Wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza kufanyiwa interview!

Wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza kufanyiwa interview!

Askari Muoga

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
6,112
Reaction score
4,663
Wanajamvi hili jambo limekaaje? Watoto wanaoingia darasa la kwanza wanafanyiwa face to face interview na wakishindwa wanarudi nyumbani hata kama miaka inamfaa aanze darasa la kwanza.

Hivi mtu anamaliza chuo lakini kwenye interview anahangaika, sasa mtoto wa chekechea unamfanyia usahili wa ana kwa ana unampa maneno asome akishindwa anarudi ndo atawezaa?
 
Ni vizuri tu.

Sababu moja ni wazazi wengi huwa hawajali maendeleo ya watoto wao tangu wanapozaliwa na kusubiri waende tu shule muda ukifika. Hii itasaidia kuwapa majukumu wanayotakiwa kuyafanya na kujali watoto wao.
 
Hiyo imekaa ki ujinga zaidi watakao ingia darasa la kwanza kufanyiwa usaili !!!!
 
Ishu ni kweli watoto wanafanyiwa usaili na wakishindwa wanarudi nyumbani
 
Nimelisikia hili ila nafikiri hata kuset namna ya mtoto kuangaliwa ( kupimwa) kumewashinda. Ni maswali ya hovyo kabisa
 
Mimi naona kuzi enlarge hizo job description za walimu wakati majukumu ya kawaida kama mwalimu ni shida, kama ni kweli kusaili wanafunzi watakao ingia darasa la kwanza ?
 
Nimelisikia hili ila nafikiri hata kuset namna ya mtoto kuangaliwa ( kupimwa) kumewashinda. Ni maswali ya hovyo kabisa
kweli ndugu mtoto mdogo anafanyiwa usaili wa face to face eti ajue kusoma tena na walimu ambao sio wa nursery fuatilieni jambo ili ni kuwanyima haki watoto wetu
 
Halafu ni kitu gani kitakufanya ama kukuzuia kumwanzisha shule mtoto wa miaka6? Huyu mtoto anajua vitu vingapi mpaka ufikie kusema hatoweza kufundishika? navyojua, wengi tulianza hatujuhi kitu sema tulikuwa na uwezo wa kufundishika na ndo maana tuko hapa leo.

Mtoto kushindwa kujibu ama kufahamu kujua jambo fulani katika umri wa miaka 6 hakumaanishi huyo mtoto hawezi kufundishika. Na ukitaka kuona mtoto anao uwezo wa kawaida wa kufundishika ni rahisi tu, muulize mama yake anaitwa nani? muulize jina na majina ya ndugu zake wa karibu, muulize mkono wake una vidole vingapi? muulize paka ana miguu mingapi. Mtoto yeyeto ukimuuliza vitu hivi ni lazima avijibu na inatosha kuelewa kwamba huyo mtoto ni mzima na ana uelewa wa kawaida kama binadamu kwasababu kikubwa ni kupima uwezo wake wa kukumbuka. Kama ubongo wake unaweza kutunza na kuweka kumbukumbu inatosha na hii ni kazi ya maswali mawili tu yanatosha, haya hayahitaji kufanywa kama intetview. Ni vitu vidogo vya kawaida, kutengeneza interview kwa ajiri ya hawa watoto eti ndo waandikishwe ni kutengeneza tatizo ambalo halina maana.
 
Hata mtoto naweza kumfanyia interview hiyo sio shida.Unachopima pale ni his/her mental capacity.Shida ni kwamba is it justified.Kwa sasa watoto walio wengi wana "autism." Nini tatizo?Chanzo ni masumu mengi yaliyojaa kwenye environment yetu.Frankly kama hizo interviews zitakuwa fair watapata watoto wachache sana ambao wata-qualify.Hali ya watoto wetu ni mbaya sana.
 
Alafu afike la7 afanye mtihani wa kuchagua Hahahahaha elimu ya kivongo ni full comedy hiv ni ln viongozi wetu watakuwa cliac inatia hasila kwakweli
 
Mimi naona limekaa poa. Kwanza unawapunguzia mwalimu wa darasa la kwanza mzigo ukilinganisha watoto wanakua wengi kiasi kwamba hawezi kuwamudu wote na mazingira si rafki. Lakini pia ni bora ajue mapema kusoma, kuandika na kuhesabu kuliko amalize darasa la Saba hajui lkn lakushangaza utakuta amechaguliwa kwenda sekondari.
 
Elimu bure imewashinda kugharamia sasa wanatafuta namna ya kuwapunguza.

Hata hivyo, tupe kwanza chanzo cha habari hii ya kushangaza maana ni ngumu kuiamini.
Acha yale mawazo ya upande mmoja, interview huwa zipo siku zote na zilichagizwa hasa na KKK. Shule makini huwa wanafanya hivyo ili kuchukua watoto wenye misingi, shule zingine hywachukua tu halafu wakifika darasa la nne hadi saba hawajui KKK utakuja na povu hapa.

Halafu kutomuchukua haimaanishi asisome ila mrudishe Chekechea akapate misingi sitahiki.

Ukilazimisha kisa umri lazimisha aende mwendo wa gari bovu.
 
Wanajamvi hili jambo limekaaje? Watoto wanaoingia darasa la kwanza wanafanyiwa face to face interview na wakishindwa wanarudi nyumbani hata kama miaka inamfaa aanze darasa la kwanza.

Hivi mtu anamaliza chuo lakini kwenye interview anahangaika, sasa mtoto wa chekechea unamfanyia usahili wa ana kwa ana unampa maneno asome akishindwa anarudi ndo atawezaa?
Unawezaje kufananisha interview ya mtoto mdogo na mtu mzima tena katika kada tofauti??

Unatakiwa kujua mtoto hasomi kwa sababu ya umri tu. Uwezo wa mtoto ndio sababu namba moja, inawezekana mtoto akawa na umri mdogo lakini uwezo mkubwa au kinyume chake.

Kwa kifupi fuata na zingatia ushauri wa Walimu.
 
Nimelisikia hili ila nafikiri hata kuset namna ya mtoto kuangaliwa ( kupimwa) kumewashinda. Ni maswali ya hovyo kabisa
Share angalau maswali matano yaliyoulizwa tuyachambue.
 
kweli ndugu mtoto mdogo anafanyiwa usaili wa face to face eti ajue kusoma tena na walimu ambao sio wa nursery fuatilieni jambo ili ni kuwanyima haki watoto wetu
Huwa mkitusumbua sana tunawaacha wote.

Hapo ndo utakuta darasa la kwanza lina wanafunzi 150. 110 kati yao hawawezi hata kushika kalamu, hapo ndo tutakuuliza kazi ya Mwalimu wa Nursery unayemrejea hapa alifanya kazi gani.

MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.
 
Back
Top Bottom