Wana MMU,
Wengi wetu hasa wale ambao tumejiunga kitambo tumekuwa tukilalamika mara kwa mara juu ya Jukwaa hili letu Pendwa la MMU Kuzorota kila siku zinapoenda. Members mbali mbali wamerusha threads za kulalamika na wengine kushauri juu ya tatizo lililopo kwenye Jukwaa hili.
Cha kusikitisha siku zinavyozidi kwenda hali inazidi kuwa mbaya zaidi na zaidi. Jukwaa la MMU ilikuwa ni Jukwaa ambalo ukiingia hukosi kitu kipya na cha kukujenga katika Mahusiano, Mapenzi na Urafiki. Members walikuwa wakichangia wanachangia kwa hoja, na hata utani ukiwepo ulikuwepo ndani ya mada na si kwa kuvuruga mada. Ilikuwa ukikuta thread ina posts nyingi, unakuwa na moyo wa kusoma post zote sababu post zote zilikuwa ni kuhusiana na mada hivyo za kujifunza pia.
Kumekuwa na wimbi za mada za Kushushiana hadhi, za kitoto, zile zinazoelemea ngono tu, zile zinazolenga kujadili utumiaji wa Tigo, na mbaya zaidi zile zilizolenga kubomoa taasisi ambayo ni nyeti katika jamii yetu ambayo ni "Ndoa". Tukiendelea hivi hivi MMU itakuwa ni moja ya Lubricator wa kubomoa maadili katika Jamii. Haipendezi.
Kama mnakumbuka thread ya kwanza kabisa kugusia mada zisizofaa hapa MMU ni ile ya Mod INNOVATOR aliyorusha hapa October, 2011. So far inaonekana kuwa nguvu kazi ya kuondoa mada hizo imeelemea kwa Mods tu na hivyo wao pia huzidiwa. Mkuu Invisible amekubali kutupa ushirikiano na kaahidi sasa hivi atatupa Mod aliye dedicated kwenye Jukwaa huku pia akitafuta suluhisho la kudumu.
Kilicho baki kwetu ni jitihada zetu kushirikiana kuweza kuboresha Jukwaa kwa njia hizi;
1. Kila tunapo ona Bandiko halifai tutumie Button ya Report Abuse kutoa taarifa mara moja ili itolewe.
2. Tujitahidi kurusha mada za kujenga na sio kubomoa au kumkomoa fulani au kuonyesha madhaifu fulani ya jamii yetu kwa kila atakae weza.
3. Tujitahidi kujadili kwa hoja na kupunguza mizaha na kejeli kwa warusha mada. Kama mada haifai ni kheri kufanya namba moja hapo juu badala ya kuchangia.
4. Kuondoa dharau kwa Mwanamke na Mwanaume pia. Mada za kusanifu Mwanaume ama Mwanamke hazijengi, zinabomoa tu.
5. Tujitahidi kuangalia pande zote za mijadala, isiwe vitu negative tu. Mfano sasa hivi kila inapokuja mada inayohusiana na ndoa huwa ni ya kukatisha tu tamaa, hata wale ambao hawapo kwenye taasisi hiyo hukatishwa tamaa kwa kukuza negatives tu na hali kuna positives pia kwa upande wa ndoa na sio kila ndoa ni majangaa au ina matatizo wapo wenye raha na furaha kwa ndoa zao
6. Masuala ya Ngono, Maumbile ni kheri yakajadiliwe Jukwaa la Wakubwa ambapo kule mjadala utakuwa wa wazi na utapata majibu yote unayoyataka na utajibiwa kwa uwazi bila kificho.
Wapendwa wana MMU, Tukiangalia baadhi ya mambo niliyo ainisha tutatambua kuwa ni vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu kurekebisha. Take note haya si mawazo yangu tu, ni mawazo ya members mbali mbali tokana na michango yao kwenye threads za malalamiko na mijadala ya hapa na pale. Hivyo pia mnaweza ongeza maarifa mengine pia.
Naomba Ushirikiano wenu wa dhati tuweze kurudisha hadhi ya Jukwaa letu pendwa la MMU Lilivyokuwa awali.
Ingependeza ujumbe huu uwafikie wadau wote wa MMU. Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu ku mention members wengi, ila bado sijaweza kukumbuka wote, hivyo kila ambae ataona kuna mdau kasahaulika tafadhali naomba tushirikiane katika hili pia.
CC: AshaDii, BAK, EMT, The Finest, The Boss, Dark City, Bishanga, Asprin, snowhite, SnowBall, HorsePower, Lizzy, Erickb52, King'asti, Blaki Womani, Husninyo, Heaven on earth, Lady doctor, amu, mimisa, Chocs, Mtambuzi, Mrembo by Nature, charminglady, Dena Amsi, Nicas Mtei, Smile, mwaJ, Judgment, watu8, Baba V, Kongosho, sweetlady, Mamndenyi, Marejesho, ladyfurahia, KOKUTONA, Roulette, Kaizer, KakaKiiza, The secretary, Mwali, Katavi, Fixed Point, Paloma, Passion Lady, cacico, kiwatengu, mimisa, sosoliso, Dark City, Kimey, Teamo, MwanajamiiOne, Preta, Arabela, Nivea, Avemaria, KOKUTONA, Bujibuji, Eiyer, Ruttashobolwa, Rutashubanyuma, Fidel80, Mzee wa Rula pakajimmy, Vin Diesel, WiseLady, Maeskron, Mentor, Mwita Maranya, Mungi, Arushaone, Tuko, Speaker, Fang, Moderator, Invisible, INNOVATOR, Pruner grafani11, Blaine