Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Wanajeshi 25 wa vikosi vya usalama Msumbiji wameuawa huku wengine 15 wakijeruhiwa baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Kiislamu katika kijiji cha Matambalale eneo la Muidumbe.
Kundi la maafisa wa kijeshi lilikuwa linashika doria eneo hilo wakati wa tukio Jumapili, kulingana na vyombo vya habari vya eneo.
Katika moja ya uvamizi, kanali na meja wamefariki dunia, vyanzo vimenukuu vyombo vya habari vya eneo.
Waathirika walikuwa sehemu ya kundi lililotumwa kuimarisha usalama baada mashambulizi ya wiki iliyopita ambapo nyumba zilichomwa moto na wakaazi kuuawa.
Bado jeshi halijathibitisha au kukanusha taarifa hizo.
Mashambulizi ya miaka mitatu yamesababisha mauaji ya zaidi ya 2,000 na kusababisha wengine 500,000 kutoroka makazi yao katika eneo la Cabo Delgado, kulingana na takwimu rasmi.