Wanafunzi Kibasila walala barabarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Kibasila walala barabarani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanajamiiOne, Sep 28, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni baada ya wenzaoo wawili kugongwa na kufa.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Barabara kuelekea Bandarini wametanda barabarani so waendao au watokau bandarini watafute njia mbadala.

  Acc. to Clouds FM
   
 3. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamekufa sasa hivi??? Wacha tusubiri tupate habari kamili unaweza kukuta kuna wanandugu wetu huko!
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Yaani hapa ndo wametangaza kuwa wamegongwa asubuhi hii. Nimesikia toka Clouds Breaking news ndo nikaona niwahabarishe so wenye watoto Kibasila please pateni confirmation juu ya usalama wa ndugu/ watoto wenu.
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Wadau mlio karibu na maeneo hayo, tafadhali tupatieni habari iliyokamilika kuhusiana na hili!
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Eneo hilo ni almaarufu kama machinjioni damu nyingi imemwagika eneo hilo na wahusika wamekaa kimya, natamani hao waliopoteza maisha wangekuwa ni watoto wa mkurugenzi wa Tanroads au mhandishi wa manispaa ya temeke.
   
 7. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #7
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  You are really burning!!!
   
 8. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, punguza munkari kidogo! Hata ingekuwa watoto wa hao uliowataja bado isingekuwa busara kuwaombea kifo. Watoto wamekosea wapi hadi wawajibishwe kwa madhambi ya wazazi wao? Tuwaombee kwa Mungu walihusika na msiba huu pamoja na ukweli kwamba bado hii habari ni tetesi!
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Swali ..

  je wamegongwa kwa uzembe wa dereva au???

  mungu aziweke roho zao mahari pema peponi Amen
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  tooo sad
   
 11. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Rip! Amen
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu Burn, hata mataa ya kuongozea magari hakuna. Na ukizingatia pale kuna makutano makubwa ya Mandela na Barabara ya Chang'ombe. Cha kusikitisha kabisa ni jirani tu na kituo cha polisi cha Kanda "Chang'ombe police". Matrafiki wapo busy sana pale wakikamata magari ya bandarini na ya shehena toka magodauni!!! Hivi huyo dereva hakupata kipigo?? Yaani pale mataa kupita ni nguvu yako na uvizie kama hakuna gari barabara ya Mandela ndipo uvuke. Wangeweka mataa ingesaidia sana.

  Rest in Peace wanangu.
   
 13. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usisahau kuwaombea watakaokufa in the future. Au usisahau kuomba mungu aeke muujiza ili asigongwe ten mtu mwingine eno hilo.
   
 14. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, kwa kuwa umekumbuka, ni vema tukaungana pamoja kuomba.
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kyachakiche,
  Huo ndiyo ukweli wenyewe. Pale hadi cku mtoto wa Kizito ATAKUFA na damu yake imwagike na heri kabisa Ubongo wake umwagike kwenye LAMI ndipo watakapopafanyia kazi.
  Kuna habari nilipata, nchi fulani kulikuwa kuna Express road moja ikitoka mjini. Kulikuwa na hizi konokono za barabarani na hivyo kuwepo NGUZO karibu. Jamaa walikuwa wakipenda sana KURUKA aneo hilo la bonde. Siku moja jamaa mmoja ambaye yeye na baba yake wana kipindi cha MAGARI kwenye TV na magazeti kama watangazaji, aliazima FERRALI na akachukua abiria na kufika eneo hilo, akapampu sijui hadi 300km/hr. Basi walirushwa na gari ikabadili mwelekeo na kwenda moja kwa moja kwenye nguzo za interchange. Ilikuwa huwezi amini kama walikuwa kwenye gari na gari sasa iko wapi. Abiria alikufa palepale na yule jamaa hadi leo nasikia kawa kama zezeta (no contact).
  Huwezi amini kuwa sasa hivi hilo eneo LIMETENGENEZWA.
  Nina kauzoefu kwa mambo ya barabara kwa mbali. Siku zote serikali huwa inafumbia macho mambo kwa kusema "ehh, subiri kidogo". Kama kukitokea ajali au watu KULALA barabarani basi hapo huwa wanatafuta solutions au hata kuelezea kwa nini iwe hivi na si vile. Ukikaa kimya na wao wanamezea.
  Safi sana wanafunzi wa KIBASILA. Mpiganie hadi hapo pajengwe kivuko cha barabara kwa juu na ziwekwe TAA na ikibidi hizo konokono zianzie hapo. This Machinjioni kwa kweli imedumu kwa muda mrefu saana na sidhani kama kujenga hiyo kitu hadi Mtu apande ndege kwenda kutafuta misaada waje watujengee....... Mie naweza kujitolea hata BURE kuchora michoro ya hizo INTERCHANGE so longer nipewe "idadi ya magari yanayopita, eneo gani linaweza kutumika kujenga hizo konokono" na sana sana itakuwa ni pesa kidogo sana kwa ajili ya kuwaona wataalamu waliobobea kwenye kudeal na maeneo hayo ya Machinjioni (Traffic Engineering).
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Tupo ukurasa mmoja mkuu, nadhani huu uzembe unasabishwa na kutokujali hizi damu, siku zitamwagika damu zinazowahusu wataweka taa na hizo konokono zitajengwa. Simnakumbuka barabara ya kinondoni karibu na msikiti wa mtambani, kila siku watoto wa makapuku walikuwa wanagongwa hadi walimu na wanafunzi wakaandamana lakini hawkusikilizwa ila alipogongwa anyewahusu tu tuta kama ukuta limejengwa, bado nasisitiza dawa ni kugongwa mtoto wa mkurugenzi wa tanroad, au mhandisi wa temeke tu.
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Mkurugenzi wa Tanroads hapa hana chake. Wee ombea watoto wa walioshika MPINI wa Tanzania. Si ulisoma alichofanya Zitto Kabwe kwenye ujenzi wa barabara ya Kigoma? Siyo kwenda Tanrods, bali kwenda Wizarani. Hapa ombea mtoto wa Waziri, Rais, mtu maarufu au Vigogo wa CCM. Unafikiri angelikuwa somebody Makamba au sijui Mkuchika ungeliona kazi. Na zaidi awe somebody Azziz wa Igunga Lowassa au Mkapa hivi ukiachilia mbali mtu anayetokea Bagamoyo ....... Hapo ungelisikia wakifoka kuwa ikibidi kula nyasi basi mtakula ila kivuko lazima kijengwe...

  Ila kuweka Taa, nafikiri wilaya ya Temeke wangeliweza kufanya wao peke yao bila kusubiri hadi Matonya waende Ulaya/USA/Asia kuomba TAA za kuongozea magari, zinazotengenezwa pale chuo cha DIT........
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu tena kuna taa za solar ambazo ni nzuri sana. Unaambiwa hata Zebra crossing pale ni kitendawili, bila kuchukua tahadhari kuwa kuna shule ya Sekondari Kibasila na ile ya Msingi. Tanzania ni njema, watendaji wabovu.
   
 19. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Wakuu Sikonge na Burn nimewasoma! Nashukuru kwa mawazo mazuri ingawaje na mimi sikuwa upande wa wasiotaka kuwajibika. Ila kama mzazi kuombea kifo kwa watoto inaniwia ngumu kidogo.
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Maamuzi mengine Mwalimu Nyerere aliwahi kusema yanahitaji 'moyo wa kiendawazimu' mkuu Kyachakiche. Sijambo la heri kuombea kifo kwa mtoto ila ni vyema pia kujua hata hao wanaomwaga damu zao kila siku ni watoto wa flani flani.
   
Loading...