Wanajamvi wenye vyeti feki muichukue kama ilivyo japo inauma

ila ujue madaraka ni matamu sana,sijui kama watakubali kuachia eti kwasababu kuna watu miaka ya 90 walifail darasa la saba na wakarudia shule kwa majina yasiyo yao,na sasa wako serikalini kwa miaka 30 ,leo aje kuwatumbua.
Kama hujui miaka ya 80 hadi 90,suala la kurudia shule kwa style hiyo,lilikua ni common,kwasababu kufaulu kwenda secondary ilikuwa vigumu sana,kwahiyo mtu aliweza kurudia hata zaidi ya mara mbili ili afaulu na kuendelea na masomo,
Hiyo haihusiani mkuu maana huyo wa darasa LA saba naamini mpaka birth certificate ina jina hilo hilo alilorudia nalo shule,I think wao wanaangalia ufojaji(bandia)wenye kutumia vyeti ambavyo sio vyao(kaka,dada.,rafiki au ndugu)aliekwisha fariki au anafanya Kazi sector nyingine.
 
nashangaa


Jamani Death & Birth Cert. zimeanza kuwa dili si hata zaidi ya miaka kumi iliyopita. Watu walikuwa wanazaliwa hospitali kabisa tena za serikali lakini hawakuwa wanapewa hivi vyeti maana ilkuwa mpaka udai. Registrar wa vifo na vizazi alikuwaga bado usingizini.
tafuta sasa
 
MIAKA ya 80,na 90 kama watu walitumia mianya kujipenyeza wakafanikiwa waachwe tu wamalizie mikataba yao.Ya nini kuaibishana?.Hii itaathiri familia nyingi kiuchumi.Au watubuliwe kisirisiri kulinda heshima zao.
 
MAAJABU mengi yanaweza kutokea kwenye hili sakata.Hebu fikiria kama wewe ni mwalimu uondolewe kazini na wanafunzi wako uliowafundisha kwa bidii zote huko nyuma wakafaulu,leo hii wanakuona feki.Aibu zingine tufunike.
 
I know there was a time the system was technical know who but that is changing now, believe me that reading you did while preparing for your exams, that research you did for your essays it's a knowledge in your head and no body can still it from you.
still=steal
 
Wapendwa habari, Kwa wale ambao vyeti vyao ni feki hasa cha form four au form six na ni muajiriwa wa serikali, na wale wanaotumia majina na vyeti vya ndugu au marafiki zao, wanashauriwa kuacha kazi mara moja.. tena kwa uharaka..

Narudia acha kazi kabla hawajaja kukugundua.. ukaguzi umeanza kwa baadhi ya taasisi na mashirika ya umma..

Watu wanazimia hovyohovyo wakiulizwa kuhusu cheti cha form four na cheti cha kuzaliwa.

Kama cheti chako cha kuzaliwa nacho kimefojiwa ili kiendane na cha form four au form six yaani wewe UMEKWISHA KABISA.

Kama mfano wewe upo idara ya elimu na aliyekupa cheti au uliyempa cheti yupo idara nyingine mfano polisi au afya, basi nyote wawili mko hatarini kufungwa na kurejesha fedha zote za serikali ikiwemo mishahara ulizowahi kulipwa.

Kwa wale ambao nyumbani walikozaliwa wanajulikana kwa majina yao halisi mfano John J. Khamisi na kazini wanaitwa Petter S. Rutaza ndio hao haswaaa wanatafutwa kwa UDI na UVUMBA.

Umetengenezwa mtandao ambapo unaratibu majina na vyeti vyote. HAPA KAZI MOJA MTU MMOJA. Mtaarifu na ndugu yako inauma hasa kwa wale mnaowategemea Ndugu walio kwenye hii kasumba ila kwa kuwa tuliipenda wenyewe basi haina budi kuvumilia MUNGU yupo

Hii ni ngumu hasa wale wa enzi za nyerere na msee ruksa. Kila unapomaliza shule uliruhusiwa kubadili jina. Unakuta mtu ana jina la primary, form four, six na chuo. na hizo zote ni halali
 
Back
Top Bottom