Wana JF niwatake radhi.

Wana JF niwatake radhi.

Sidhani, kama ni kweli...

Kimo sio factor ya tabia ya mtu, na haiko scientific proven

Watu wafupi mara nyingi wanapenda kuonyesha tabia za ushindani mkubwa, kujiamini kupiliza, au kutaka kusikilizwa zaidi.

tofauti na watu warefu au wenye kimo wastani.

Ww si unaishi kwenye Jumuiya ya watu. Angalia tabia zao na jinsi Mind zao zinavyofanya kazi wakiwa miongoni mwa watu.

Nimesema hivyo kwa kuwa BICHWA KOMWE - ni andunje na unaona anavyojitutumua😊😊😊😊
 
Jamaa unachukulia kila kitu kwa undani sana wa nafsi na akili yako.
Unataka watu wakuzingatie (attention) wewe kama mtoto wao. Ukija kuoa utamsumbua sana mkeo.
Ukizeeka au ukiumwa utawasumbua sana watoto wako na nduguzo
Je, unadhani kuongelea vitu vya maana ni kutafuta attention?

Mbona wamatumbi mnapenda sana, kuuziba ukweli kwa drama zisizo na kichwa wala miguu?
 
Kwa maandishi yako ya JF.

Kuna siku ulilalamika watu wanakujua ila wanakuchukia.

Nikasema kinyangarika gani huyu anasema tunamjua wakati ndiyo kwanza namuona leo?

Mbona anapenda kujipa umuhimu ambao hata hana?
Umesoma uzi wangu?

Nimeongelea maswala sensitive sana humo
 
Kumbe huu uzi ni wangu!? mi sina Habari.
kijana nilimuweka wazi tu kuhusu tabia yangu isiyoweza kubadilika.

Huyu mtoto nitamkausha tu maji...
Aisee, wewe unanipa Hamada ya kuja kukuta futa kwa Hali na mali, sio kwa dhihaka hizi
 
1. Uchambuzi wa Aya ya 1 na 2: Mfano wa Gurudumu na Kivuli
Aya hizi zinatumia mifano miwili mizuri sana ya maisha ya vijijini ili kuelezea jinsi akili inavyofanya kazi kisaikolojia.
  • Mfano wa Gurudumu na Ng'ombe (Aya ya 1): Buddha anasema mtu mwenye nia mbaya anafanana na ng'ombe anayevuta mkokoteni ambapo gurudumu linamfuata nyuma na kukanyaga nyayo zake. Kisaikolojia, hii inamaanisha kuwa mawazo mabaya (kama hasira, wivu, au ubinafsi) huacha athari nzito na zenye maumivu mwilini na rohoni. Kama vile gurudumu linavyomchosha ng'ombe, ndivyo msongo wa mawazo na chuki zinavyomtesa yule anayezihifadhi akilini mwake.
  • Mfano wa Kivuli (Aya ya 2): Kwa upande wa mtu mwenye mawazo safi, furaha inamfuata kama kivuli. Kivuli hakituhitaji kikitunze, hakina uzito, na hakipotei maadamu kuna mwanga. Kisaikolojia, unapofanya vitendo vya wema na upendo, furaha inakuwa matokeo ya asili yasiyohitaji nguvu nyingi. Inakuwa sehemu ya utu wako.

2. Uchambuzi wa Aya ya 5: Kwa Nini Chuki Haishindwi kwa Chuki?
Huu ni ushauri wa kisaikolojia ambao hata sayansi ya kisasa ya tabia za binadamu inaukubali:
  • Mzunguko wa Kisasi: Ukijibu chuki kwa chuki (kwa mfano, mtu akikutukana nawe ukamtukana), unachochea moto uendelee kuwaka. Kisaikolojia, tabia hii inalisha mfumo wa ubongo wa kujihami na kushambulia (fight or flight), jambo linalofanya pande zote mbili zizidi kuwa maadui.
  • Nguvu ya Kisaikolojia ya Wema: Unapomjibu mtu mwenye chuki kwa utulivu na upendo, unavunja ule mnyororo wa kisasi. Hii inamfanya yule mwenye chuki akose sababu ya kuendelea kukushambulia, na mara nyingi inampa nafasi ya kujitafakari na kutulia.


Wisdom to live by.... Thanks mkuu🙏
 
Umesoma uzi wangu?

Nimeongelea maswala sensitive sana humo
Hiyo habari ya "nimeongelea maswala sensitive sana humo" ndiyo kujipa umuhinu kwenyewe.

Waache watu wengine waseme kama ni masuala (masuala, si maswala) sensitive sana au uduanzi tu.

Usilazimishe wewe unayesema kuyafanya yawe sensitive sana.

Unaweza kuwa unajipa umuhinu tu bila sababu.
 
