Mwalimu suala la kuwa na pesa mfukoni au kuwa na misingi ya kimahusiano imara na ndgu ni pana zaidi ya tujuavyo. Zimebaki familia chache zinazo jivunia umoja wa kindugu. Kunawa wamekuwa wamekuta ndg hawaelewani. Utaambiwa babako alizinguana na ndg zake kwasababu ya mali, hivyo tangu unazaliwa unakuta misingi ya mahusiano ilisha bomoka.
Si hivyo tu mwalimu, heshima ya Ndg kwako na upendo, utavipata kulingana na ulicho nacho mkononi/mfukoni. Tunaheshimiana kwa sababu na si vinginevyo. Ndg yangu kama unao ndg wanaoweza kukuamini wakakupa hayo manoti, inua macho juu mtukuze Mungu. Vinginevyo familia nyingi sasa mambo ni kama mbinguni kila mtu anabeba mzigo wake.