Ndugu wana JamiiForum,nipo hapa kuwaomba ushauri wenu kwangu ni jinsi gani nitaweza kupata elimu ambayo niliikosa huko nyuma. elimu yangu tuseme ni ya ufundi kwani nilianza secondary mwaka kidato cha kwanza 1998 nikashindwa kuendelea ikabidi nipelekwe chuo cha ufundi Veta ( DAKAWA ) Morogoro nikamaliza 2000 nilisoma Plumbing and Pipefitting na pia Welding.
Kwa kipindi chote baada ya kutoka chuo niliajiriwa kwenye kiwanda cha nguo cha KTM Mbagala ambapo nilifanya kwa miaka miwili baadaye niliacha nikaa tu nyumbani sikuwa na wazo lolote la kujiendeleza basi ikabidi niingie kwenye magari nikaanza kufanya kazi ka kondakta ikafika muda niaacha ndipo nikachukuliwa Kaka yangu ktk ofisi yake nikawa kama messenger kwa kuwa nilikuwa nilikuwa najua pia kuendesha gari tena ya kila aina watu walikuwa wananituma hata kazi zao za familia kiasi kwamba nilijenga uaminifu mpaka ikawa zikitokea kazi za kwenda mikoani wananielekeza na nikifika nafanya kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi kwamba utadhani nimeisomea hiyo kazi.nimekuwa nikihudhuria ktk seminar mbalimbali mpaka ikafika mahali wakaniajiri mpaka leo na hapa nilipo sina cheti zaidi ya Veta na driving licence yangu mpaka naona aibu.hivyo kupitia haya naomba ushauri wenu iliniweze kuchagua masomo ambayo hayataniangusha ili niweze kupata cheti cha Form six nimeshaenda ktk kituo cha elimu ya watu wazima hivyo natakiwa nianze jan,2013
umesema kupata cheti cha 4m 6 ina maana cha 4m 4 ushapata au mikakati unayoiweka ni ipi?ndugu wana jamiiforum,nipo hapa kuwaomba ushauri wenu kwangu ni jinsi gani nitaweza kupata elimu ambayo niliikosa huko nyuma. Elimu yangu tuseme ni ya ufundi kwani nilianza secondary mwaka kidato cha kwanza 1998 nikashindwa kuendelea ikabidi nipelekwe chuo cha ufundi veta ( dakawa ) morogoro nikamaliza 2000 nilisoma plumbing and pipefitting na pia welding.
Kwa kipindi chote baada ya kutoka chuo niliajiriwa kwenye kiwanda cha nguo cha ktm mbagala ambapo nilifanya kwa miaka miwili baadaye niliacha nikaa tu nyumbani sikuwa na wazo lolote la kujiendeleza basi ikabidi niingie kwenye magari nikaanza kufanya kazi ka kondakta ikafika muda niaacha ndipo nikachukuliwa kaka yangu ktk ofisi yake nikawa kama messenger kwa kuwa nilikuwa nilikuwa najua pia kuendesha gari tena ya kila aina watu walikuwa wananituma hata kazi zao za familia kiasi kwamba nilijenga uaminifu mpaka ikawa zikitokea kazi za kwenda mikoani wananielekeza na nikifika nafanya kwa ufanisi wa hali ya juu kiasi kwamba utadhani nimeisomea hiyo kazi.nimekuwa nikihudhuria ktk seminar mbalimbali mpaka ikafika mahali wakaniajiri mpaka leo na hapa nilipo sina cheti zaidi ya veta na driving licence yangu mpaka naona aibu.hivyo kupitia haya naomba ushauri wenu iliniweze kuchagua masomo ambayo hayataniangusha ili niweze kupata cheti cha form six nimeshaenda ktk kituo cha elimu ya watu wazima hivyo natakiwa nianze jan,2013
Ikiwa kama elimu ya watu wazima itakusadia ni vyema ukaing'ang'ania. Mimi siyo mtaalamu sana wa elimu ya watu wazima. Ila mawazo ya pesa weka mbali ikiwa kama utadhamiria kubukua. Kaza msuli angalau upate cheti.
Kuna jamaa yangu aliajiriwa voda na kufanya kazi kama wewe. alibweteka, baadaye Vodacom wakadai vyeti vya elimu, jamaa akawa hana, kibarua kikaota nyani ikabidi arudi elimu ya sec. ya miaka miwili, na mwaka jana amehitimu Advanced Piploma in Procurement.