Wana jf kwa ikhsani zenu kuna mtu yoyote hapa anakumbuka ya tokeo hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana jf kwa ikhsani zenu kuna mtu yoyote hapa anakumbuka ya tokeo hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sonara, Jul 7, 2009.

 1. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Napenda kuwaomba wa Tanzania wezangu wenye kumbukumbu ya ule mwaka ambao Mlezi wa Taifa letu Mwalim Nyerere, alipotangaza rasmi kuanzia siku ile kiswahili ndio kitakuwa Lugha ya Taifa.
   
  Last edited: Jul 7, 2009
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ilikuwa mwaka 1964. Tangazo lilitolewa na Waziri Mkuu Rashid Mfaume Kawawa.
   
 3. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  one of the best things Mwalimu ever done for us.... hata kama kuna watu watasema Mwalimu alikuwa na mapungufu, kwa kweli wangetembea waone, pamoja na mengine mengi kutumika kwa kiswahili kama lugha ya Taifa kwa kweli imesaidia sana kuleta "UMOJA WA KITAIFA".....

  Mwalimu aliona mbali sana zaidi ya wengi wetu wakati ule na kwa kweli ukiangalia mambo yanavyoenda, mpaka sasa
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jamani mnaweza kuthibitisha kwamba nchi ambazo hazina lugha yao rasmi ya kitaifa HAZINA UMOJA WA KITAIFA??? Tazameni mbali ndugu zangu, sifa na mbwembwe zingine tunazowapa viongozi wetu hazina tija na wala hazitusaidii kuondokana na umasikini unaokua kwa kasi kila siku. Mi naamini kwa watawala the so called UMOJA WA KITAIFA umewasaidia sana, kwa sababu wametuibia na wanaendelea kutuibia rasilimali zetu kwa kuendelea kutupumbaza na misemo isiyo na tija.

  Sijui amani na umoja wa kitaifa vinatusaidia nini, kama wazalendo wa nchi hii tunazidi kutopea kwenye lindi la ufukara wa kutupwa. Wenye nacho (watawala) wanazidi kurithishana uongozi ili waendelee kuwa nacho milele na milele, huku masikini wa tanzania (majority) wakibaki kuimbishwa ngonjera zisizokuwa na kichwa wala miguu kila kukicha!!!
   
 5. Z

  ZuluBoy Member

  #5
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati Mzee wetu Reginald Abraham Mengi anajaribu kupambana na Mafisadi Papa, ndani ya nyumba yake si shwari hususan katika Kampuni ya The Guardian Ltd.

  Wafanyakazi wanapiga miayo bila mishahara, huku wanene wakipigana vita ya kupata utukufu wa Bwana Mengi.

  Ndugu yetu Kiondo Mshana, Mkurugenzi Mtendaji wa IPP MEDIA, amefaulu kumuondoa sakina kwa mbinu mbili--Ushirikina na fitina kali ambayo kwa karibu alisaidiwa na bibie Joyce Kisaka au Wakuvunga ukitaka.

  Joyce kamaliza swahiba wake Sakina kwa kumchunguza nyendo zake na kisha kuripoti kwa wanene. Mshana kaendelea kuingia viwanja kutafuta uchawi ili kuhakikisha anabakia kuwa top. Sakina kaangukia pua sasa ameamua kujiuzulu.

  Msaki aliponusa vita ijayo, akaamua kuchomoka na kurudi Mwananchi. Eti kila alipokuwa akiingia ofisini mara kichwa, mara macho hayaoni, akiwa nje mzima kama bikira wa Kiarabu!

  Sasa mkakati unaendelea na kuna wahariri wawili ambao wanalengwa kwa udi na uvumba lazima wang'oke ili Mshana apata kupumua. Katika Mkakati huo, ataendelea kumtumia bibie Kisaka---Mrembo anayewaliza hata wanene pale Ikulu.

  Joyce kabebwa na Sakina kwa miaka kadhaa na inasemekana walikuwa mashoga wakubwa, wanaosafiri pamoja na kutembea pamoja lakini cha ajabu, Sakina hajui nyumbani kwa Joyce na wala hata kama ni mke wa mtu.

  Wahariri hao wawili ambao inasemekana wana msimamo thabiti dhidi ya uongozi dhaifu wa Mshana, ni lazima waondoke kwa gharama ya yoyote ile ikibidi hata kuuaawa. Nimefanikiwa kupenyeza kinasa sauti ndani ya Kikao cha siri kati ya Mshana na Kisaka punde tu aliporudi toka Uingereza anakodai alikwenda kuhudhuria semina.

  Lakini ukweli alitumwa kwenda kupiga fitina na mnene mmoja ndani ya Ikulu ikiwa ni pamoja na kuiba nyaraka za Serious Fraud Office Zinazowahusu wakubwa hapa Bongo, baada ya kudai anaweza kuleta faili lote.

  Lakini kaambulia patupu na mmoja wa wanene wanaotuhumiwa kwenye kesi ya SFO sasa anadai arudishiwe ngawira zake, na Mama katishia kulipua bomu. Mshana anaujua Mpango huu ambao bosi wake hana taarifa nao.

  Ndani ya miezi mitatu ijayo mtayasikia haya na mtanikumbuka.
   
 6. Violet

  Violet Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiswahili kimetusaidia sana sana , imepunguza sana mambo ya ukabila. Fikiria tusingekuwa na kiswahili na sio kila mtu anzungumza kingereza.
   
 7. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  Hii habari ya Sakina hapa imeingiaje jamani....? Mods mko wapi..?
   
Loading...