Wanajeshi wanavyowadhalilisha wachimbaji kwa kuwapekuwa sehemu za siri Mererani

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
187
442
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia.

Wanajeshi hao ambao hivi karibuni wamemuua kwa kumtesa mchimbaji mdogo baada kumkuta na kipande cha Tanzanite mdomoni, wanalalamikiwa kuwadhalilisha wachimbaji kwa kuwafanyia upekuzi sehemu za siri kwa kuwavua nguo zote.

Hali kadhalika wanajeshi hao huwapwkuwa sehemu za siri wakina mama kwa kuwataka wapanue miguu wakiwa uchi wa mnyama jambo ambalo halikubaliki katika tamaduni za Mtanzania.

Ni vema rais Magufuli akafika Mererani ili kusilia kilio cha wachimbaji.
 
Wewe tulia kabisa kabisa taratibu za ukaguzi migodini unazijua

Mnataka kuendelea kuiba tu

Vijana wa JWTZ pigeni kazi kulinda mali za Taifa
Huu ndo ujinga ambao unapigwa Vita .

Miaka zaidi ya 58 ya Uhuru bado Askari wetu wanatumia njia za 'kijima' kudhalilisha utu wa mwanadamu, eti tu kukaguliwa madini yasiibiwe.

Hivi body scanner security hazipo au hazifanyi kazi?
 
Wewe tulia kbsa kbsa taratibu za ukaguzi migodini unazijua

Mnataka kuendelea kuiba Tuu

Vijana wa Jwtz pigeni kazi kulinda mali za Taifa
Mkuu nenda taratibu,TZ ni yetu sote, na Utu wa mtu ni kitu muhimu kuliko chochote kile.Taratibu za kumpekua mtu ni kwamba Mwanamke anapekuliwa na Askari wa kike halikadhalika Mwanaume anapekuliwa na Askari mwanaume.
 
Huu ndo ujinga ambao unapigwa Vita .

Miaka zaidi ya 58 ya Uhuru bado Askari wetu wanatumia njia za 'kijima' kudhalilisha utu wa mwanadamu, eti tu kukaguliwa madini yasiibiwe.

Hivi body scanner security hazipo au hazifanyi kazi?
Body scanners zilikuwepo, lakini zikahujumiwa na kulaumiwa kwamba zinatumia mionzi na hivyo kuhatarisha maisha ya wachimbaji. Kwa kuliona hilo, sasa mambo ndiyo hayo, vigorous physical search kwenye tundu lolote (sorry to say so)!
 
Duh! Kwa hiyo ni mwendo wa kupanua panua, ndio Afande au? Wa mererani tuthibitishieni haya madai ni ya kweli?
 
Wewe tulia kbsa kbsa taratibu za ukaguzi migodini unazijua

Mnataka kuendelea kuiba Tuu

Vijana wa Jwtz pigeni kazi kulinda mali za Taifa
Jeshi awafai kutumika kwenye masuala yanayohusu michanganyiko na Jamii. Wao wamefunzwa kuuwa na sio kulinda uhai . Kama wanakiuka taratibu za upekuzi sio utu. Mwanamke apekuliwe na mwanamke na mwanaume hivyo hivyo.
 
Yule dogo waliyemuuwa bado familia imewasusia?

Maana Askari mwafrika akiuaa mwafrika mwenzake sio habari, akiuaa mzungu sio habari, habari ni Askari mzungu kuuwa mwafrika dunia nzima itajua.
 
Mkuu angalia tu usijekuwa unatudanganya maana uongo sio jambo jema.
 
Body scanners zilikuwepo, lakini zikahujumiwa na kulaumiwa kwamba zinatumia mionzi na hivyo kuhatarisha maisha ya wachimbaji. Kwa kuliona hilo, sasa mambo ndiyo hayo, vigorous physical search kwenye tundu lolote (sorry to say so)!
Bila shaka 'walizihujumu' hizo mashine ..ili waendelee kuvuna madini kwa njia zisizo halali.
 
No body for any reason that can humiliate an Tanzanian.

The freedom, life and Security of our citizens is most considerable than money
 
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia.....
Sidhani kama jambo hili ni geni kwenye migodi mikubwa.Niliwahi kumsikia mtu mmoja aliewahi kufanya kazi Williamson Diomond mines ya Mwadui miaka hiyo ya ukoloni kulikuwa na upekuzi wa aina hiyo,sijajua teknolojia sasa hivi ikoje, labda wangeweza kutafuta njia mbadala ili kuwapunguzia adha wahusika.
 
Sipo upande wowote ila niseme kitu, wanajeshi kwanza swala la jinsia hawalifuati (nadhani wanachukulia watu wote ni sawa) yaani raia .
Kwa wale mliopitia jkt na jw nadhani mtakubaliana na mimi kuwa tochi hawaangalii wewe ni wa kike au wa kiume kama daktari ni wa kike atapima wote na kama ni wakiume pis atapima wote.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom