Wanajeshi wa Msumbiji wauawa na Wanamgambo

Wanajeshi wa Msumbiji wauawa na Wanamgambo

Wanakuwa miongoni mwa raia, wanatumia taarifa kwa wenzao kila kinachoendelea na wapo askari wa serikali wapo.
Wanaojua sasa wanajeshi wanafanya nini.

Wanamgambo wanavaa nguo kama raia, wanaficha silaha majumbani mwa raia au nyumba za ibada za raia.

Wanatumia usafiri wa raia wa kawaida, wanapewa mahitaji yao muhimu na raia.

Wavae sare za kijeshi na kukaa kambi rasmi za kijeshi uone itakuwaje.

Ina maana hata wanapoteka eneo serikali inapotuma askari wao wanaambiwa na raia watoa taarifa kila hatua walipo Askari wa serikali. Waasi wanavaa kiraia kisha wanashambulia ghafla, wakishafanikisha kuwadhibiti Askari wa serikali wanavaa rasmi kanzu, kombat I ya juu au suruali za kijeshi, na kuanika bunduki hadharani wanafanya propaganda online na kwenye media zingine.
Asante sana kwa ufafanuzi mkuu
 
Mbona Hata wa kwetu wanafyekwa tu sema mpambano unaendeleaj kimya kimya. Hata mme wa shagazi yangu amepangwa kwenda huko awamu inayofuata Sasa alikuwa anawaza ila Hana namna. Anasema walishapeleka vikosi Mara kadhaa majamaa yanafyekelea mbali
naskia askari wetu nao walichezeaga kichapo huko kitaya matwara
 
Hao jamaa wanavaa ndala lakini moto wao ni nyoko!
Wanajeshi na mafunzo yao, vifaa vyao, magari yao na intellijensia yao wanafyekwa kirahisi namna hiyo?

Roho zao zinafanana na hizo badala wanazovaa. Hakika wanayofanya sio kazi ya Mwenyezi Mungu. Dawa yao ipo jikoni.
Naona Msumbiji wanambwelambwela tu. Hawa wanatakiwa wafundishwe adabu kama wale waasi wa Congo
 
Huko kulikuwa na watu wanaitwa Bandido, hao jamaa walikuwa hatari sana wakiingia kwenye kijiji ni balaaa, hawana viatu mguuni Serikali ya Msumbji iliwashindwa. nakumbuka tulipambana nao sana, japo tuliwashinda lakini watu wetu wengi walilala kaburini. Nadhani msumbiji ijiangalie namna inavyoongoza watu wake hasa kuhusu haki na usawa kiuchumi,kisiasa, ajira n.k

Serikali ya Msumbiji wanajua kula rushwa tu. Ile kashfa ya rushwa ya kununua maboti ya uvuvi ambayo Rais alihusishwa, imeifilisi Msumbiji. Ndio maana jeshi lao ni dhaifu sana.
 
Nilifika Amboni Caves kutalii. Yule muongozaji nikamuuliza humu ndipo walikuja magaidi? Akajibu hapana, ni sehemu nyingine mbali na hapa. Nikamwambia lakini taarifa zinasema walikuja Amboni, akasema ni kule karibu na Kenya. Nikajua jamaa anajibu kimahesabu ili asiharibu utalii
Ni kweli, hawakuwa katika mapango ya Amboni hapo wanapoingia watalii!! Kuna mapango mengine yapo kama unakwenda border na Kenya.

Hayo ya Amboni hayakuguswa kabisa
 
Ulinzi wetu ukoje mkuu.

Tatizo wengi hatuoni kazi kubwa inayofanywa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Hawa watu tu kile kitendo cha kuvaa sare za majeshi husika na kuwa na vituo vyao vya kazi huo ni ulinzi tosha.

Hebu chukulia Rais atangaze leo "HAKUNA JESHI LOLOTE NIMEFUTA KUANZIA JESHI LA WANANCHI HADI MGAMBO, KILA AJILINDE YEYE NA MALI ZAKE". Hapo sasa ndio utajua umuhimu wa vyombo hivyo. Kwanza vibaka wote watajaa nyumbani kwako hakuna cha fensi ya umeme wala nini. Wanawake watabakwa hadharani mbele za watu, mitaa itatawaliwa na mateja na majambazi yatashika hatamu, hakuna mtu anaweza kufanya biashara, mabenki yatafungwa. Hata hao wanaolilia kuandamana hawataweza kwani wanaandamana kwa kuwa kuna amani.

Kwa hiyo, kile kitendo tu cha kusema POLISI, tayari inaleta picha fulani kichwani mwa mtu kuhusu usalama na udhibiti wa uharifu.

Jeshi letu ni imara na ndiyo maana liliwadhibiti hao washenzi pale Amboni na Kibiti wakakimbilia huko Copa Delgado Msumbiji
Hiyo tunaita Deterrance
 
Ni kweli mkuu, walikuwa mwambao wa Kenya huko mlipokuwa walikuwa wanaambaa kufuata mahitaji kwa wanananchi na kwenda hadi Tanga mjini. Aisee walikiona kilichomtoa Kanga manyoya shingoni.

Wengine walijaribu kujikusanya pori la Udzungwa maeneo ya Kidatu, usiombee njaa bhana si wakashuka na wananchi wakawashtukia wakatiwa mbaroni.

