Siku zote ufaulu wa mwanafunzi hutegemea jitihada zake mwenyewe, walimu pamoja na jitihada za mzazi, kama mwanafunzi hajawa tayari kufanya vizuri hizo jitihada za mwl.+ wazazi zinakuwa ni kazi bure katika kuleta matokeo chanya.
Kwa level hii (A' level) wazazi wengi wamekuwa wakijisahau kukakazania na kufuatilia maendeleo ya watoto wao wawapo shuleni na hata baada ya kurudi nyumbani, wanawaamini kupitiliza na kuwachukulia wameshakuwa na ufahamu wa kujiongoza na kujiassess wenyewe katika taaluma yao. Mwisho wa siku inafika siku ya mtihani wa mwisho mzazi hajui mwanafunzi amejiandaa vipi katika mitihani yake, matokeo yake ndio haya.
Na kuna wanafunzi wengine hawajitambui pia, pasipo purukushani purukushani za walimu mambo hayaendi, lakini hii pia inawaletea matatizo baadhi ya walimu wa kiume wanaofundisha shule za kike, mwl.akifuatilia sana maendeleo ya mwanafunzi mwisho wa siku wanafunzi huwageuzia kibao kwamba wanawataka kimapenzi (wanafunzi wasiojielewa)...Hivyo walimu pia wanaamua kuacha kuwabugudhi..
Sidhani pia kama kuwahamisha walimu hao ndio suluhisho,...kwamba walimu wote takribani 39 wamechangia ufaulu mbovu wa wanafunzi hao?? Sio kweli.
Wanaowazomea ni kutokujielewa tu, waliofeli wamefeli hivyo wasiwafanye hawa waliobaki hapo jangwani kujiona hawafai na kwamba hawapo sehemu sahihi...Wasiwafanye kutokujiamini.