Wana JF, Karibuni kwenye Mkesha wa Escrow...

Wana JF, Karibuni kwenye Mkesha wa Escrow...

WILLAFRICA

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2013
Posts
4,027
Reaction score
933
Kesho ndio kesho ,mseja jala na wala si mwala. >>pinda,maswi,muhongo,tibaijuka,werema,chenge,rugema na timu escrow nzima matumbo moto .walilolila kwa tila wanalilipa kwa hila. Mjomba na lake tezi, muhimbili na vyetu vifo!. Ha! Haa nakumbushia tu zama za umalenga. **watanzania tunasubiri maamuzi magumu kesho yenye ugumu zaidi ya kula nyama ya mtu!.
 
Kesho tutakuwa wadogo tu masaa 12 kwa CCM ni mengi sana kufanya nyeusi kuwa nyeupe.yangu macho ila kesho si mbali
 
Nadhani ni wakati muafaka wa kuanza kuzipiga kiberiti ofisi zote za CCM ndio watu watapata akili.
 
Hii penati Makinda anaipaza kwa makusudi na timu ya Muhongo inapata ushindi
 
umenivutia na ughani wako mkuu...nimelikumbuka GAMBA Tambalizeni
 
Kama ukiwa umepania kitu sana kawaida hakitokei, sasa kesho hakuna mjadala, kesi iko mahakamani
 
Tunaambiwa Katibu wa Bunge amekataa kupokea barua. Labda Mungu anaanza kusikiliza kilio cha waja wake.
 
Sitarajii mapya ya zaidi ya kawaida ya kulindana ,viongozi wanaiba(wezi)mali ya umma wanajiuzulu na kwenda kutumia kwa raha zao walichokwapua na hawafilisiwi wala kufungwa na unafikiri tutakuwa tumeondoa tatizo au ndio tutakuwa tumeongeza matatizo mengine?.Yeyote atakaepata nafasi nae ataiba kwa sababu hakuna madhara kwake na maisha yanaendelea kama kawaida.Wale wale wenye mikono michafu ndio hao hao waliopewa jukumu la kuandika katiba na ndio hao hao hupongezwa na kumwagiwa sifa lukuki halafu mnatarajia jipya?.
 
Kesho ndio kesho ,mseja jala na wala si mwala. >>pinda,maswi,muhongo,tibaijuka,werema,chenge,rugema na timu escrow nzima matumbo moto .walilolila kwa tila wanalilipa kwa hila. Mjomba na lake tezi, muhimbili na vyetu vifo!. Ha! Haa nakumbushia tu zama za umalenga. **watanzania tunasubiri maamuzi magumu kesho yenye ugumu zaidi ya kula nyama ya mtu!.

Sawa Hemed Kivuyo wa JF!!
 
Wenye kujua ratiba za bunge hivi kesho asubuhi wanaanza na maswali na majibu au ni moja kwa moja kwenye escrow report? Tupeane taarifa tufungulie TV mapema
 
Tunaomba radhi jf haitakua hewani kesho kwa masaa 24 kwa matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu
......natania tu.....
 
Umeme utakatwa ktk mitaa yote ya walalahoi...na matngazo yakakuwa hayaeleweki..vipaza sauti vya Tbc vitashindwa ku function...
------aaaaah natania tu jamani------
 
Hili la escrow ni kama Maji tuloyavulia nguo hatuna budi kuyaoga... Kesho ndio kesho, huo ushuzi wa mahakama ya kina muhongo na werema waendelee nap huko huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom