Wanaharakati wa Tanzania mko Wapi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati wa Tanzania mko Wapi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaJambazi, May 11, 2010.

 1. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 14,998
  Likes Received: 3,179
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kufuatilia mambo mbalimbali ya kimataifa yanayotendeka hapa Tanzania.

  Mfano tu ni huu mkutano wa WEF uliofanyika wiki iliyopita.
  Ivi mbona hamuonyeshi kama mpo hai??
  Mi nilitegemea mngekesha nje ya ukumbi wa mkutano na mabango yenu kama tunavyoona huko Ulaya na Amerika. Hata Kenya wanatushinda? au wako bright kuliko sisi nyie??
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wapo hai sana, waliomba kibali jeshi la polisi kufanya maandamano ( si unajua sheria za kitanzania) basi Kova akainuka na kusema si ruhusa atakayesogea atakiona cha moto jamaa wakaamua kufanya maandamano toka ofisini mpaka nje ya jengo moja silikumbuki na kufanya mkutano uliohutubiwa na Prof. Issa Shivji.

  Tatizo ni sheria zetu na uelewa wa polisi, hivi Kova ukimuambia unapinga mkutano wa WEF wakati zimemwaga posho za Usalama na Ulinzi unadhani atakuelewa au kukupa kibali cha maandamano, thubutu.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu wewe sio mwanaharakati?
   
Loading...