Wanafunzi wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu: Je, ukasome shahada na chuo gani?

Karibu sana.

Sijajua kwa vyuo vingine lakini kwa chuo chetu (UDSM) nimeona wanapata shida sana kwa sababu ya ugumu wa hesabu. Tofauti na IT, computer science inahitaji hesabu ngumu kidogo na kwa mtu ambaye hajasoma hesabu za A-level anapata wakati mgumu sana. Nimeona waliingia degree kupitia line ya kutoka diploma wengi wana-straggle sana. Ningemshauri kijana ambaye hajasoma A-level atafute alternative programme kama vile IT au information systems kama zipo. Computer Science core itamsumbua kwenye hesabu.

MM
Nashukuru kwani nilisha uliza swali la kama hesabu za diploma zinamtayarisha kijana kumudu course za CS na IT chuo bahati mbaya sikupata jibu. Lakini nilitegemea vyuo vikuu kama (UDSM na UDOM) wanaotoa Certificate na Diploma in CS wanafundisha hesabu za kutosha kwa matayarisho ya BSc in CS and the like. But nimekuelewa kwamba in general hali ndiyo hiyo. Ahsante.
 
Karibu sana.

Sijajua kwa vyuo vingine lakini kwa chuo chetu (UDSM) nimeona wanapata shida sana kwa sababu ya ugumu wa hesabu. Tofauti na IT, computer science inahitaji hesabu ngumu kidogo na kwa mtu ambaye hajasoma hesabu za A-level anapata wakati mgumu sana. Nimeona waliingia degree kupitia line ya kutoka diploma wengi wana-straggle sana. Ningemshauri kijana ambaye hajasoma A-level atafute alternative programme kama vile IT au information systems kama zipo. Computer Science core itamsumbua kwenye hesabu.

MM
Xamahan ngependa kuuliza kwa mtu km mm mnmesoma hkl....na ngepend kuxoma..kidogo mambo ya social science,public admnstratn,na...asa ngependa kujua field zake zinakuaje..km ilivo kwa walim kufany field zao kwa kufundxha katka shule mblmbl

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nina dogo kamaliza form six kapata two ya 10.. chemistry D.. biology C geography C Anaomba msaada wa kusomea course gani chuo.. nilipendekeza kati ya hizi

1. Bachelor science in human nutrition
2. Bachelor science in biotechnology and laboratory
3. Bachelor science in nutrition
4. Bachelor science in environmental health sciences

Naomba ushauri wenu maana kuwa wajuzi wa mambo haya..kazi ya hizo ni course gani ina soko la ajira?
Au kama kuna mdau anajua course nzuri kwa CBG naomba msaada wenu
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdogo wangu sio kazi ya chuo kikuu kumwandaa mwanafunzi kwa hesabu au lolote ili afae kusoma program anayoitaka. Chuo Kikuu kinapokea watu ambao wameshajiandaa kukabiliana na mikiki ya shahada na ndio mana munadahiliwa based qualifications. Kw ahiyo anayekuja na diploma yeye ndio anakua kakiambia chuo kwamba amejiandaa. Na hii ndio mana ninasema ni muhim vijana mufahamu kila programme munayoomba inahitaji vitu gani ili kuwasidia kufanya maamuzi sahihi badala ya kuchagua tu jina la programme.

MM
Nilimaanisha kwenye certificate na diploma courses za CS na IT ambazo zipo vyuo vya UDSM na UDOM nilitegemea dose ya hesabu wanayofundishwa ingekua ni matayarisho mazuri kwa wale wanaomaliza hiyo diploma yao (ya UDSM na UDOM) na kuamua kujiunga na degree courses za field hizo (CS na IT).
 
Tatizo ni kwamba ukifanya hizo programme ziwe na dozi kubw aya hesabu utakua umezibadilisha malengo maana hazitakua zimelenga kumpa mtu certificate na deploma bali zitakua kama ni foundation courses za degree. Kumbuka sio wote wanaokuja kusoma hizo programmes wanataka wenda degree. Wako wanaotaka certificate tu..na diploma tu. Sasa kuwaongezea mzigo wa hesabu kwa kigezo cha kuwaandaa na degree sio sawa. Pia sio wote wakitoka hapo lazima wakaendelee na CS au IT. Wanaweza kusoma certificate na diploma hizo lakini huko kwenye degree wakachepuka kwenye kitu kingine kabisa cha tofauti.

Kingine, kumbuka wanasoma certificate na diploma wengi ni wale amboa mitihani ya necta haikuwaendea vema (ikiwa ni pamoja na hesabu).. hivyo ukizifanya programme hizo kuwa na kile kilichowakimbiza sekondari basi nazo watafeli. Mimi nadhani kwa yule anayefanya diploma kama maandalizi ya kwenda degree ndio anatakiwa ajipe kazi ya ziada ikiwa ni pamoja na kuendelea kujiweka vizuri na hesabu yeye binafsi

MM
Nimekuelewa mkuu, itazingatiwa ukifika wakati wa kupeana ushauri na mhusika.
 
Back
Top Bottom