Waziri Biteko apiga marufuku ukaguzi unaodhalilisha utu Mirerani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Waziri wa Madini, Dotto Biteko amezitaka mamlaka zinazohusika na ukaguzi katika lango kuu la Madini ya Tanzanite Mererani, kuachana na upekuzi unaodhalilisha badala yake waangalie namna bora itakayolinda heshima na utu wa Binadamu.

"Kabla ya onyo hilo Askari wanaohusika na upekuzi ambao ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wanadaiwa kuwapekuwa sehemu za Siri wanawake huku wakiwavua nguo na kuwataka wachuchumae au kuinama huku wakiwachokonoa kwa vidole sehemu za Siri na wanaume kushikwa makende na sehemu za haja kubwa Jambo ambalo lililalamikiwa kuwa linadhalilisha utu wa Binadamu.

Aidha amesema serikali ipo katika hatua ya kuboresha shughuli za upekuzi katika lango hilo ikiwemo kufunga mitambo ya kisasa itakayoondoa malalamiko kwa wadau wa Madini wakati wa kutoka mgodini.

Hata hivyo waziri Biteko ameonya tabia ya baadhi ya wachimbaji kutorosha madini na kudai kuwa kuanzia sasa watakaokamatwa watapigwa picha na kisha picha zao kubandikwa katika ubao wa matangazo na kisha watapigwa marufuku kukanyaga eneo hilo kwa muda wa mwaka mmoja.

Biteko,alitoa kauli hiyo jana katika mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wakati kamati ya kudumu ya nishati na madini ilipotembelea katika mgodi huo kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea na Baadhi ya wabunge kupata fursa ya kuingia chini ya mgodi walipotembelea mgodi wa Franone mining unaomilikiwa na mchimbaji mdogo ,Onesmo Mbise .

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya kamati hiyo Biteko alisema serikali itaweka utaratibu mzuri wa ukaguzi wa wachimbaji katika eneo la lango kuu utakaowezesha wachimbaji kukaguliwa kwa haraka na bila kudhalilishwa na upoteza muda mrefu .

Alisema kwamba tayari serikali inakamilisha jengo la kisasa la ukaguzi litakalofungwa mitambo ya kisasa ambalo litatumika kufanya ukaguzi wa faragha kwa wachimbaji mbalimbali wanaotoka nje ya lango hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Madini na nishati ,Dunstan Kitandula amesema kamati hiyo imeridhishwa na namna serikali inavyopambana kudhibiti utoroshwaji wa Madini katika mgodi wa Madini ya Tanzanite , Simanjiro na kupelekea kuongeza kwa mapato yatokanayo na madini

Mwenyekiti huyo amesema ujenzi wa mifumo ya ulinzi kama ufungaji wa cctv camera na ujenzi wa barabara ya ndani inayozunguka ukuta, kumedhihirisha wazi kuwa mapendekezo yanatekelezwa vizuri.

"Baada ya kutembelea mgodi huu tumeridhika na udhibiti wa utoroshwaji wa Madini ila tunapendekeza adhabu Kali zitolewe kwa watu wanaoendelea na tabia ya utoroshwaji Madini"amesema

Aliongeza kwamba kamati imeridhishwa na ujenzi wa barabara ya ndani inayozunguka ukuta wa Mererani na itasaidia kuimarisha ulinzi.

Alisema kwamba kamati imeridhishwa na namna ukuta ulivyosaidia kuimarisha ulinzi na kuzuia utoroshwaji wa madini ya Tanzanite hali itakayosaidia kukuza mapato ya serikali .

Alisema kwamba wapo baadhi ya wafanyabiashara wanaojaribu kutorosha madini na kuikosesha serikali mapato lakini serikali inafanya namna ya kudhibiti hali hiyo.

“Sisi kamati tumejionea mambo mbalimbali yanayoendelea hapa kimsingi serikali inataka mapato kupitia kamati yetu tutajitahidi kuiambia serikali iweke mitambo ya kisasa eneo la lango kuu “alisema Kitandula

Naye mjumbe wa kamati hiyo,Christopher Ole Sendeka ambaye no mbunge was Simanjiro alikemea tabia ya baadhi ya wachimbaji wadogo kutorosha madini huku akisisitiza kwamba lazima wawe waaminifu kwa kuwa serikali inahitaji mapato.

Ole Sendeka alitoa wito kwa serikali kufungulia migodi mikubwa na midogo ili kukuza ajira na kukuza mapato ya nchi.

“Tunataka serikali ifungulie migodi mikubwa na midogo yote iliyofungwa ili tukuze ajira na serikali ipate mapato “alisema Ole Sendeka

Ends...

IMG_20210315_110629_458.jpg
IMG_20210315_111426_606.jpg
IMG_20210315_111632_936.jpg
 
Christopher Ole Sendeka ambaye ni mbunge wa Simanjiro, tunaomba maji yafungwe ndani ya ukuta wa mererani. Vijana wachimbaji wanateseka sana kupata huduma hiyo.

Kamati imekagua mapato ,ila huduma za kijamii ndani ya ukuta wa mererani hakuna. Mfano, maji safi na salama, vyoo, hospital, maduka, pia kamati hakusema chochote kuhusu kuendelea leseni kubwa iliyopo ndani ya ukuta ambayo hadi sasa haina mwekezaji .
 
Naona mawaziri wameshaanza kupata kauli zao!!juzi kati tumeambiwa wafungwa marufuku kufanya kazi binafsi na sasa tunaambiwa kuhusu ukaguzi hapo mgodini lazima ufuate sheria!....muda utaamua sio muda mrefu!
 
Kwani zile mashine za ukaguzi zikikuwa mbwembwe tu, si ajabu hata cctv hazifanyi kazi! Bongo nyoso
 
Naona mawaziri wameshaanza kupata kauli zao!!juzi kati tumeambiwa wafungwa marufuku kufanya kazi binafsi na sasa tunaambiwa kuhusu ukaguzi hapo mgodini lazima ufuate sheria!....muda utaamua sio muda mrefu!
Kama yule RC aliyesema viongozi watumie akili na sio nguvu jana...

Naona waanaanza kupata pata sasa
 
Back
Top Bottom