Wana ndugu watapeliwa na mganga (sangoma)

Wana ndugu watapeliwa na mganga (sangoma)

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
4,411
Reaction score
6,496
Enyi Wagalatia, ni nani aliyewaroga?
Na ni kwa nini mnawaamini sana waganga!

PASHA HABARI
Wanandugu watatu kati ya wanne wameingia katika simanzi kubwa baada ya kutapeliwa na mtaalamu/mganga/witchdoctor.

Ungana nami mkuu radicals hapa, upate true story kamili ilivyokuwa.

MWANZO WA KISA
Ilikuwa hivi tajiri mmoja mnono aliwafuata akaomba wamuuzie nyumba yao ya urithi (ipo location nzuri sana, pale magomeni main road kabisa). Lengo la tajiri ni kujenga hoteli kubwa pale. Tajiri aliwapa offer ya milioni mia tatu (300m).

wanandugu wakashauriana weeee, wakakubaliana wauze kwa m 400 ili kila mmoja apate walau m100.

Baada ya makubaliano na kukamilisha taratibu zote za mauziano, tajiri akawaingizia benki m 400 zote, akawapa na muda wa miezi 6 waendelee kukaa in da house ili wajipange kutafuta makazi mapya.

SEKESEKE LILIPOANZIA
Kama unavyojua , kama hujawahi kukamata pesa nyingi at per(kwa mkupuo) lazima uwewesekee. Wanandugu washauriana yule tajiri asije kuwa amewapa pesa za mapepo/chuma ulete( yaan hawatofanyia cha maana zitapukutika haraka kwa matumizi ya ovyo).

Wakasema waende kwa mtaalamu akazizindike, ila mmoja wao kati ya wale wanne akagoma.

(huyu nadhani elimu ya form six ilimsaidia maana aliwashauri wenzie waende kwa wataalamu/wasomi wa mambo ya fedha ili wawashauri jinsi ya kutumia fedha hizo katika kuanzisha miradi).

Na huyu ndie aliyetusimulia mkasa huu, maana alikuja ofisini kwa washauri nami nilikuwepo pia.

Basi ndugu wale watatu wakamtenga mwenzao , wakampa 100m yake huku wakimpa kila aina ya kejeli, wao wakaenda kwa ndugu MGANGA.

WAMEFIKA KWA MGANGA
Walipofka kwa mtaalamu Bagamoyo na cash zao m 300. Walipokelewa vizuri, wakaeleza azma yao kuwa wamekuja na hela wanataka zifanyiwe zindiko ili wakazitumie vizuri.

E bwana eeh, kilichowakuta haikuwa siri yao tena. yaani walikosa hata nauli elfu 6 ya kurudia dar, na mmoja akapata uchizi pale pale.

To cut the long story short. Mganga alipooona wamezimwaga cash m 300 akawaambia ngoja aingie chumba cha ndani(CHUMBA CHA MIZIMU maana muda huo walikuwa sebuleni) aongee na mizimu direct, ili azifanyie zindiko moja kali sana.....(deadly, in dj afro voice)........
Mganga huyo akazama ndani na m300

Wakaanza kusubiri zindiko lifanyike kule ndani .........nusu saa ikapita.....saa moja ikapita......saa moja na nusu,........mbiliiiiii.......tatu
...........mmmmh......

Wakaambizana mbona MTAALAMU anakawia hivi, wakaanza kumuita......TAWIRE BABAAA, chumban kimyaaaa.....TAWIRE BABAAA, kimyaaaa .........mmmmh

Mh, wakaona mbona kimya kingi, wakashairiana waingie chumba cha MIZIMU.

Kuingia chumbani, hakuna mtu wala pesa, kuna zana za uganga tu. Wakaanza kumsaka huku wakiita. MTAALAAM, MTAALAM upo wapi!

KUMBEEEE, katika kusachi sachi na kufungua mashuka/kaniki yaliyotundikwa, walibaini chumba kina mlango wa kutokea nje, na upo wazi.

Mmoja mwenye roho nyepesi alianguka pale pale na kupata uchizi........

Ndio mambo yalivyokuwa, jamaa wametapeliwa na mtaalamu huyo, na mtaalamu hajaonekana hadi kesho............
 
Aisee! na wapigwe tuu maana hakuna namna nyingine! How
 
Kama hawajui biashara nafuu wangefungua "fixed account" wale faida kimyakimya. Ila hiyo story ni fix, hawangeweza kupeleka pesa yote kwa sangoma.
 
Yohana 10:

10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
 
Duh mm wangenikopesha laki 2 tu ningeanza kufungua biashara ya matunda thn baada ya mda nikawarejeshea
 
Kama ni Story ya kweli Basi hao Jamaa ni Mataahira.
 
Kama hawajui biashara nafuu wangefungua "fixed account" wale faida kimyakimya. Ila hiyo story ni fix, hawangeweza kupeleka pesa yote kwa sangoma.
mimi naona walipeleka yote ili iweke zindiko ndio waanze kutumia
 
Back
Top Bottom