Jick
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 1,429
- 2,222
Umesema vema sana, je unadhani maswali hayo hayaulizwi?? Pia kwa fikra zako unadhani hakuna cha ziada zaidi ya hapo??Halafu ni kitu gani kitakufanya ama kukuzuia kumwanzisha shule mtoto wa miaka6? Huyu mtoto anajua vitu vingapi mpaka ufikie kusema hatoweza kufundishika? navyojua, wengi tulianza hatujuhi kitu sema tulikuwa na uwezo wa kufundishika na ndo maana tuko hapa leo.
Mtoto kushindwa kujibu ama kufahamu kujua jambo fulani katika umri wa miaka 6 hakumaanishi huyo mtoto hawezi kufundishika. Na ukitaka kuona mtoto anao uwezo wa kawaida wa kufundishika ni rahisi tu, muulize mama yake anaitwa nani? muulize jina na majina ya ndugu zake wa karibu, muulize mkono wake una vidole vingapi? muulize paka ana miguu mingapi. Mtoto yeyeto ukimuuliza vitu hivi ni lazima avijibu na inatosha kuelewa kwamba huyo mtoto ni mzima na ana uelewa wa kawaida kama binadamu kwasababu kikubwa ni kupima uwezo wake wa kukumbuka. Kama ubongo wake unaweza kutunza na kuweka kumbukumbu inatosha na hii ni kazi ya maswali mawili tu yanatosha, haya hayahitaji kufanywa kama intetview. Ni vitu vidogo vya kawaida, kutengeneza interview kwa ajiri ya hawa watoto eti ndo waandikishwe ni kutengeneza tatizo ambalo halina maana.
TAFAKARI
* Enzi zenu mlikuwa wangapi darasani??
* Wito wa walimu wako wa zamani unalingana na wa walimu wa Leo??
*Utayari wa wanafunzi wa Leo ni sawa na wenu wa zamani??
Niishie hapa, ila ukitaka mwanao aende la kwanza kisa tu ana miaka Sita, usitoe povu ukiona anahitimu pasipo kujua K. K.K kwa kiwango cha drs la 7