Wanafunzi 24,000 Kutojiunga na kidato cha 5 sio inshu: Tupo busy tunatumbua MAJIPU

BUSAMUDA

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
612
358
Sioni Kama hiki kitu kinamsisitizo wowote kwenye hii awamu ya kutumbua MAJIPU na Hapa ni kazi tu.

Leo wanafunzi 24000 wanakosa nafasi wakati Elimu si Bure.

Je baada ya Miaka 4 wanafunzi wangapi watakosa nafasi?

Je mkakati upo ? wa kuhakikisha madarasa ya Kutosha yapo na walimu WA kutosha wapo?

Je ni kweli kipaumbele chetu kilikuwa

1. Maabara.

2. Elimu Bure.

3. Madawati.

4.

-------------------------------

Kati ya wanafunzi 393,734 waliokalia mtihani wa kidato cha nne nchini Tanzania mwaka uliopita,takriban wanafunzi 24,528 ambao walipita mtihani huo huenda wasijiunge na kidato cha tano mara moja kutokana na uhaba wa madarasa.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo wale watakaoathiriwa ,ni pamoja na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na taasisi za kiufundi zilizopo nchini humo.
Shule za uma hazitaweza kuchukua wanafunzi wote waliofuzu kuendelea na kidato cha tano.
Akitangaza matokeo hayo ya wanafunzi waliochaguliwa ,waziri katika ofisi ya rais anayesimamia utawala wa kijimbo na serikali za mtaa Bw George Simbachawene alisema: ''ni swala lenye changamoto lakini tunafanya juhudi kuhakikisha kuwa madarasa zaidi yanajengwa ili wanafunzi wote waliofuzu waendelee na masomo''.
Kulingana na The Citizen,amesema kuwa wanafunzi walioachwa nje ni pamoja na wasichana 6,789 na wavulana 17,739.
 
Mkuu hii nchi inasikitisha sana mtu ana div 3 ya point 22 na masomo ya sayansi kafauru vizuri,serikali sikivu ya walala hoi inaacha kumchagua kwenda adv,halafu mwingine anachaguliwa mwenye div 3 ya point 25 tena unbalanced combination tena
.Kweli hii ni serikali ya viwanda.
 
Dah.... Kuna majanga mengi ila wafuasi wa UKAWA ni janga lingine kwa Taifa...
 
Tukubali ukweli ,wana chadema uwezo wa kufikili upo chini sana , ila uwezo wa kupotosha upo juu sana
Hata kichaa anaweza kukwambia tairi limepasuka. Tuwe na tabia ya kusikiliza mawazo ya wengine. Si kila kitu tufanye siasa.
 
kwenda private ni uamuzi wa mtu na hii haisababishwi nakukosa nafasi shule za serikali,wote waliofanya vzuri wanatakiwa wapangiwe sehemu zao issue ya private ni uamuzi wa mtu

waliofanya vizuri wamepangiwa, hakuna hata mmoja aliyeachwa, na pia ungekuwa na akili nzuri ungejiuliza kwa nini katika nchi hii kuna private schools, zipo kwa ajili ya urembo au? nafahamu ugumu wa kuelewa hili hasa kama elimu na uelewa wako ni wa mashaka mashaka
 
Acha ujinga wewe na kuendekeza uvyama,mdogo wangu kaachwa na kafauru vizuri tu,ana three ya point 22 na combination imebalance tena PCM,halafu kaachwa wanachukuliwa wenye point 25 unbalanced combination.
 
Sioni Kama hiki kitu kinamsisitizo wowote kwenye hii awamu ya kutumbua MAJIPU na Hapa ni kazi tu.

Leo wanafunzi 24000 wanakosa nafasi wakati Elimu si Bure.

Je baada ya Miaka 4 wanafunzi wangapi watakosa nafasi?

Je mkakati upo ? wa kuhakikisha madarasa ya Kutosha yapo na walimu WA kutosha wapo?

Je ni kweli kipaumbele chetu kilikuwa

1. Maabara.

2. Elimu Bure.

3. Madawati.

4.

-------------------------------

Kati ya wanafunzi 393,734 waliokalia mtihani wa kidato cha nne nchini Tanzania mwaka uliopita,takriban wanafunzi 24,528 ambao walipita mtihani huo huenda wasijiunge na kidato cha tano mara moja kutokana na uhaba wa madarasa.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo wale watakaoathiriwa ,ni pamoja na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na taasisi za kiufundi zilizopo nchini humo.
Shule za uma hazitaweza kuchukua wanafunzi wote waliofuzu kuendelea na kidato cha tano.
Akitangaza matokeo hayo ya wanafunzi waliochaguliwa ,waziri katika ofisi ya rais anayesimamia utawala wa kijimbo na serikali za mtaa Bw George Simbachawene alisema: ''ni swala lenye changamoto lakini tunafanya juhudi kuhakikisha kuwa madarasa zaidi yanajengwa ili wanafunzi wote waliofuzu waendelee na masomo''.
Kulingana na The Citizen,amesema kuwa wanafunzi walioachwa nje ni pamoja na wasichana 6,789 na wavulana 17,739.
Kuna ambao wameachwa kwa kuwa wana zaidi ya miaka 25.
 
Tukubali ukweli ,wana chadema uwezo wa kufikili upo chini sana , ila uwezo wa kupotosha upo juu sana
Mkuu ebu tufafanulie wengine ambao hatujasoma hii habari kwenye gazeti bwana. Siamini kama serikali inaweza kufanya hivi. Watu humu wanapenda kupotosha vitu ili ionekane serikali yetu haifanyi kitu. Hebu tiririka mkuu nasi tuweze kujua kiundani.
 
wewe una akili kweli wewe? unafahamu ppp? unafahamu kwa nini kuna shule za private? au ndio unawashwa bila ksema pumba yeyote husikii raha? Lini nchi hii wanafunzi wote wanaopaswa kuingia kidato cha tano walimezwa na shule za serikali pekee?
Wangapi watamudu gharama za kusoma private?
 
Wataenda makambini kulima hapa kazi.Waache walime mahindi wakalishwe waliochaguliwa.Hii itaokoa gharama za serikali.Hiyo hela itawasaidia wanaolala chini hospitali.
 
Hivi hapa tatizo ni uhaba Wa madarasa au ni wanafunzi kukosa vigezo?. Lakini kwa kumbukumbu zangu elimu ni bure.
 
Kuna ambao wameachwa kwa kuwa wana zaidi ya miaka 25.
Kuwaacha sababu ya umri huu ni ubaguzi kabisa. Total descrimination. Huwezi kumnyima mtu fursa ya kupata elimu kwa kisingizio cha umri. Hata UN convention on right to education haija sema mtu anyimwe haki ya kupata elimu kwa sababu ya umri wake. Hii serikali kama inafanya mambo haya basi inasikitisha. Kila binadamu anahaki ya kupata elimu sehemu yoyote regardless of his/her gender, background, belief, sexual orientation, color, age etc. Kwani wakati wanawachukua kujiunga kidato cha kwanza hawakujua umri wao? siyo haki kabisa kuwanyima fursa ambayo ni haki yao. Kwanza walitakiwa kupewa motisha, pamoja na kwamba wamesoma wakiwa na umri mkubwa lakini wamefaulu.
 
Back
Top Bottom