Wanafanyaga mazoezi muda Gani?

Muuza Viat

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2022
Posts
2,874
Reaction score
7,481
Nilikua nimekaa zangu karume mchikichin pale sokon napiga mishe zangu za usabanga ghafla tu simu ikaita kumuangalia mpigaj ni mteja wangu mmoja hv wa kitaambo huyu jamaa nilishamuambiaga akipata dili anishtue sasa km zari kulikua na kijidili Cha udereva harusini.


Mzee mzima baada ya kupewa maelezo ya kutosha kuhusu wajibu na maslahi yangu binafsi nikaikubali ile dili na km zari siku ikafika nikapewa noah ya kubeba watu kulingana na maelekezo ya muajiri.


Muda ulifika tukaenda zetu ukumbini na kwa bakhti mbaya madereva wote hatukupewa kadi kwa hiyo tuliishia kupiga story kwenye parking tu.


Km unavyojua kamati za kibongo huwa hazikosagi makosa jamaa waliratibu mambo yooote lkn walisahau kuandaa wabeba zawadi kuingiza ukumbini na zawadi zenyew zilikua lundo la maua na maboks kwa hiyo kupitia kazi hiyo tukapata viza ya kuingia ukumbini bila kadi.


Mule ndani sherehe ilifana kinomanoma na menu zao zilikua za kibabe km hotelin.


Mwishooon kuna mmama mmama haswa ana trako ana tumbo na nyonyo usipime alishika maik na kutangaza "haya shoga zangu huu ndio muda wa kutoa stress njoon tufurahie vijana wetu kufunga ndoa" ghafla Dj akaweka jimbo la chura supa star liliimbwa na meja kunta ebwana eee ilikua balaa mpaka wenye wake zao walishangaa kutokana na kilichokuwa kinafanywa pale ukumbini wamama walikua wanapiga hadi misamba.


kuna Mzee wakichaga alikua anatafuta dawa za mkewe za presha ili ampelekee ameze mwishowe akajikuta anazimeza yey kutokana na balaa alilofanya mkewe


Kwa wale ambao wanashiriki kwenye vikao vya kamati je kunakuwaga na utaratibu wa kufanya mazoezi ya kunengua kwa wanawake siku ya sherehe???
 
We unaoa lini?...
 
Nje ya mada, nina shida na Stan Smith Adidas nyeusi hapo Karume,number 43..
 
Umetukosea kuanzia hapa
 
kuna Mzee wakichaga alikua anatafuta dawa za mkewe za presha ili ampelekee ameze mwishowe akajikuta anazimeza yey kutokana na balaa alilofanya mkewe🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
kuna Mzee wakichaga alikua anatafuta dawa za mkewe za presha ili ampelekee ameze mwishowe akajikuta anazimeza yey kutokana na balaa alilofanya mkewe🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
😂😂😂 noma sanaaa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…