Wanaanga Wanne Watua Duniani Baada ya Siku 167 Angani..

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,751
21,204
Sisi tuendelee kupambana na waliokufa wakati wenzetu masaa machache yaliyopita wameshuka kutoka kwenye chombo cha Anga za mbali cha ISS.

Najisikia hatia kila ninapofuatilia habari kama hizi na kurudisha akili kwa hizi nchi za kiafrika, baya zaidi nikiamtazama jamaa flani kwa mambo anayofanya dhidi ya binadamu mwenzake wakati hata uwezo wa KUFUGA MENDE HAWEZI!.
👇🏾
Washington, Marekani.
Chombo cha kampuni ya utafiti wa anga za juu ya SpaceX, kilichobeba wanaanga wanne kimerejea duniani na kutua Florida jana Jumapili asubuhi, ikiwa ni mara ya kwanza kutua usiku baharini.
Wanaanga hao wameripotiwa kuwa wanaendelea vizuri kiafya baada ya kurejea duniani baada ya kuwa katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) kwa miezi sita, taasisi ya NASA ilisema.

54399929_303.jpg

PICHA: Chombo kikitua majini na tayari usaidizi wa boat na meri ukisogea kuwapokea.​

Chombo hicho kilitua saa 8:56 usiku katika ghuba ya Mexico nje ya Panama City baada ya kusafiri kwa saa sita-na-nusu kutoka ISS, picha za usiku zilizotolewa na NASA zinaonyesha.

angani-pc-data.jpg

PICHA: Mmoja kati ya wanaanga hao ambye ni mjapani akipata usaidizi kutoka kwenye walichokuja nacho.​

Timu zilizokuwa katika meli ya Navigator zilikivuta chombo hicho na kukipakia melini kwa karibu saa moka-na-nusu baadaye. Kwa NASA, hii ni mara ya kwanza kwa chombo cha anga za juu kutua usiku tangu wanaanga waliokuwa katika chombo cha Apollo 8 walipotua Bahari ya Pacific Desemba 27, 1968.

Kamanda Michael Hopkins alikuwa wa kwanza kushuka baada ya mlango wa chombo hicho mithili ya yai kufunguliwa, akijaribu kunyanyua miguu melini, na muda mfupi baadaye kufuatiwa na mwanaanga mwenzake wa NASA, Victor Glover.

gcmlopmpmlv.jpeg

PICHA: Hii ni taswira ya chombo kilichowafikisha salama dunia, ambacho kampuni ya spaceX ilikiunda.​

"Kwa niaba ya wanaanga na familia zetu, tunataka tuseme tu asante ... Ni kitu cha kufurahisha kwa kile tunachoweza kufanikisha wakati watu wakishirikiana. Wote mnaibadili dunia. Hongera. Ni kitu kizuri kurejea," Hopkins alisema katika ujumbe wa NASA uliotumwa Twitter.

Mwanaanga wa NASA, Shannon Walker na Mjapani Soichi Noguchi ni watu wengine waliokuwa katika chombo hicho.

👉🏾Zilikuwa maili milioni 71 ambazo wanaanga hao wanne walienda anga za juu Novemba mwaka jana wakiwa katika mpango wa kwanza kamilifu wa kikazi katika kituo cha ISS wakitumia chombo kilichotengenezwa na kampuni ya SpaceX inayomilikiwa na Elon Musk.

Screenshot_20210503_230202.jpg

PICHA: Wanaanga wote wanne mara baada ya kufika duniani kutoka kwenye kituo cha kimataifa cha anga za mbali.​

SpaceX imekuwa mshirika ambaye NASA inaonekana kupenda kufanya naye usafirishaji wa kibiashara kwenda anga za juu.
Wanaanga hao walisafiri maili milioni 71.2 (sawa na kilomita milioni 114.6) ndani ya siku 168 walizokuwa katika mzingo wa dunia (zikiwemo siku 167 walizokuwa katika kituo hicho cha anga za juu), NASA ilisema.

Baada ya uchunguzi wa kiafya, wanaanga hao wanne walitarajiwa kusafirishwa kwa helikopta kwenda Pensacola kwa ajili ya kupanda ndege ya kuwapeleka Houston kuungana tena na familia zao na marafiki, NASA ilisema.
Kabla ya safari yao, wanaanga wawili wa Kimarekani walifanya majaribio ya kwenda ISS mwezi Mei na kuishi huko kwa miezi miwili.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kuanzisha safari ya kwenda ISS kutokea ardhi ya Marekani tangu mwaka 2011. Pia ilikuwa ni safari ya kwanza iliyojumuisha wanaanga kuendeshwa na kampuni binafsi, tofauti na za NASA.

Asante mwananchi online kwa kurahisisha habari hii.
 
Sisi tuendelee kupambana na waliokufa wakati wenzetu masaa machache yaliyopita wameshuka kutoka kwenye chombo cha Anga za mbali cha ISS.

