Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,590
- 8,718
Kikwete aliwaacha mja*&$mbe nyie mkaamua kumuharishia....aliwaacha mkojoe mkamrushia mkojo usoni...
Mlimuita JK ni dhaifu leo hii mnamuita Magufuli dikteta.
Hivi kuna mlevi wa madaraka kama Mbowe?
Alibadili katiba ya Chadema ili aendelee kuwa Mwenyekiti...aliwafukuza kina Zitto kisa tu uwenyekiti bila kusahau figisu figisu dhidi ya Wangwe.Huyo ndio mlevi wa madaraka ambaye akiwa pamoja na wewe mbobezi wa kumshabikia mnatuaminisha kuwa mnaijua demokrasia...so sad ...!
Ccm ndio yenye dola na umma kwa sasa...yaani CCM ikiamua kuwaingiza wanachama na wafuasi wake barabarani hata kwa showoff tu hakutakalika.
Hata mimi natoa ushauri unbiased ila wewe umeamua kuungalia kwa jicho biased
ni ushauri tu nimetoa wala sijajinasibisha na chama nimeongea kama mtaalamu tu basi ...ndio maana nikasema Hutaki Acha .....ni mambo mengi tu tushasema na yakawa ..
In the actual fact ccm ikitaka kuweka maandamano ni kweli hakutakalika basi na iweke ....kama wafuasi "hewa" wanaotokana na kura "hewa" wanaweza kuandamana waandamane !!
Kuna kitu kimoja kama umegundua wakati wa kikwete mfano matokeo ya uchaguzi yakitangazwa ccm wakashinda ilikuwa tunaona mashabiki na wakereketwa wakipita huko na huko kwa mbwembwe wakishangili ....hii kisiasa ina maana chama kina watu wanakipenda na wanafurahia ushindi wa jasho lao ..
Nimefanya tathmini baada ya matokeo ya Kata 43 Na haya ya juzi ......sioni wana ccm wakijimwaga barabarani kushangilia kama zamani ,sioni shamra shamra ....na ule utani wa jadi tuliozoea ....hii ina maana gani kama kweli kura 40,0000 au 30,000 zimesema ndio alafu wanaoshangilia ushindi hawafiki 100 na wanaonekana wanyonge .....kwenye makundi ya whatsapp sioni makada wakipeana hongera na hata zikiwepo sio za dhati ....hii ina maana gani ??? je wanajiona hawakustahili ushindi kwanini hawatambi na kujigamba na ushindi kama ilivyo ada ya siasa .....nani alipiga hizo kura ???
Tusiende Rwanda ambako Rais anashinda kwa kura za 99% lakini ukitazama taswira ya nchi huoni vicheko vya 99%
Kwenye uchaguzi mkuu wa ccm nilihoji ...ule ushindi wa 100% ukumbini sikuona sura ya shangilio la 100% kwa waliokuwapo wanajua au tazameni clips ....hii mjuwe mambo yanapotokea huwa tunatazama vitu vingi ..tunasoma taswira ....
Zamani mwenyekiti anashinda kwa 90% na ukitazama ukumbi unavyovuma unaiona furaha ya moyoni