Wana JF naombeni MNIFUNDE

oh no way.mi huwa naogopa sana kujifanyia experiment. eti nilisikia pia kuwa hata mtu akifunga upande wa khanga yake mjamzito hajifungui je ni kweli? na pia wanasema eti si vizur kuwatajia watu tarehe ya kujifungua?

me hiyo ya kukaa kizingitini ilinitokea wazee wanambia
 
Kongosho, ukikaa mlangoni utakumbwa na nini?
Hakika nina mengi sana ya kujifunza, naomba msaada wenu wapendwa



We mama lea mimba yako kwa amani siku ikifika wahi hospitali na kwa uwezo wake mwenyezi ujifungue bila matatizo,hayo mengine naona kama unataka kujifunza uchawi tu..
 
usiwe na shaka yoyote, huzulia clinic km kawaida utajifungua salama dada angu.
kuhusu mila na desturi zinatofautiana kutoka clan moja na nyingine, usidharau mambo ya mila za kwenu, waone nyakanga na kungwi wa mila za kwenu watakujuza nini ufanye na kipi ukiepuke.
KUDHARAU MILA NA DESTURI NI KUWADHARAU WALIOLIFIKISHA TAIFA HILI HAPA TULIPO HATA SI AIBU KUJIITA M-TZ, BIBI NA BABU ZETU.
Kama umo ndoani zaidi ya 5yrr na una watoto unafahamu kuwa mila na desturi ni part and parcel ktk maisha ya ndoa.
 
Aisee, hongera sana. At last umekuwa pinned down eeh! Ni yule handsome anayejua naniliu? Mmefunga ndoa ama mmekatisha route?
 
nazjaz mdogo wangu(am just assuming since mi nna watoto 2 wa kwanza ana miaka 13 sasa)imani nyingi za kiafrika huwa tunasema hazina proof kwa sababu hatuwezi kuziprove right lakini pia hatuwezi kuziprove wrong,so hizi vitu za kukaa mlangoni ukiwa mjamzto,kutokusema siku ya kujifungua(by the why shud u? )kuhakikisha mtoto akikatika kitovu hakiangukii kwenye dudu yake,since wazazi wetu walizitumia na sisi tukawa vile tulivyo leo mi nafikir hakuna haja ya kutake a risk!as long as havikuathri ukivisikiliza we visikilze na MSUBIRI MTOTO WAKO KWA AMANI:A S-baby:.otherwise nazidi kuona umuhimu wa informal education as far as jinsia na uzazi is concerned
 
Mie nafikiri vitu vingine tulikuwa tuaambiwa tu lakini ukitazama kiuhalisia sioni mantiki yakukataza kuvifanya; Mfano mie kule kwetu haturuhusiwi kukata kucha usiku, mwanamke haruhusiwi kukalia "ngata", haturuhusiwi kufagia usiku, haturuhisiwi kuosha vyombo ulivyolia chakula usiku, ukiuliza sababu nini unapewa jibu lisiloeleweka. Ajabu mbona huku mijini vinafanyika na sioni kinachotokea?. Nije kwenye hicho ulichouliza, mimi nina mtoto nakumbuka nilipojifungua bibiyangu alikuwa akisisitiza sana kitovu kisiangukie kwenye uume wa mtoto nilipouliza sababu nikapewa hicho ulichoambiwa. lakini nikitazama mantiki ya kusema hivyo labda wanataka tuwe makini katika ulezi na mara nyingi kitovu cha mtoto kinahitaji usafi ulio makini sana.
 
mimi huwa si muumini wa mambo ya kale hasa yasiyokuwa na logic km hili ulilouliza,uhusiano apo uko wapi?kila kitu ni imani...ukiamini hivyo itakua hivyo n vise versa is true,otherwise hizo ni stori za alinacha zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 
Back
Top Bottom