Najisikia hatia kila ninapofuatilia habari kama hizi na kurudisha akili kwa hizi nchi za kiafrika, baya zaidi nikiamtazama jamaa flani kwa mambo anayofanya dhidi ya binadamu mwenzake wakati hata uwezo wa KUFUGA MENDE HAWEZI!.
👇🏾
Washington, Marekani.
Chombo cha kampuni ya utafiti wa anga za juu ya SpaceX, kilichobeba wanaanga wanne kimerejea duniani na kutua Florida jana Jumapili asubuhi, ikiwa ni mara ya kwanza kutua usiku baharini.
Wanaanga hao wameripotiwa kuwa wanaendelea vizuri kiafya baada ya kurejea duniani baada ya kuwa katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) kwa miezi sita, taasisi ya NASA ilisema.

View attachment 1772531
PICHA: Chombo kikitua majini na tayari usaidizi wa boat na meri ukisogea kuwapokea.​

Chombo hicho kilitua saa 8:56 usiku katika ghuba ya Mexico nje ya Panama City baada ya kusafiri kwa saa sita-na-nusu kutoka ISS, picha za usiku zilizotolewa na NASA zinaonyesha.

View attachment 1772527
PICHA: Mmoja kati ya wanaanga hao ambye ni mjapani akipata usaidizi kutoka kwenye walichokuja nacho.​

Timu zilizokuwa katika meli ya Navigator zilikivuta chombo hicho na kukipakia melini kwa karibu saa moka-na-nusu baadaye. Kwa NASA, hii ni mara ya kwanza kwa chombo cha anga za juu kutua usiku tangu wanaanga waliokuwa katika chombo cha Apollo 8 walipotua Bahari ya Pacific Desemba 27, 1968.

Kamanda Michael Hopkins alikuwa wa kwanza kushuka baada ya mlango wa chombo hicho mithili ya yai kufunguliwa, akijaribu kunyanyua miguu melini, na muda mfupi baadaye kufuatiwa na mwanaanga mwenzake wa NASA, Victor Glover.

View attachment 1772532
PICHA: Hii ni taswira ya chombo kilichowafikisha salama dunia, ambacho kampuni ya spaceX ilikiunda.​

"Kwa niaba ya wanaanga na familia zetu, tunataka tuseme tu asante ... Ni kitu cha kufurahisha kwa kile tunachoweza kufanikisha wakati watu wakishirikiana. Wote mnaibadili dunia. Hongera. Ni kitu kizuri kurejea," Hopkins alisema katika ujumbe wa NASA uliotumwa Twitter.

Mwanaanga wa NASA, Shannon Walker na Mjapani Soichi Noguchi ni watu wengine waliokuwa katika chombo hicho.

👉🏾Zilikuwa maili milioni 71 ambazo wanaanga hao wanne walienda anga za juu Novemba mwaka jana wakiwa katika mpango wa kwanza kamilifu wa kikazi katika kituo cha ISS wakitumia chombo kilichotengenezwa na kampuni ya SpaceX inayomilikiwa na Elon Musk.

View attachment 1772534
PICHA: Wanaanga wote wanne mara baada ya kufika duniani kutoka kwenye kituo cha kimataifa cha anga za mbali.​

SpaceX imekuwa mshirika ambaye NASA inaonekana kupenda kufanya naye usafirishaji wa kibiashara kwenda anga za juu.
Wanaanga hao walisafiri maili milioni 71.2 (sawa na kilomita milioni 114.6) ndani ya siku 168 walizokuwa katika mzingo wa dunia (zikiwemo siku 167 walizokuwa katika kituo hicho cha anga za juu), NASA ilisema.

Baada ya uchunguzi wa kiafya, wanaanga hao wanne walitarajiwa kusafirishwa kwa helikopta kwenda Pensacola kwa ajili ya kupanda ndege ya kuwapeleka Houston kuungana tena na familia zao na marafiki, NASA ilisema.
Kabla ya safari yao, wanaanga wawili wa Kimarekani walifanya majaribio ya kwenda ISS mwezi Mei na kuishi huko kwa miezi miwili.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kuanzisha safari ya kwenda ISS kutokea ardhi ya Marekani tangu mwaka 2011. Pia ilikuwa ni safari ya kwanza iliyojumuisha wanaanga kuendeshwa na kampuni binafsi, tofauti na za NASA.

Asante mwananchi online kwa kurahisisha habari hii.
Sometimes habari Kama hizi hua nafikiri ni stori za kutungwa.
Ukute walikuwa jimbo fulani la Marekani wanakula Bata.
 
Ahahahahaaaa...
Chief umenifikilisha sana aseee do!.

Yaani wachukue, familia zao, ndg, jamaa na marafiki wawadanganye kwa kuwaweka kwenye runinga inayoonyesha chombo kikiondoka kwenda anga za mbali.

Alafu wanaondoka wakijua jamaa zao wapo angani kumbe wanakula 🦆 hapo Virginia 😁, lengo eti kuihadaa dunia, mmh HAPANA!.

These was real man.
 
Sasa sisi tuende angani kufanya nini? Ardhini yenyewe hatujapamaliza, duniani kwenyewe hata robo tu Mtu mweusi hajaifika, bahari yenyewe hatuijui vizuri

Tunakabiliwa na njaa huko angani kuna nafaka?
 
Sasa mgegedo veepe wengine wiki nzima kupita bila kutimiza majukumu ya mkuyenge haiwezekani
 
Timiza tu jukumu lako mkuu, ndio jukumu lako; jukumu lao ni kwenda angani huko, wanatimiza jukumu lao.

Ndio maana tuko hapa na wao wako kule.
 
Back
Top Bottom