Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,024
- 1,611
KAMATI ya tathmini ya mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST), imesema haijapokea uthibitisho wa kutosha kutoka kwa wanafunzi na walalamikaji wengine kuhusu tatizo la kufeli kwa wingi wanafunzi
Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti, Waziri mstaafu wa Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, ilipewa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi wake na jana iliwasilisha ripoti hiyo.
“Pamoja na wadau kuwasilisha malalamiko ya rushwa, uonevu au upendeleo katika utungaji au usahihishaji wa mitihani, hakuna ushahidi uliowasilishwa kuthibitisha tuhuma hizo,” alisema.
“Hata hivyo, kwa kuzingatia unyeti wa taasisi na wajibu ilionao ambao unahitaji uadilifu wa hali ya juu wa taasisi ili uweze kufuatilia mienendo yao. Tuhuma zikiendelea, kamati inashauri wakufunzi wanaolalamikiwa wahamishiwe katika idara nyingine za serikali ili kulinda taswira ya taasisi.”
Kamati hiyo ilibaini kasoro kwenye taasisi hiyo ni pamoja na kukosekana na huduma ya chakula katika eneo hilo, hosteli hususani kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Dar es Salaam hali inayowafanya waishi maisha magumu.
Pia miundombinu chakavu ambayo haijafanyiwa ukarabati muda mrefu ikiwamo kutofanya kazi kwa kangavuke (generator), uchakavu wa viti vya kukalia, mifumo ya sauti katika kumbi za mihadhara kutokufanya kazi vizuri, kumbi za mikutano kuvuja, mifumo ya Tehama na viyoyozi kutokufanya kazi.
Mengine ni baadhi ya vyumba vya semina kutokuwa na vifaa vya kazi kwa vitendo kama vile vizimba vya kujifunzia vinavyochangia kuathiri mfumo mzima wa uendeshaji wa mafunzo ya uanasheria kwa vitendo.
Kutokuwapo kwa mahakama ya kufundishia kwa vitendo ili kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa kushuhudia wenyewe mashauri yanayoendeshwa na mahakama, nyaraka zinazotegemewa na weledi katika kujenga hoja na utetezi.
Kuhusu malalamiko ya wanafunzi kwa Taasisi hiyo ya sheria nchini Dk. Mwakyembe alisema: “Kamati ililalamikiwa na wanafunzi kuwa LST kwa mujibu wa kanuni za rufani inatoa fursa kwa wanafunzi kukata rufani ndani ya siku 14 tangu kutangazwa kwa matokeo endapo hawakubaliani nayo, lakini wanafunzi wanadai kuwa fursa hiyo ni kiini macho kwa sababu mwanafunzi anaruhusiwa kukata rufani bila kuona karatasi yake ya mitihani iliyosahihishwa au bila kuelezwa swali gani alishindwa kujibu vizuri.”
“Pili, mwanafunzi anaruhusiwa kukata rufani akilalamikia ukokotoaji wa alama za ufaulu bila kuona karatasi yake ya mitihani iliyosahihishwa. Wanafunzi walilalamikia utaratibu wa LST kukaa na mitihani iliyokwisha kufanyika kwa zaidi ya miezi saba bila kutoa majibu kwa wanafunzi na kuwafanya wasijue udhaifu na ubora wao na namna ya kujipanga.”
“Walilalamikia mfumo wa utoaji matokeo kielektroniki kuwa unatoa matokeo yenye mkanganyiko, mathalani, kubadilika kwa alama za ufaulu na kusababisha taharuki kwa watahiniwa,”alisema na kuongeza:
“Kamati ilipokea malalamiko kuhusu kuwapo kwa mgongano wa kiutendaji ndani ya bodi ya uendeshaji wa taasisi katika kushughulikia rufani za wanafunzi. Bodi hiyo inathibitisha matokeo ya mitihani na majibu ya rufani kutoka kwenye kamati ya mafunzo na mitihani na wakati huohuo bodi hiyo inafanya kazi kama chombo cha mwisho cha maamuzi ya rufani.”
Mwenyekiti huyo alisema kamati iliona msingi wa hoja hizo za wanafunzi za malalamiko na kushauri ufanyiwe marekebisho.
“Kamati imeuona msingi wa hoja wa malalamiko ya wanafunzi kuhusu mchakato wa rufani dhidi ya matokeo ya mitihani yanayolalamikiwa kwamba haujakaa vizuri kwani haumpi haki mlalamikaji kujua kwa uhakika msingi wa malalamiko yake.
“Vilevile kanuni za rufani tajwa hazilazimu taasisi kushughulikia rufani na kutoa majibu kwa mwanafunzi katika kipindi mahsusi. Kuhusu chombo kimoja ambacho ni bodi ya taasisi kuidhinisha taarifa za rufani na wakati huohuo kuwa chombo cha mwisho cha rufani, kamati nayo inauona mkwamo bayana wa uwajibikaji.
“Hivyo inashauri kanuni ziweke sharti litakalomtaka mwanafunzi wa somo ambalo ameshindwa, kuainisha maswali ambayo alishindwa na alama alizopata. Pili, kanuni ziainishe muda mahsusi wa kushughulikia rufani na kutoa matokeo kwa mlalamikaji na ziweke sharti kuwa matokeo ya mitihani yakitangazwa, michakato yote ikiwa ni pamoja na rufani za mitihani ziwe zimekamilika.”
Kuhusu taasisi hiyo kukaa muda mrefu bila kusahihisha mitihani ya wanafunzi hao, Dk. Mwakyembe alisema: “Kamati haijaridhishwa na sababu za Taasisi na kushauri iondokane na utaratubu huo na imeshauri iimarishe mfumo wa Tehama ili kuondoa malalamiko. Pia ilishauri kutumia vitendo zaidi kuliko nadharia.”
Kamati hiyo ilishauri kwamba umefika wakati kwa serikali kuunda kwa haraka Baraza la Elimu ya Sheria nchini, sekretarieti yake, ofisi zake na kuipa bajeti yake ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake yote yaliyoainishwa kisheri ikiwamo kushirikiana na TCU kupandisha vigezo vya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na nne kwa watakaotaka kusoma sheria vyuo vikuu nchini.
Kamati hiyo iliundwa Oktoba 13, mwaka huu na Waziri wa Katiba na Sheria kwa ajili ya kufanya tathmini ya mafunzo yanayotolewa kufuatilia malalamiko ya wanafunzi kuwa kuna rushwa mbalimbali ikiwamo ya ngono na kufelisha wanafunzi bila sababu.
Chanzo: Nipashe