo..!! hebu fikiria mtu yeyote anayeijua historia yangu anapoona nafanya mambo in my own interest,, not to the interest ya mlezi wangu mimi, lazima ataniona sina shukran 100%...,,

Mtaniona sina ubinadamu,, na pengine sina kweli.,, kwa sababu ya tabia yangu ya kufanya vitu nnavoamini ndani yangu kwamba ni sahihi na sio kutembea ndani ya mawazo na dreams za mtu mwingine tofauti..!!!

Kuna profession tofauti humu ndani, wanasheria, wanasakolojia, walezi pia, watu wenye mapenzi mema, na watu waliopitia mengi zaid yangu in life.... Pengine wanaweza kua msaada sana kwangu, sio kwa kunisupport tu ktka maamuzi yangu lkn wanaweza kutoa mwelekeo wa nn cha kufanya in this situation ingawa tayari moyo wangu umeamua na kuuzuia it's out of my control..!!!

Na ingawa nimeamua kuifata njia yangu napoteza ujasiri now,, Nahisi kama confidence inanikimbia kwa haraka sana,, ni kama moyo wangu umevunjika,, Najua siwezi kufata njia yake mpaka sasa lkn pia kutoaniamini na hii vita aloianzisha na mimi inanimaliza,, nashindwa kushika na kutembea ktka njia yangu perfectly,,

it's like am loosing hope!!.HELP ME PLZ!!!
I have friends and a lover but it's like Am lonely in a dense forest, hunted by something very dangerous...!!!

Naamini kwa kiasi kikubwa wengi wetu tunaishi ktka jamii moja ya kitanzania, mkoa mmoja, mji mmoja, na pengine hata mtaa mmoja,, Nyinyi ndo mtakua wa kwanza kuninyooshea mimi kidole, na macho yenu ndo yatakua ya kwanza mimi kuyakimbia,, Ndo mana nimekuja kwenu,, "Judge me the way you think i deserve to be judged in this situation."

UPDATED : njia ninayotaka niifuate mimi na njia ya mlezi wangu anayotaka niifuate nimeijibu kwenye comment zangu hapo chini,, page ya pili, ili thread isiwe ndefu sana ikawapa uvivu wakusoma...!!
 
mkuu ili upate ushauri au msaada mzuri zaidi ungejaribu kuweka wazi hizo njia mbili tofauti, yaani hyo anayokushauri mlezi wako na hiyo ya kwako, kama inawezekana. naimani hapo kwa experience za watu tofauti humu utapata msaada mzuri tu, mim ni moja ya watu niliosaidiwa sana na JF lakini nilikuwa muwazi
 
Dogo, unapokuja kuandika humu kwanza tambua sisi hatutaki matumizi mabaya ya lugha yetu pendwa ya taifa.

Andika maneno kama ambavyo inatakiwa. Mambo ya kutuandikia ki-facebook ukome kuanzia sasa hivi.

Kuandika kifacebook ni kuharibu lugha na kuitengenezea maana nyingine tofauti kabisa. Mfano matumizi ya maneno kama kabixa, cku

Kama utaamua kuandika Kingereza,Go ahead. Kama ni Kiswahili basi andika kilichonyooka ndugu.
 
Ndugu, kwanza Shukuru kwa kumpata mtu wa aina hiyo. Watu wa kukusaidia katika kipindi chote cha Elimu yako. Kuna wengine ndoto zao zinaozea kitandani kwa kukosa watu wa kuwashika mikono waweze kuyafikia yao malengo. Firstly, be thankful to her. Wengine wanaisaka hasa hiyo nafasi na wasiipate.

Pili, you are grown up enough to make decisions. Labda anachokitaka wewe ukifanye ni quietly different from what you want and wish to do. Huyo ni kama mzazi wako kabisa. Kama mzazi akikuambia hivi halafu ukaona siyo sahihi, kaa muelezee kuwa siyo sahihi na badala ingependeza iwe hivi. Vivyo hivyo kwa mlezi wako. Toa sababu za wewe kukataa jinsi unavyotaka yeye. Naamini atakusikiliza na kukuelewa.

Tatu, washirikishe wazazi wako halali. Waombe ushauri juu ya anachotaka kiwe mlezi wako. Wao huenda wakawa na mazuri zaidi ya kukuelezea na watakuwa mwanga wa kifanyike nini.

Mungu akubariki.