Kwa ujumla hawa watu ni shida sana.
Walikuwa raia wa nchi Gani?
 
Pili, waasi wanashirikiana na raia huku wakiishi miongoni mwa raia wa kawaida hivyo wanawafuatilia kirahisi jeshi la serikali bila kujulikana ni adui.
Hili hutokea pale Sirikali inapowakandamiza raia wake wenyewe, kuwadhulumu, kuwabagua, kuwanyima fursa, kutowajali hali zao za maisha. Serikali ikiwa ivi, basi raia nao huwaona waasi kuwa ni wakombozi wao. Huko kujifanya Al shabbab ni kuzuga tu, lakini kundi hilo lina watu ambao wamechoshwa na sirikali yao tu. Afrika inajulikana maandamano kwa mikono mitupu raia wataumia tu, sasa heri kwao kujiunga kwenye vikundi ivo kupambana kwa silaha.

Kitu kingine ivi vikundi ukitizama vimeanziaje, utaona tu sababu ndio ile ile, has to do with how the government is running the country
 
There you are, you nailed it. Ukitaka wengi wapone inabidi hizo hatua mbili hapo zizingatiwe. Hasa hiyo namba mbili kwani hata kama utakuwa na kikosi imara namna gani hauwezi kushinda.

Kumbuka kwa mfano, yale magaidi ya Westgate pale Kenya mara baada ya kufanya unyama, yalijibadili na kuwa raia wanaohitaji kuokolewa na yakatoka salama kabisa kwenye mstari wa wahanga. Imposters au mapandikizi ni adui namba moja na mbaya sana
Kwanini raia washirikiane na waasi? Unahitaji kujua jibu la swali hilo na kuanza kuishuhulikia hio sababu kabla haijawa too late.
 
Kuna mambo mawili makubwa hapo lazima uyaelewe kwanini wanamgambo wa waasi wanaonekana Wana nguvu.

Mosi, jeshi la Msumbiji ni dhaifu kwa Sasa.
Pili, waasi wanashirikiana na raia huku wakiishi miongoni mwa raia wa kawaida hivyo wanawafuatilia kirahisi jeshi la serikali bila kujulikana ni adui.

Hapo inatakiwa operesheni ya chini ya zuria nyumba kwa nyumba, sinagogi kwa sinagogi, unyama kwa unyama ....hapa nadhani umenielewa...
Tanzania ipo imara kwa sababu sisi ni wapendwa wa Mungu
 
Hili hutokea pale Sirikali inapowakandamiza raia wake wenyewe, kuwadhulumu, kuwabagua, kuwanyima fursa, kutowajali hali zao za maisha. Serikali ikiwa ivi, basi raia nao huwaona waasi kuwa ni wakombozi wao. Huko kujifanya Al shabbab ni kuzuga tu, lakini kundi hilo lina watu ambao wamechoshwa na sirikali yao tu. Afrika inajulikana maandamano kwa mikono mitupu raia wataumia tu, sasa heri kwao kujiunga kwenye vikundi ivo kupambana kwa silaha.

Kitu kingine ivi vikundi ukitizama vimeanziaje, utaona tu sababu ndio ile ile, has to do with how the government is running the country
Mkuu hii mada pana sana, hayo mengine yote ni sababu tu lakini msingi wa yote ni mambo ya kiiimani ya kidini.
 
Hii kauli ya kusema jeshi la mzumbiji ni dhaifu mlianza kuitoa baada ya hili kundi kuteka vijiji na baadae bandari.
Sasa hebu tupe ufafanuzi jeshi hilo ni dhaifu kivipi wakati nchi yote imetulia isipokuwa hapo Cado Delgado?
Unasema wanamgambo wanajificha miongoni mwa raia kauli ambayo sio kweli! Wanamgambo hao wanaua raia wa maeneo wanayoyateka na kuwajumlisha kundini wale wanaokubali kuungana nao

Hebu fafanua ni vipi wanajificha kwa raia na ni vipi jeshi la Mozambique ni dhaifu. Tumeona kule Nigeria boko haram nao wanavamia maeneo ya raia na kukimbia, kwanini jeshi la Nigeria limeshindwa kuwamaliza boko haram wakati jeshi hilo sio dhaifu kama la mzumbiji? Siku wakiteka vijiji na wilaya huku kwetu mtaanza kusema jeshi letu ni dhaifu
Alichomaanisha kiongozi ni kwamba

Hao wanamgambo ni kama hawana sare na wanakaa na raia hivyo kupigana nao ni vigumu kwa sababu hujui Raia nani na mwanamgambo nani
 
Mkuu hii mada pana sana, hayo mengine yote ni sababu tu lakini msingi wa yote ni mambo ya kiiimani ya kidini.
Dini ni mwamvuli tu. Lakini uhalisia ni vita baina ya serikali na wananchi waliochoshwa tu. Kama dini ingeanza Saudia Arabia kwenye kitovu
 
Wazalendo Wapumzike kwa amani.. naikumbuka Cabo Delgado ya '83 nikiwa huko.

Hawa jamaa zangu hawa wamesambaratika sana sababu ya rushwa. Ni bahati mbaya tunafikiria kuwa jeshi ni dhaifu, bila kujua jeshi lazima liwe na mahitaji yote muhimu ili lifanye kazi sawasawa
 
Back
Top Bottom