Wanachama waliojiunga CDM - Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachama waliojiunga CDM - Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Du Bois ideas, May 7, 2011.

 1. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg viongozi wa CDM mlioko sasa Mbeya,

  Nimeona maandamano katika picha hapa JF yalifana saana, sasa nilipenda kujua kama mlipata idadi ya watu waliojiunga na chama ili nasi tulioko mbali tufahamu na tupongezane wote. Na je, Ratiba ya maandamano hayo kusini yakoje, naomba kujua tarehe na mahali mtakapokuwa ili tuweze kufuatilia matukio kwani jana na leo nimejaribu kuangalia media zetu sioni hata moja iliyoonesha maandamano ya Mbeya Kuna shida gani ya media zetu na CDM?
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,188
  Trophy Points: 280
  Inategemea ni magazeti gani unaangalia kama unasoma Uhuru na Mzalendo huwezi kuona habari za CDM mle.

  Mwananchi: 0diggsdigg

  [​IMG]Boniface Meena na Brandy Nelson Mbeya
  CHADEMA jana waliliteka Jiji la Mbeya kwa maandamano makubwa yaliyowashirikisha mamia ya wakazi wake, wakiwamo wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
  Maandamano hayo yaliyoongozwa na viongozi wa ngazi ya juu kitaifa wa Chadema, yalianzia katika eneo la Mafiati na kuishia kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi ya Luanda- Nzovwe.
  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi walikuwa mstari wa mbele kuongoza maandamo hayo, huku wakishangiliwa na wananchi wa Jiji hilo.
  Pia alikuwepo Mbunge wa Mbozi Magharibi, Silinde David na Wabunge wa Viti Maalum, Susan Kiwanga, Joyce Mukya na Grace Kiwelu.Pikipiki, baiskeli na magari yaliyokuwa yamepambwa bendera za Chadema yalitanda katikati ya Jiji la Mbeya kuanzia mchana, huku baadhi ya wapenzi wa chama hicho wakipiga kelele za kumkashifu, Sambwee Shitambala kwa kukihama chama hicho na kukimbilia CCM.
  Kabla ya kuhamia CCM, Shitambala alikuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Mbeya.
  Maandamano hayo ya Chadema yalilenga kuishinikiza Serikali iachane na mambo kadhaa, ikiwamo muswada wa kubadilisha Sheria ya Ununuzi wa Umma ili kuruhusu ununuzi wa vitu chakavu, mchakato wa katiba uondolewe mikononi mwa CCM, kuunganisha nguvu ya umma ili kupinga bidhaa kupanda bei na kutaka uchaguzi wa Meya wa Arusha ufanyike upya.
  Wakati maandamano hayo yakiwasili katika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Luanda-Nzovwe tayari umati mkubwa wa watu ulikuwa umeshafurika kuwasubiri viongozi wa kitaifa wa chama hicho.Polisi walionekana maeneo mbalimbali yalikopita maandamano hayo wakiendelea kulinda usalama wa watu na mali zao.
  Wafuasi wa Chadema walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali, huku wengine wakisema kama Dk Slaa si Rais wa Tanzania basi ni Rais wa Mbeya.Wengine walikuwa wamebeba mabango yanayokebei hatua ya CCM ya kujivua gamba na mengine yakilalamikia maoni ya Katiba mpya yanavyoendeshwa.
  Wakati akifungua tawi la chama hicho katika chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), kabla ya maandamano hayo kuanza, Dk Slaa alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kuacha kuvitisha vyama kwa barua kuwa visifungue matawi vyuoni."Tendwa ajue kuwa wanafunzi nao ni wananchi na ajue kuwa sisi kama Chadema tunafuata taratibu, hivyo asitutishe," alisema Dk Slaa.
  Mbowe kupinga kodi
  Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe alisema chama hicho kitapinga ongezeko la kodi yoyote bungeni katika bajeti ijayo mpaka kieleweke na kwamba Serikali isipofanya hivyo watapigana bungeni kwa maslahi ya wananchi.
  Mbowe alisema ongezeko la kodi linawaumiza wananchi na Serikali imekaa kimya wakati hali ya maisha inaendela kuwa mbaya. Mbowe alisema kuwa mapambano hayo watayafanya bungeni, ikishindikana watayahamishia kwa wananchi ili Serikali ielewe kuwa hali ya maisha kwa wananchi wa chini si nzuri."Wabunge wa Chadema tutaendelea kukomaa mpaka kieleweke kwa kuwa hatuvunji amani, bali tunawahangaikia wananchi ili wawe na maisha bora," alisema Mbowe.
  Mbowe alisema kuwa Taifa lina msiba mkubwa wa umaskini na Chadema itapambana bungeni na nje ya Bunge mpaka kieleweke.Alisema kuwa Serikali imezoea kupanda kodi ambayo husababisha kupandisha gharama ya maisha kwa wananchi kwa kuwa serikalini hawana shida.

