Wanajamvi wenye vyeti feki muichukue kama ilivyo japo inauma

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,378
2,390
Wapendwa habari, Kwa wale ambao vyeti vyao ni feki hasa cha form four au form six na ni muajiriwa wa serikali, na wale wanaotumia majina na vyeti vya ndugu au marafiki zao, wanashauriwa kuacha kazi mara moja.. tena kwa uharaka..

Narudia acha kazi kabla hawajaja kukugundua.. ukaguzi umeanza kwa baadhi ya taasisi na mashirika ya umma..

Watu wanazimia hovyohovyo wakiulizwa kuhusu cheti cha form four na cheti cha kuzaliwa.

Kama cheti chako cha kuzaliwa nacho kimefojiwa ili kiendane na cha form four au form six yaani wewe UMEKWISHA KABISA.

Kama mfano wewe upo idara ya elimu na aliyekupa cheti au uliyempa cheti yupo idara nyingine mfano polisi au afya, basi nyote wawili mko hatarini kufungwa na kurejesha fedha zote za serikali ikiwemo mishahara ulizowahi kulipwa.

Kwa wale ambao nyumbani walikozaliwa wanajulikana kwa majina yao halisi mfano John J. Khamisi na kazini wanaitwa Petter S. Rutaza ndio hao haswaaa wanatafutwa kwa UDI na UVUMBA.

Umetengenezwa mtandao ambapo unaratibu majina na vyeti vyote. HAPA KAZI MOJA MTU MMOJA. Mtaarifu na ndugu yako inauma hasa kwa wale mnaowategemea Ndugu walio kwenye hii kasumba ila kwa kuwa tuliipenda wenyewe basi haina budi kuvumilia MUNGU yupo
 
MIMI NINA CHETI CHA FORM CHA MTU MWINGINE LKN CHETI HICHO SIO FEKI NA NIKAKITUMIA KUSOMEA CERTIFICATE SASA NIMEAJIRIWA SERIKALI JE WATAWEZA KUNIBAINI?MWENYE CHETI HICHO ALISHAKUFA NA HAKUWAIKUAJIRIWA SERIKALINI
Ndiyo wote mnaotafutwa, subiri zamu yako ifike...
 
MIMI NINA CHETI CHA FORM CHA MTU MWINGINE LKN CHETI HICHO SIO FEKI NA NIKAKITUMIA KUSOMEA CERTIFICATE SASA NIMEAJIRIWA SERIKALI JE WATAWEZA KUNIBAINI?MWENYE CHETI HICHO ALISHAKUFA NA HAKUWAIKUAJIRIWA SERIKALINI
MIMI NINA CHETI CHA FORM CHA MTU MWINGINE LKN CHETI HICHO SIO FEKI NA NIKAKITUMIA KUSOMEA CERTIFICATE SASA NIMEAJIRIWA SERIKALI JE WATAWEZA KUNIBAINI?MWENYE CHETI HICHO ALISHAKUFA NA HAKUWAIKUAJIRIWA SERIKALINI
Jisalimishe kabisa
 
Back
Top Bottom