Wanajeshi wanavyowadhalilisha wachimbaji kwa kuwapekuwa sehemu za siri Mererani

Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia...
Pigeni chini huyu Magufuli. Inashangaza mnadhani atawaletea solution wakati ndiyo aliyewatuma. Jihamasisheni mpige kura kwa Lissu na kulinda kura kwa hali zote.
 
Huu mradi wafaidika ni wanajeshi. Yani kule jeshini ni mara mia sasa usipewe cheo upeqe nafasi ya kukinda pale getini. Mijamaa inapiga pesa hatari.
 
Jeshi awafai kutumika kwenye masuala yanayohusu michanganyiko na Jamii. Wao wamefunzwa kuuwa na sio kulinda uhai . Kama wanakiuka taratibu za upekuzi sio utu. Mwanamke apekuliwe na mwanamke na mwanaume hivyo hivyo.
Jeshi hawafundishwi kuua. Wao ni walinzi wa usalama, mali na mipaka ya nchi. Kuua ni matokeo ya anayedhibitiwa kuleta jeuri au hatari.

Unahisi kwa nini vitani kuna retreat, surrender, truce, prisoners of war (POWs).

Jeshi wanafundishwa kulinda uhai kuliko hata wewe unayejikuta huna hatia. Navy wanaweza okoa ajali za majini, air wing wanaweza kutoa usafiri wa anga kufika eneo la ajari au kuzima moto. Madaraja, uokoaji wa majengo yaliyobomoka, n.k yanafanywa na army. Hospitali za jeshi zipo na watoa huduma wa kijeshi wapo.
 
Pigeni chini huyu Magufuli. Inashangaza mnadhani atawaletea solution wakati ndiyo aliyewatuma. Jihamasisheni mpige kura kwa Lissu na kulinda kura kwa hali zote.
Hakuna mwana mererani atakaempa kura ili ateseke tena miaka 5
 
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia.

Wanajeshi hao ambao hivi karibuni wamemuua kwa kumtesa mchimbaji mdogo baada kumkuta na kipande cha Tanzanite mdomoni, wanalalamikiwa kuwadhalilisha wachimbaji kwa kuwafanyia upekuzi sehemu za siri kwa kuwavua nguo zote.

Hali kadhalika wanajeshi hao huwapwkuwa sehemu za siri wakina mama kwa kuwataka wapanue miguu wakiwa uchi wa mnyama jambo ambalo halikubaliki katika tamaduni za Mtanzania.

Ni vema rais Magufuli akafika Mererani ili kusilia kilio cha wachimbaji.
Nawewe ulipanuliwa kwa nyuma wakati wanatafuta mawe ya Tanzanite
 
Hakuna sheria za nchi zinazomruhusu askari wa jwtz kumpekua mtu. Kisheria askari polisi ndiye mwenye mamlaka ya kumpekua mtu yeyote na anajua taratibu za upekuzi kwani amesomea.
Wewe buda kama hujui kitu nyamaza unaonesha jinsi upeo wako ulivyo mchanga
 
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia...
Hayo ni machimbo ya madin toka enz na enz ayo mambo ypo km umejua leo bas pole kule unapekuliwa mpaka sasa waje wakyshtukie umelimeza jiwe wanakuua na kukufanyia upasuaj apo apo live bila chenga wanatafuta jiwe kwenye utumbo
 
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia...
Wao wapo kutimiza maelekezo na kufanya kazi wangeliwekwa police napo mngelalamika basi chagueni kati ya hao wanajeshi au police wapi ndo wasimamie rasilimali hizo maana wabongo hawakosi lawama

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Rais John Magufuli tunakuomba uje Mererani usikilize kilio cha wachimbaji wa madini ya Tanzanite wanavyoteswa na kudhalilishwa na wanajeshi wakati wa upekuzi katika lango la kuingilia...
mbona wao wanakaguliwa pia wakati wa usaili wao, na wanavua nguo zote. Hilo swala la kawaida sana mbona acha walinde mali hiyo
 
Haya ya sasa niliyaona wakati wa Nyerere.

Kama wahenga wasemavyo 'historia hujirudia'.

Sera za utawala wa Nyerere, hazikuruhusu uchimbaji wa madini kama ilivyo sasa.

Kulikoonekana kumevamiwa na wachimbaji wadogo, hima walipelekwa askari polisi 'kutawanya' na walipozidiwa lilipelekwa jeshi siyo kutawanya tena, bali kujenga kambi na makazi kabisa eneo husika.

Ilikuwa ikitokea hivyo wachimbaji wenyewe wali'surrender' na kuondoka 'bila kinyongo'.

Hayo niliyashuhudia Nyang'hwale na Buhemba.

Serikali ikiona raia wakivunja sheria za binadamu(wizi)kwa kisingizio cha kudai
kutendewa haki za kibinadamu, basi hutumia jeshi katika kudhibiti uhalifu huo.

Sasa tuseme kama kusingelikuwa na kisababishi( uhalifu), tungeyasikia yote haya?

Kila mmoja akitimiza wajibu wake hapatakuwa na lawama.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iliwahi kuletwa habari hapa JF, kuwa kuna mtu alificha risasi mbili sehemu za siri kwa ajili ya kufanya " assassination!!!
 
Sidhani kama jambo hili ni geni kwenye migodi mikubwa.Niliwahi kumsikia mtu mmoja aliewahi kufanya kazi Williamson Diomond mines ya Mwadui miaka hiyo ya ukoloni kulikuwa na upekuzi wa aina hiyo,sijajua teknolojia sasa hivi ikoje, labda wangeweza kutafuta njia mbadala ili kuwapunguzia adha wahusika.
Kupigwa miale mizito ya x-ray na kukaguliwa bila kupigwa hiyo miale kipi bora!!!
 
Ila nivema tukajaribu kutafuta haki ya Kila upande wakat was upekuz nakuzingatia hutu wa mtu
 
Bongo kola mtu mjuaji, hebu leo ngoja nipate maarifa mapya.
Nakuomba uniwekee hiyo sheria inayomkataza askari wa jwtz kufanya upekuzi
Mfano unaingia kambi ya jeshi, inabidi jeshi wawaite polisi waje kukagua walioingia?
Kwani hapo walipekuliwa walikiwa kambi ya Jeshi?
 
Back
Top Bottom