Na tuwachape tu,wezi wa Fedha za Escrow

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Feb 15, 2014
1,173
1,250
Hukumu yangu mimi mwananchi wa Tz niliyekasirishwa na wezi waliochota mabilioni ya Tegeta Escrow wakati watanzania kibao wanakufa kutokana na kukosekana dawa hospitalini,

Chenge,huyu popote alipo mwambie anadeni langu la viboko 24,kwa sababu huyu ameonekana ni fisadi mzoefu,kila dili la kifisadi,basi ujue Chenge kapiga hela,Lowassa naomba umfikishie taarifa hii mh Chenge,

Jaji Werema wewe kwanza ninakuchukia sana,umeiba pesa zetu,then unamwita Mkigoma mwenzangu Tumbili na kumtishia maisha,kisa bilioni 1.6😡😡,wewe hufai kujiita wa Mara,kutokana na ubabe wako,na kwa niaba ya watanzania waliochukizwa na ufisadi wako maubabe yako ninakudai fimbo 14,mwanasheria wa Bunge Tundu Lissu,fikisha ujumbe wangu,

Le profesel Muhongo,wewe kwakuwa ulipewa zamana ya kuhakikisha watanzania wanapata mwanga bora wa maisha kutokana na kupatikana huduma bora za umeme,bt still pamoja na kushindwa kuboresha shirika na huduma ya umeme ukaruhusu wizi kufanywa na kutokana na majibu yako ya dharau,wewe kwa niaba ya mkoa wangu,na heshima ya baba wa taifa Nyerere na kaka wa taifa Warioba unaotoka nao mkoa mmoja,viboko12 vitakuhusu ili ukumbuke maadili ya mkoa wako 😠😠

Maswi,wewe ukiwa kama katibu wa wizara ya Nishati na madhahabu,na kwa makusudi ukaruhusu pesa za umma kuchotwa na watu wachache wakiongozwa na yule Singasinga,then ukawatishia kuwapiga kaka zangu Zitto Kabwe na Kafulila,wakati unajua walikuwa wanatimiza jukumu la kuwatetea watanzania,wewe adhabu yako ni viboko 10 mfululizo,

Mtani wangu Mama Tibajuka,nimeelewa sasa kwanini ulirudishwa nyumbani Tz kutoka UN,bilioni 1.6 eti ukaendeleze shule zako za Kajumilo?wewe viboko 8 ni halali yako kwa niaba ya mabepali wote wa Bukoba na Muleba,

Pinda kweli wewe unatokea Sumbawanga,sakata lote hilo umelipanchi?hata hivyo mahakama ya umma inakutia hatiahani kwa uzembe na kudanganya kwamba hayo mabilioni si yetu watanzania,bila kujali kwamba huku kwetu Chigoma hakuna barabara za lami zinazoongonisha na mikoa mingine,so viboko 6 vya nguvu vitatupunguza machungu,

Na kwa wale watumishi wa Mungu waliopiga pesa zetu wakiongozwa na askofu Kigumu,adhabu yenu ni kutotoa sadaka nchi nzima kwa mda wa miezi 2 ili kufidia pesa zetu mlizokula,

Na kwa Ruge na wahaya wzenzake waliopiga pesa zetu,sisi kama watanzania tunaazimia kuchana na mipango yote ya kuja kuoa na Bukoba kwa mda wa miaka 2😔,ili muoane wenyewe,😢adhabu nyingine zinaendelea kujadiliwa,

Ni mimi mwakilishi wa Waha na waTz wa nje ya Bunge 🏤Nicholaus Kilunga ,toka Kigoma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom