Wanafunzi hawa waliopata zero wanaenda wap?

Wanafunzi hawa waliopata zero wanaenda wap?

instanbul

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2016
Posts
12,544
Reaction score
19,491
Yaan zero zaidi ya 100 yaan miaka 4 yote kapa aisee
Screenshot_20230129-122634.jpg
Screenshot_20230129-122714.jpg
 
Kuna diplomasia
Uhamiaji
Kurasini
ZIMEPAKANA HIZO
Watoto wanakula bangi kama chakula.
Mwalimu jichanganye wanakudunda... yaani hata class ukimshikia fimbo mwanafunzi wanakusaka nje ya shule wanakupiga hatari.

Ulizia walimu hapo
Kuna mmoja alimfata mwalimu akamwambia upo kwenye list kaa kwa kitulia usifatilie watu
.....nakaa maeneo ya karibu na hizo shule....

WATOTO NI WAHUNI KULIKO MAELEZO.
Tena nahisi hayo matokeo wamestandadaiz.halali halali hamna wa kupata 3 pale.na woote hao walimaliza la saba kwa ufaulu wa A$B
 
Hata aliyepata 4 ana utofauti gani na 0? Aaaaah
Kwahiyo mwenye "D" zote na "C" mbili atleast akapata division 4 ya point 26 ambayo anaweza kwenda chuo au kusoma kidato cha tano (5) huku ana-reseat ni sawa na wenye "F" zote?! 😳 we vipi?!

Division 0 maana yake ni Failure!.. ni kama la saba tu wala haesabiki kwenye kundi la waliosoma sekondari. (Huyu kapoteza muda tu..., yaan alienda kukua,kujifunza uhuni wa kijinga, kupata mademu, mabwana na kupata washkaji na kuvuta bange basi!)

Division 4 hana ufaulu wa kwenda kidato cha tano ila anaweza kusoma mambo mengine au kurudia shule na akafanya vizuri.
 
Halafu utakuta walikuwa wanapigwa fimbo kila siku badala ya kujua changamoto zinazowakabili na kwanini hawaelewi

Ni mjinga tu atakaefurahia haya ila kuna tatizo kwenye mfumo wote wa Elimu
Yaani hawajui kufundisha na waliofaulu wamekariri tu kila kitu
 
Back
Top Bottom