Wanafunzi 66,987 Wapangiwa Mikopo ya Tsh. Bilioni 215.3 na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB)

Wanafunzi 66,987 Wapangiwa Mikopo ya Tsh. Bilioni 215.3 na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
TAARIFA KWA UMMA

Dar es Salaam, 07 Novemba, 2025


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Ijumaa, Novemba 7, 2025 imetoa awamu ya pili ya upangaji mikopo na ruzuku yenye jumla ya wanafunzi 66,987. Idadi hii inajumuisha wanafunzi wafuatao:

Wanafunzi 43,562 wa shahada ya awali na wanafunzi 1,179 wa stashahada waliopangiwa mikopo kiasi cha TZS. 143.7 bilioni.

Wanafunzi 288 wa Samia Skolashipu waliopangiwa ruzuku kiasi cha TZS. 575 milioni.

Wanafunzi 230 wa Shule ya Sheria Tanzania waliopangiwa kiasi cha TZS. 1.5 bilioni.

Wanafunzi 21,729 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mikopo na ruzuku ya kiasi cha TZS. 69.4 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliotangulia.

Mpaka sasa HESLB imekamilisha upangaji wa mikopo kwa wanafunzi 202,227 yenye thamani ya Shilingi 641.8 bilioni kati ya Shilingi 916.7 bilioni zilizotengwa na Serikali kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Baada ya kukamilisha upangaji mikopo HESLB inawataarifu wanafunzi ambao hawajafanikiwa kupangiwa mikopo katika awamu zote mbili na wanaamini wana sifa za ziada ambazo hawakuweza kuziwasilisha wakati wa maombi ya mikopo wanashauriwa kukata rufaa. Dirisha la rufaa litafunguliwa Tarehe 10 hadi 17 Novemba, 2025.

Maelekezo ya kukata rufaa yanapatikana katika akaunti binafsi ya mwombaji (SIPA).

HESLB itaendelea kupanga mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo kwa kadiri itakapopokea matokeo kutoka vyuoni.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

1762579503900.png
 
Back
Top Bottom