Wana JF Iringa mjini gesti gani nzuri kufikia?

aliyeulizia gesti leo keshapata na ss hv anagida tusker lite briiidi huyu wa Iringa bado tu ?
 
Natarajia wiki hii kutembelea iringa nisaidien ,wapi na eneo gani kuna guest nzuri na pia eneo gan zuri kwa mapumuziko wikiend .Tafadhali chumba kisizidi 15000.
Ukishuka sttendi Iringa mjini,uliza mtaa unaoitwa barabara mbili,it ia a walking distance kutoka hapo stendi.

Mtaa huo utapata guest zinazoridhisha,kwa hiyo amount ya 15,ambayo ndiyo umesema,unaweza kuafford.
 
Jaman ile pale kwa chini b4 hujakata kona kuingia stendi kuu ya mabasi, nimeisahau jina, kigorofa fulan cheupe...ni hotel nzuri kaka, nafasi ya kutosha chumban, kitanda sita kwa sita, vyoo saaafi, chanel lukuki, lift inakusindikiza kukuokolea muda! Ila ni 55,000 kwa chumba, hiyo ya 15 haina haja ya kuuliza maana mh majanga best.
Mkuu ngoja nikukumbushe hiyo sehemu inaitwa Kalenga Westpark Hotel.

Ni sehemu nzuri na ni among the best places kwa kufikia hapa Iringa mjini.

Lakini mwenye kuleta thread,si umemsikia,anakwambia hiyo sehemu anayoweza kuafford isiwe more than 15 thou!
 
Natarajia wiki hii kutembelea iringa nisaidien ,wapi na eneo gani kuna guest nzuri na pia eneo gan zuri kwa mapumuziko wikiend .Tafadhali chumba kisizidi 15000.

Mkuu mi nikienda huwa nafikia KALENGA WEST PARK HOTEL. ni pazuri pale.
 
Chumba chini ya 15000 utapata Ipogolo au Makanyagio lakini jiandae kukesha kwa makelele ya walevi maana guest house za sh. 15000 zimezungukwa na vilabu vya komono , wanzuki, kangara na ulanzi.

Kuna kitu nimejifunza kutoka mada hii. Tupo wengi na kila mmoja na mtazamo wake. Jambo la msingi wengi tumetoa majibu kutokana na mtazamo binafsi bila kusoma anachokitaka mleta mada.

Mleta mada ni mtu mstaarabu, anayetaka kufanya upembuzi yakinifu kabla hajatua katika mji huo, pia yuko wazi katika kupanga bajeti yake tofauti na wengi wa wachangiaji wanaofikiria kufikia nyumba ghali wakati kuna za kawaida tu zikampa mapumziko mazuri zaidi na kwa gharama nafuu.

Nakumbuka Mjengwa alipoenda likizoni Ulaya alituambia ili kupanga bajeti vizuri alipofika Hispania aliamua kuchagua guest ya gharama nafuu na kufikiria njia bora ya kupunguza gharama za chakula kwa familia yake. Katika pitapita zangu kuna guest nchi za ulaya na marekani kuna kitchen (microwave) na special rates reduced rates weekly or monthly kwa wale wa kiwango changu tunaopenda kupanga bajeti na kubana matumizi. Jiwa napenda kufikia za kiwango hicho kwani weekly zipo za $200-$300, zipo ambazo unaweza ukalipa malipo kwa mwezi $600, lakini kwa hotelini maelfu yatakutoka. Nikienda zangu kama nitakaa miezi miwili na nikapata kibarua nitafanikiwa kulipia chumba na kubakiza cha kurudi nacho bongo. Haya ndiyo maisha ya akina yakhe tunayoyataka, wenye kufika juu zaidi tuwaache maana kuiga kiwango anachotoa tembo yatanishinda.

Nakukpongeza mleta mada kwa uwazi wako, pengine kwa sisi wengine umetupa funzo kubwa, maana wengine safari ni kuonyesha nini unacho hata kufikia kuparamia kinachokuzidi uwezo na unaporudi kwako ni kuanza upya kwa kulalamikia kwa nini mshahara wa mwezi huu haujafika mapema wakati tarehe za mwezi hazijafikia ukingoni kabisa.

Siko tayari kuwaiga wenye uwezo, hata kama naweza kujitahidi kufikia lakini kwangu mpango wa bajeti kwa malengo niliyojiwekea ndio huu wa Tsh 15,000 natapa chumba ambacho ni self contained na pia kuna usalama, maji safi na nafuliwa nguo bila shida, inatosha, kinachobaki ni kwa mlo swafi narudi home nimebakiza changu mfukoni kununulia sarudi na block za kuongeza mistari miwili ya vyumba vyangu viwili.

Huu ndio mpango mziwa wa wenye kupanga bajeti.
 
[/QUOTE
Nashukuru.
 
Unapoingia stendi mkono wa kushoto utaona guest house inaitwa TEMBO bei 7000
 
Kule kihesa dodima road kuna ile gold... iko poa itakufaa Augustino ameri
 
kuna gesti bubu moja maarufu sana hapo stendi. short time buku. kulala buku tatu. tatizo shuka zinakua zimetumiwa mchana kutwa na madereva wa taxi na mautingo kwa shot time.
Kwa hali hiyo hata airfreshiner hazihitajiki.
 
Back
Top Bottom