  "Kama Serikali inataka kuona uwezo wetu wa kuhamasisha Watanzania wapandishe kodi katika bajeti ya mwaka huu," alisema Mbowe.Alisema wamekuwa wakifanyiwa hila kuwazuia kutumia haki yao ya kidemokrasia bungeni kwa madai kwamba wabunge wa Chadema wanavunja kanuni, lakini haielezwi ni kanuni gani zimevunjwa.

  Dk Slaa na bei ya bidhaa
  Naye Dk Slaa alisema lazima Serikali ishushe bei ya sukari na mafuta kwa kuwa kutofanya hivyo ni kama Serikali haipo."Haiwezekani wanavuana magamba halafu wananchi wanaendelea kuteseka. Magamba ni yao, hivyo wananchi waangaliwe," alisema Dk Slaa.
  Alisema kuwa wataendelea kuandamana kwa vile ni haki iliyopo kikatiba, hivyo Jeshi la Polisi haliwezi kuzuia au kutishia kuzuia maandamano yao.
  "Tunawahamasisha Watanzania kuangalia hali ya maisha yao kwa sababu ni haki yetu ya msingi, na tunataka wananchi waionyeshe Serikali yao mambo yanayowasumbua," alisema Dk Slaa.
  Akihutubia mkutano huo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema, alimtaka Dk Slaa asimjibu Ridhiwani Kikwete katika hizo siku alizotoa, bali ampe Rais Kikwete siku saba za kuhakikisha kuwa mafisadi wote wanatokomea.
  Alisema mapambano yake yataendelea bungeni kwa kuwa suala lake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, bado halijaisha, hivyo Bunge lijalo litawaka moto. "Pinda alinibeep bungeni nikampigia, Makinda akapokea. Lakini mvutano wangu na Pinda haujaisha, nikiingia bungeni mtanisikia," alisema Lema.
   
 3. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu mwitikio wa watu kujiunga Cdm inatisha.juzi kwenye maandamano ya mbeya mjini,kadi zaidi ya 1500,ziliuzwa,jana nikiwa ktk msafara wa mh Mbowe,amefanya mikutano 5,ktk jimbo la Mwakyusa,kadi 485 za cdm zimeuzwa,leo tupo kyela,tutaelezana
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mbona hamtoi live updates sasa,au ndo mpo porini sana?
   
 5. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Good inatia moyo, Mh Mdee alisema CCM watauona mziki wa Chadema
   
 6. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kamanda kiukweli hata muda wa kuchezea cm ckuwa nao,mnisamehe kwa hilo,leo tunaanza kwa kufungua matawi hapa kyela mjini,kisha mkutano matema,ngyeke,ipinda,tunamalizia kyela mjini jioni,
   
 7. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana ndugu Kijallo kwa kutujuza yaliyojiri upande wa idadi ya wanachama waliojiunga na chama chetu cha ukombozi. tunaomba uendelee kutujuza. picha zina nguvu zaidi ya kuhabarisha. Asante sana
   
 8. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  kijani kazi wanayo!, mpaka wamalize kuvuana magamba watakua hawana mwanachama wa ukweli! Sasa naona tofauti ya cdm na nccr ya 95!, watu wamedhamilia sio upepo wa siasa!
   
 9. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa kaka, nimeona mambo ya CDM Mbeya, endeleeni kutujuza. Zitto yeye yuko wapi?
   
 10. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jana Mh Zitto,alikuwa na mikutano mi4 ktk jimbo la mbozi mash,leo ameenda njombe pamoja na mh Mbowe msibani kwa mama Makinda,leo jioni Zitto atafanya mkutano Rujewa.
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Zitto anamuhudumia mama yake kwanza...nadhani bunge likianza maza ake atakuwa keshapona na zitto atakuwa available bungeni.
   
 12. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hekima mkuu nibule
   
 13. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jimbo la mweshimiwa silinde ratiba imekaeje?
   
 14. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #14
  May 8, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,248
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Ninaamini kabisa Mkweree roho inadunda kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jana walikuwa na mh makamu mwenyekiti znz,cjajua ratba ya leo!
   
 16. k

  kakini Senior Member

  #16
  May 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mpaka sasa nimetembea sehemu nyingi Tanzania sijaona mtu akajitokeza wazi wazi na kusema yeye ni CCM yaani akawa kifua mbele kukitetea
   
 17. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 940
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ccm wako hoi bin taaban kusikia jinsi CHADEMA inavyozidi kupendwa na wananchi wa rika zote.
   
 18. z

  zamlock JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  na bado nataka maandamani hp dar tufanye kufuru ya kufa mtu
   
 19. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  zitto safi sana tunataka ukazane hvyo hvyo na ushirikiane na viongozi wenzako km hivi.Sisi tunakupenda sana na tulikuwa tunasononeshwa ulivyokuwa umebaki nyuma kipenzi chetu na tegemeo letu kuikomboa nchi yetu iliyopo mikononi mwa walanguzi.
   
 20. B

  Baba Jose Senior Member

  #20
  May 9, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani chonde naomba kujua kama wataenda ileje,mwenye taarifa tafadhali
   
Loading...