Kwanza kabisa nianze na Kutoa Shukran kwa waendeshaji wa jukwaa hili, japo lina changamoto zake, ila bado lina mchango mkubwa sana. Nimeweza kujiona Niki kuwa katika mtazamo since najiunga humu... Hauwezi kuona ila uki look back to how ulikuwa unafikiri na kuchangia mada 3 or 4 yrs ago ndo utaona vizuri.

Pili, naomba huu uzi uwe kama mfano kwa wengine, wale wanakuja humu kwa lengo la kudhihaki watu, kuweka watu chini, na kuongea kwa namna ya kuzua taharuki(najua matani muhimu, ila yakipitiliza inakuwa kero)

Niende moja kwa moja, kwenye kuwasilisha radhi zangu..

Binafsi nimekuwa mtu wa kufanya watu wajiskie ovyo sana, na si kwamba ninapenda bali ni kwa sababu ya treatment, kipindi naingia humu, kuna muda ilikuwa naona au ku experience watu wakiwa bully wengine, unakuta mtu Kaletra post yake anashinda, then inakuja jitu lina weka comment ya mauzi na fedheha just yule anaye taka msaada ajoine hana maana.

Huo ni mfano mdogo tu, ila nahisi mnanielewa nikisema hivyo..

Sio kila kiumbe kinazaliwa kikiwa kibaya, angalia watoto wadogo walivyo na upendo pure, it is this messy world that weakens and destroys a soul.

Sasa, binafsi... Nilikuja kama mtu mkarimu na mwenye kuchangia na kuwapa watu mioyo, ila baada ya interactions kadhaa, Nilikuja kugundua kuwa watu hawana moyo kama wangu, kuna majitu ya ovyo ambayo kazi yao ni ku spread negative energy.

Nilikuwa so toxicated na ile dark ego yangu ikaja juu, plus pia situations za maisha zilinifunza kuwa kukaa kinyongo unakuwa target, yaani kila mtu ana kufanya zuria la kukanyagwa.

Sasa, nikasema ngoja waone kuwa hata sisi wastaarabu huwa tuna hasira vile vile. Ndo maana Nika geuka kuwa mbogo.

Nahisi mnajua nimekuwa mtu mkaidi sana katika hilo jukwaa. Mtu akija kwa kutaka kuni challenge lazima a one kuwa mimi sio mtu wa mchezo mchezo.. Sio kwamba ninapenda, bali uhalisia Unanitaka hivyo.

NIMEKUWA MWIBA MKUBWA KWA WANAWAKE, sio kwamba wao ni tatizo(especially wote, bali ni kwa sababu ya wachache wenye viburi, katika jamii tishio leo, wanawake wamekuwa toxic sana, ni wanavuruga alaf tatizo linaonekana as if hawakuhusika) angalieni misukosuko katika ndoa. Wanawake hawajui kabisa kitu watakacho besides money.

Sasa nimekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha nasema ukweli bila kuficha, sio kwamba nataka vita na wanawake, ila kwa sabubu uchafu wa wanawake wachache hauongelewi ipasvyo. Tunaslide tu na kuendelea loop zile zile bila kuangalia mzizi.

Radhi yenyewe
Wanabodi, kwanza kuna perception ambayo ni so negative kunihusu, kuna member wengi sana humu wenye chuki na mimi, wananiona kama mtu mkaidi, wala nisiye na staha, mpka kuna wengine wananizushia kuwa mimi omba omba.... Sipendezwi na hilo kabisa.

Kama kuna mtu nilishawahi kumfanya ajihisi low, na vibaya atambuwe kuwa sikukusudia kabisa. Mimi ni mtu poa sana, sinaga hizo hulka, huwa nafanya for the sake of fun, tu. **** unanifatilia vizuri likija jambo sensitive huwa unajaribu kuweka matani pembeni.

Najua, kuna watu wa nafikiri, hizi drama na kuzushiana mambo mabaya zina effect mtu! Hapana, bali hazina maana kabisa... Najua hilo kwa sababu ubongo wa bialnadamu haujui difference btn matani na real scene, ndo maana unaweza kuangalia movie na kulia, wakati wao wana fanya maigizo.

Naomba, tuache kuwa na battle zisizo na manufaa, kwamfano mimi tayari nimeahakuqa mtu mzima, naona it's all crap kukaa kila siku natukanana na watu, ni utoto na ujinga, we've lots of things to work on.

Nilio wakwaza tusameheane, Nimeacha rasmi drama(japo mda wa matani upo) ila kuchukua things serious ndo sijawahi kufanya kabisa...

Nawasilisha...

Naitakia Simba ushindi mnono.
Mbona hatukufahamu newcomer , au wewe ndiye yule kijana msumbufu 11 AKA Chiwawa?
 
Back
Top Bottom