Hapa umechemsha. Mnaua Elimu yetu. Ni kwa vipi Elimu inaendeshwa kwa kufinyanga finyanga mambo? mlianza na maabara mkafinyanga yako wapi? mkaja na walimu wa sayansi mkafinyanga yako wapi? Walimu fasta fasta mkafinyanga yako wapi? elimu bure mnafinyanga finyanga yako wapi? Sasa la madawati. Hata mabanzi yametengeneza madawati, mbao za mipapai zinatengeneza madawati nk na madawati yamefuatia musukumo kama aliokuwa nao ombaomba Matonya. Alipokuwa akiomba ukamunyima anakufuatisha matusi, alikuwa akiomba kila mtu bila kujali ni adui au rafiki yake. Nilishangaa nilipokuta Uzi ha jf ukisema Jpm amesema Wachina wana pesa nyingi tu kutukopesha. Ilikuwa baada ya kukopeshwa trillion 16. Nikajiuliza maswali. Reli no muhimu lakini Elimu no muhimu zaidi na zaidi. Kama kupanga no kuchagua kwa nini huo mkopo wote usingekopwa kuboresha Elimu? Basi labda IPO sababu, kwa nini wasikope kwa vyote maana tumeshazoea madeni? Wakati mwingine mjue hata wa vijijini wana fikiri. Kuna siku mbuzi hawa watakata kamba.