Ila una bahati asee, umekula mpaka nyama ya Mlezi wako? (Kidding)
 
Duh!nmejaribu tuu kupata picha in general kweli uko katika kipindi kigumu sana!I've been there,ingawa sijajua hasa hizo njia mbili ni zipi maana umeifunga sana hii nashindwa kuelewa kama ni kiupande wa imani(dini),au sijui labda mwenza(mke/mume),au labda professionalism...au sijui nini hata nashindwa kukisia ni upande upi hasa,kama ukiweza japo kuifunua kidogo itasaidia watu kutoa ushauri wao kwa uhakika.
 
Pole sana,,my hubby aliwahi kutofautiana na mlezi wake aliyemlea kuhusu professional ohooooo.... Haikuwa kazi rahisi! Ila ukimya Wa kiasi.. Neno" nisamehe nimekosea* kusalimia bila kuchoka yamekuwa msaada sana hadi alipofanikiwa... Sasa yy ndiye shujaa na anawashauri wadogo zake( watoto) Wa mlezi wake.... Ila haikuwa kazi rahisi
 
Mkuu maelezo yako yamevuta usikivu wangu vyakutosha ila......umenitaifisha akili uku nawaza njia mbili ambazo mmetofautiana ni zip????

Huenda mlezi yuko sahihi kuliko wewe kulingana na kile anachokitaka wewe ufanye au wewe uko right....

Sasa nashindwa kutia neno la ushauri kwa kukosa ukweli wa mambo.

Funguka mkuu usaidike humu ni zaidi ya shule.
 
Mkuu umeeleza jinsi ulivyo wewe kua unapenda kusimamia maamuzi yako sio ya kufuata ya mwingine na kwamba hukutaka kufuata njia ya mlezi wako kwa sababu unataka ndoto yako itimie.ushauri upi unao utaka maana hujaweka hizo njia mbili.mimi nahisi lengo lako sio kuomba ushauri bali tukutie moyo kwenye ndoto yako ya mafanikio.kila rakheli mkuu Mungu akutangulie ufikie malengo yako
 
Ndugu, kwanza Shukuru kwa kumpata mtu wa aina hiyo. Watu wa kukusaidia katika kipindi chote cha Elimu yako. Kuna wengine ndoto zao zinaozea kitandani kwa kukosa watu wa kuwashika mikono waweze kuyafikia yao malengo. Firstly, be thankful to her. Wengine wanaisaka hasa hiyo nafasi na wasiipate.

Pili, you are grown up enough to make decisions. Labda anachokitaka wewe ukifanye ni quietly different from what you want and wish to do. Huyo ni kama mzazi wako kabisa. Kama mzazi akikuambia hivi halafu ukaona siyo sahihi, kaa muelezee kuwa siyo sahihi na badala ingependeza iwe hivi. Vivyo hivyo kwa mlezi wako. Toa sababu za wewe kukataa jinsi unavyotaka yeye. Naamini atakusikiliza na kukuelewa.

Tatu, washirikishe wazazi wako halali. Waombe ushauri juu ya anachotaka kiwe mlezi wako. Wao huenda wakawa na mazuri zaidi ya kukuelezea na watakuwa mwanga wa kifanyike nini.

Mungu akubariki.

Ila una bahati asee, umekula mpaka nyama ya Mlezi wako? (Kidding)
Sasa naww mbona umechanganya lugha wakat ulimwambia achague kama kuandika kiswahili au kiingereza
 
Umeandika kitu ambacho kimenigusa Sana Sana,Nimepitia ayo maisha yakuchaguliwa Kitu
cha kusoma, kufata upande ambao mlezi wangu alihitaji niufate kutokana na yeye kuona kwake ni sawa,kiukweli upande wangu sikuwa najinsi,Sababu aliniambia kuwa nisipomfata basi mimi na yeye tumemaliza na sikuwa na njia au mtu yeyote wakuweza kunisaidia kwa kipindi kile..

Ila leo Naweza sema amenivusha sana na amenisaidia sana kwa upande mkubwa sababu nilifata alichohitaji akanisaidia kwa moyo wote japo kwa maneno maneno,Ila alinishika mkono akanivuta mpka sehemu ivi..Baada ya apo nilijishika,nikajishika mpaka apa ambapo leo nipo,Nashukulu Mola kwa hilo ila ilianzia kwake..

Kwa upande wako ni,Kama unaona unaweza jisimamia,unaweza kusimama peke yako bila kuwa na msaada wake,kwangu mi naona ufate ndoto zako,Sisemi kuwa na uanze kumuoneshea jeuri Hapana muheshimu mpaka mwisho wa maisha yako,Sababu bado utahitaji ata msaada wa mawazo yake,Fata ndoto zako ufanye vizuri, ata yeye mwisho wa siku aone ni kweli alikuwa anakuzuia kitu bora kwako...Ila usisahau kumuheshimu na Kumtakia Mema kwa Mola..
 
Bado kuolewa tu sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom