Wanafunzi Kibasila walala barabarani

Wanafunzi Kibasila walala barabarani

Mkuu tena kuna taa za solar ambazo ni nzuri sana. .

Nadhani jiji hili kuna matatizo na hizi taa ebu chukulia:
Mwenge-Ubungo - taa haziwaki zinawaka kipande kidogo
Ubungo - Kimara - zinawaka kipande kidogo tu
Pale Magomeni kuna taa kama mbili tatu pale centre kwingine kote giza
 
Madenti Dar walala barabarani




Na Emmanuel Lengwa



28th September 2009







Kova1(4).jpg

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alhaj Suleiman Kova.



Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari (Kibasila), leo asubuhi wamefunga kwa muda barabara za Mandela na Chang'ombe kwa staili ya kulala barabarani, lengo likiwa kushinikiza eneo hilo kuwekewa matuta au taa.
Tukio hilo limefanyika kuanzia mishale ya saa 3:30 asubuhi na kusababisha foleni kubwa ya magari katika barabara hizo.
Mwandishi wa gazeti hili ameshuhudia wanafunzi hao wakiwa wamepanga mawe, majani na wao wenyewe kulala katika makutano ya barabara hizo, eneo ambalo ni maarufu kwa jina la Machinjioni, kutokana na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo hilo.
Hali hiyo ilisababisha magari kushindwa kupita, hali iliyoleta usumbufu mkubwa kwa watu waliokuwa wakiwahi makazini.
Baada ya wanafunzi hao kufunga barabara hizo kwa muda, gari la Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, FFU, lilifika eneo hilo, lakini wanafunzi hao wakaanza kulizomea huku wakipiga kelele za kutaka wasikilizwe.
Baadhi ya wanafunzi hao wamedai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa matukio ya wezao kugongwa mara kwa mara katika eneo hilo.
"Wenzetu kibao wamegongwa katika eneo hilo, wengine wamekufa na wengine wamekuwa vilema, tumelalamika sana lakini hawatusikii ndio sababu leo tumeamua kufunga barabara," akasema mwanafunzi mmoja kwa sharti la kutotaja jina lake.
Alasiri ilipomtafuta Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke ili kuzungumzia tukio hilo, hakupatikana mara moja kutokana na simu yake ya kiganjani kuita bila majibu.
Aidha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alhaj Suleiman Kova naye simu yake ilikuwa ikiita bila kujibiwa.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, wanafunzi hao walikuwa bado wakiendelea kufunga barabara hizo na hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyekuwa amefika katika eneo hilo.




CHANZO: NIPASHE
 
Poleni sana wafiwa.

Sadly, ni hadi watu wafe ndo utawasikia wakina Kova wakiingilia kati. Sheria zipo. watu wanalipa kodi. kuweka tu taa za kuongozea magari ni tatizo. si ajabu HAKUNA TUNACHOWEZA kufanya...
 
Tanzania tunatia aibu, hawa watoto wamefanya kitendo cha ujasiri ambacho sisi watu wazima tunashindwa kwa uoga. Hawa kama ni sample ya generation ijayo wanafaa kuungwa mkono.

Inabidi kila anayedhulumiwa haki yake achukue hatua mkononi ndiyo wenzetu walioko madarakani watashtuka, otherwise nawapongeza watoto wa shule.
 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Kibasila, Dar es Salaam wakiwa wakiwa katikati ya Barabara za Mandela na Chang'ombe, Dar es Salaam jana na kuzuia magari kupita wakishinikiza kuwekwa kwa matuta kutokana na wanafunzi wenzao kufa kwa kugongwa na magari katika barabara hizo ambazo hata hivyo hazina taa za kuongozea magari. (Picha na Zuberi Mussa)


Edmund Mihale na Makumba Mwemezi
WANAFUNZI wa Shule za Sekondari na Msingi Kibasila jana walifanya vurugu kubwa zilizohusisha kulala barabarani na kupiga mawe magari kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuweka matuta katika barabara ya Chang'ombe baada ya wenzao kugongwa na gari.

Vurugu hizo zilizoambatana na nyimbo na mayowe zilidumu kwa saa 5 ambapo zilianza 3: 00 hadi saa 8: 00 mchana, huku zikisababisha usumbufu mkubwa kwa wenye magari na waenda kwa miguu katika eneo hilo.

Wanafunzi hao walikuwa na mabango yenye ujumbe, 'Leo lazima kieleweke', 'tunataka haki zetu kama vile taa za kuongoza magari', matuta katika barabara ya Mandela na Changombe' na 'Tumechoka kuzika kuzika bila kuuguza'.

Mgomo huo ulioshirikisha zaidi ya wanafunzi 3,000 kutoka katika shule hizo na wakazi mbalimbali wa eneo hilo umetokea baada ya wanafunzi watatu na mkazi wa eneo hilo kugongwa huku mwingine akipoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu jana.

Mmoja wa shuhuda alisema kuwa jana asubuhi wanafunzi Consolata Kilaza na Winston Sango wote wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibasila, waligongwa na kupata ulemavu wa kudumu wakati wakisaidiwa kuvushwa na msamaria ambaye pia aligongwa.

Alisema Winston Sango alivunjika mguu na kukimbizwa katika Hopitali ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI) na Kilaza alivunjika mkono na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manispaa ya Temeke.

Shuhuda huyo alisema siku ya Septemba 25 mwaka huu katika makutano ya barabara hizo mwanafunzi mmoja wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Kibasila, Zubeda Walisinjo aligongwa na kufa papo hapo wakati akijaribu kuvuka.

Tukio hilo lilisababisha magari kutoka katika maeneo mbalimbali kupitia katika makutano hayo kushindwa kupita katika eneo hilo baada ya wanafunzi hao kufunga barabara na kurusha mawe kwa madereva waliokaidi amri.

Katika hali iliyoashiria kuwa wanafunzi hao walikuwa tayari kukabiliana na jambo lolote kuna wakati walishikana mashati na askari wa kutuliza ghasia.

Katika sakata hilo Mkuu wa Upepelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salamu, Bw Charles Mkumbo na askari wengine walikuwa na wakati mgumu kuwanasua askari kadhaa waliokuwa wameshikwa na wanafunzi ambao walikuwa wakimwokoa mwenzao alikamatwa na polisi hao.

Majira ilishuhudia msururu wa magari yakiwemo ya matatu yakiwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Polisi na Jeshi la Magereza yakiwa yamebeba askari aliokuwa wakienda katika vituo vyao vya kazi yakilazimika kutii amri ya wanafunzi hao.

Juhudi za Bw. Mkumbo kujalibu kuzima ghasia hizo hazikufanikiwa kutokana na wanafunzi kusisitiza kuwa walitaka mkuu wa mkoa aje kutoa kauli.

Vurugu hizo zilitulizwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Lugimbana aliyefika katika eneo hilo kama Kaimu Mkuu wa wilaya ya Temeke, ambaye aliitisha kikao cha dharula kilichohusisha uongozi wa wanafunzi, walimu na wanahabari kujadili suluhuisho la vurugu hizo.

Wakizungumza katika kikao hicho viongozi wa wanafunzi walisema ni jambo la kusikitisha kuona serikali inashindwa kuweka alama za barabarani katika barabara hiyo muhimu.

"Eneo hili limepewa jina la 'barabara ya machinjio' kutokana na umaarufu wake wa matukio kama haya, watu wengi wamekufa na serikali inafahamu, ilipaswa kuwa imeshalifanyika kazi," alisema mmoja viongozi wa wanafunzi hao kwa jazba.

Rugimbana aliwaahidi wanafunzi hao kulifanyia kazi suala hilo haraka na kuwaomba waonane leo saa tatu kwa ajili ya majibu ya hatua zitakazochukuliwa.
 
This is what we need! Vinginevyo itakuwa gumzo la kila siku. Viongozi wengi, kazi inayoendelea sifuri!!
 
Sasa umefika wakati watoto wetu wameshaanza kutufundisha sisi wakubwa wao njia sahihi za kudai uwajibikaji kutoka kwa wahusika. Sisi kama haturidhiki na jambo tumebaki kupiga domo tuu na kulalamika. Sasa tuaambiwa kuwa Action speaks louder than words.
Mengi hayaendi sawa maana viongozi wamelala, Tuamke kama wanafunzi wa Kibasila.
 
hayo matuta yatakuja kuwekwa mwaka kesho
Kuna ajali sana eneo hilo na pia kama ingekuwa katika Taifa lingine ajali za kila mara na mara waziri angekwenda na maji, tumechoka kuona watoto wetu, mama zetu wanakufa
 
hayo matuta yatakuja kuwekwa mwaka kesho
Habari nilizosikia ni kuwa serikali imefyata mkia kwa shinikizo la wanafunzi na RC amekubali matuta na alama zingine za barabara ziwekwe mara moja.
Kama nilivyosema Hawa watoto wametufundisha njia sahihi ya kulazimisha viongozi wawajibike sio kupiga domo na kulalamika maana kwao huo ni mziki mwororo.
 
Back
Top Bottom