Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Katika Website ya Law School of Tanzania (www.lst.ac.tz), imeandikwa kama tangazo kwamba: "Transcripts and Progress Statements for the Second Cohort students can be obtained from the School's Offices upon request." Swali kwa wale waliochukua, Je, transcripts zenu zimeandikwa Postgraduate Diploma in Legal Practice au just certificate of attendance? Msingi wa swali langu ni kwamba nilisikia kwamba wakubwa wa LST (Law School of Tanzania) walikuwa na kigugumizi cha kutoa award ya PDLP (Post Graduate Diploma in Legal Practice) kwa kuwa eti hakuna Diploma inayoweza kusomwa kwa mwaka mmoja. Jambo jingine ambalo lilikuwa linaleta utata ni kuhusu wahitimu kupata u-Advocate baada ya kumaliza masomo ya mwaka mmoja. Je, wakubwa wa LST wanasemaje juu ya huo u-Advocate ambao umetamkwa kabisa ndani ya Law School of Tanzania Act, 2007, No. 18 of 2007? Unapatikana au wanaenda kinyume na Sheria ya nchi?