Wanajeshi wanavyowadhalilisha wachimbaji kwa kuwapekuwa sehemu za siri Mererani

Huu ndo ujinga ambao unapigwa Vita .

Miaka zaidi ya 58 ya Uhuru bado Askari wetu wanatumia njia za 'kijima' kudhalilisha utu wa mwanadamu, eti tu kukaguliwa madini yasiibiwe.

Hivi body scanner security hazipo au hazifanyi kazi?
Kamatwa kule marekani ndipo utajua maana ya Uncle Sam
 
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia....
Hakuna sheria za nchi zinazomruhusu askari wa jwtz kumpekua mtu. Kisheria askari polisi ndiye mwenye mamlaka ya kumpekua mtu yeyote na anajua taratibu za upekuzi kwani amesomea.
 
Vipi wewe ulikaguliwa hadi 'mtaroni' huko Marekani?

Maana nasikia hao 'wajeda' ndicho wanachofanya huko mirerani!
Aha....Sina jibu kwa swali lako...ila pengine ukimuuliza baba yako mzazi na mama yako mzazi pengine unaweza kupata jibu lake kwa maana Kama katika maisha yao waliwahi kukaguliwa kihivyo...majibu yao unaweza kutuletea humu sijui wanasemaje...
 
Bongo kola mtu mjuaji, hebu leo ngoja nipate maarifa mapya.
Nakuomba uniwekee hiyo sheria inayomkataza askari wa jwtz kufanya upekuzi
Mfano unaingia kambi ya jeshi, inabidi jeshi wawaite polisi waje kukagua walioingia?
Hakuna sheria za nchi zinazomruhusu askari wa jwtz kumpekua mtu. Kisheria askari polisi ndiye mwenye mamlaka ya kumpekua mtu yeyote na anajua taratibu za upekuzi kwani amesomea.
 
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia...
Hujaeleweka hapa Hoja yako Kuu ni nini je, ni Mchimbaji Kuuwawa na Wanajeshi au Wanajeshi Kuwakagua Wachimbaji sehemu zao za Siri / Ikulu?
 
Kwa sababu wazungu wametupiga mtungo miaka mia nne bila mimba na bado wanaendelea. Kuna ile hasira ya miaka 400. Watuache waafrika tunyanyasane kivyetu kwa sababu ni drama zetu na ni matatizo yetu tukichoka tutaya solve wenyewe. Ila mzungu kumuua muafrika huwa kuna possibility nyingi ikiwemo ubaguzi. Jambo linalotia wasiwasi.
Yule dogo waliyemuuwa bado familia imewasusia?

Maana Askari mwafrika akiuaa mwafrika mwenzake sio habari, akiuaa mzungu sio habari, habari ni Askari mzungu kuuwa mwafrika dunia nzima itajua.
 
Kwa sababu wazungu wametupiga mtungo miaka mia nne bila mimba na bado wanaendelea. Kuna ile hasira ya miaka 400. Watuache waafrika tunyanyasane kivyetu kwa sababu ni drama zetu na ni matatizo yetu tukichoka tutaya solve wenyewe. Ila mzungu kumuua muafrika huwa kuna possibility nyingi ikiwemo ubaguzi. Jambo linalotia wasiwasi.
Kuna Jamii isiyo baguzi duniani?
 
Kuna Jamii isiyo baguzi duniani?
Kwa hiyo kwa sababu hakuna jamii baguzi duniani ndio tuhalalishe uonevu wa mtu mweusi. Kwamba ikitokea mtu mweusi kauliwa kwa sababu ya ubaguzi utasema askari asifungwe kwa sababu kuna ubaguzi jamii zote.
 
Hakuna sheria za nchi zinazomruhusu askari wa jwtz kumpekua mtu. Kisheria askari polisi ndiye mwenye mamlaka ya kumpekua mtu yeyote na anajua taratibu za upekuzi kwani amesomea.
Duh...aisee...kwanini usiende huko mgodini halafu uwaambie hao wajeda hayo...Rais Ana mamlaka kutumia JWTZ kwa maslahi ya taifa...Sasa wajeda wapo hapo na wana namna zao za kufanya ukaguzi...nenda kule halafu ukatae kukaguliwa...
 
Body scanners zilikuwepo, lakini zikahujumiwa na kulaumiwa kwamba zinatumia mionzi na hivyo kuhatarisha maisha ya wachimbaji. Kwa kuliona hilo, sasa mambo ndiyo hayo, vigorous physical search kwenye tundu lolote (sorry to say so)!
Kama scanner zilihujumiwa Basi no way out, ni mwendo wa kupekuana tuu, tukianza kuingiza siasa na haki za Nini sijui kwenye Hili tutarajie kusikia Kenya ndio muuzaji mkubwa wa tanzanite, Ila tuu ni muhimu kuwa na maafande wa kike
 
Huu ndo ujinga ambao unapigwa Vita .

Miaka zaidi ya 58 ya Uhuru bado Askari wetu wanatumia njia za 'kijima' kudhalilisha utu wa mwanadamu, eti tu kukaguliwa madini yasiibiwe.

Hivi body scanner security hazipo au hazifanyi kazi?
kabsaaa mkuuu kama unapata kvant pitia kwa mangi nakuja kulipa ile kubwaaa
 
Jeshi awafai kutumika kwenye masuala yanayohusu michanganyiko na Jamii. Wao wamefunzwa kuuwa na sio kulinda uhai . Kama wanakiuka taratibu za upekuzi sio utu. Mwanamke apekuliwe na mwanamke na mwanaume hivyo hivyo.
Wanawake wanapekuliwa na wanawake
Na wanaume tunapekuliwa na wanaume
 
Body scanners zilikuwepo, lakini zikahujumiwa na kulaumiwa kwamba zinatumia mionzi na hivyo kuhatarisha maisha ya wachimbaji. Kwa kuliona hilo, sasa mambo ndiyo hayo, vigorous physical search kwenye tundu lolote (sorry to say so)!
Walidai pia zinapoteza nguvu za kiume
 
Back
Top Bottom