Wanajeshi watesa na kuua raia Monduli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi watesa na kuua raia Monduli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FreedomTZ, Aug 18, 2012.

 1. F

  FreedomTZ JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 1,086
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wanajeshi kadhaa wa JWTZ kikosi cha mizingo wanaoishi katika mji wa Monduli wamewatesa vijana wawili waliowatuhumu kwa kuwaibia vifaa vya elektroniki. Mateso hayo ya kipigo kwa siku mbili mfululizo yamepelekea kijana mmoja kati ya walioteswa kwa kupigwa mbele ya maafisa wa jeshi la polisi na UWT kupoteza maisha. Ndugu wa kijana aliyeuwawa wamekataa kuuchukua mwili hospitalini kwa ajili ya maziko hadi uchunguzi unaoridhisha utakapofanyika na wauaji kufikishwa mahakamani. Inasemekana kuwa askari hao wa JWTZ walitoa taarifa ya kuibiwa mali zao kituo cha polisi Monduli. Baada ya kuona polisi hawachukui hatua kwa haraka kama walivyotarajia ndipo walipoamua kujichukulia sheria mkononi.

  Hii ndiyo nchi ya amani na utulivu.
   
 2. J

  James lerombo New Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  oooh,,that is tz,,,,,,,,,,
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  wasionyeshe ubabe kwa raia, waende Syria na Iraq, wakirudi tutawaita wanaume!
   
 4. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Yaani hayo ni mambo ya kizamani kweli! Wanataka walete ishu za enzi hizo kwamba ukimuona mwanajeshi basi ujue ana haki ya kukufanya lolote. Wanaua walipa kodi wanaowalipa mishahara bila ushahidi wa kutosha. Hiyo sio haki kabisa. Naamini ni wanajeshi wachache waliokosa nidhamu ndio wanataka waharibu sura ya jeshi letu.
   
 5. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Maofisa wa UWT ni watu gani?
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,024
  Trophy Points: 280
  Wapi pedesheeee papaa mopao Lowassa?
   
 7. Salathiel m.

  Salathiel m. JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mi wala sishangai kabsaaaa,icho kitu n cha kawaida sana kwakua hata raia wanaua mwizi,wezi wangapi wameuwawa mitaani? Kwani wanajeshi ndo wanapenda wizi au ndo hawajachoshwa na uharifu? Aya mambo tumezoea hii itapunguza uharifu!
   
Loading...