Wana-CHADEMA wengi wajitokeza kugombea Uenyeviti wa Vijiji na Vitongoji Muheza

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
886
206
Wanajamvi habari zenu,

Kama mjuavyo tunaelekea kwenye uchaguzi wa vijiji na vitongoji nchi nzima,taarifa za CHADEMA Muheza mpaka sasa wana chadema Muheza wamejitokeza kugombea,mpaka sasa nusu ya vijiji 74 na vitongoji 521 wagombea zaidi ya mmoja wamejitokeza kwa kutia nia ya kugombea.

Hapa CHADEMA inaimarika Muheza kwa nguvu sana huku hatua ya kura ya maoni kuchagua anayefaa kugombea kati ya walioomba ikisubiri mchakato wa chama kwa mujibu wa kanuni,taratibu,miongozo na katiba ya chama!

Mchakato unaendelea kukamilisha zoezi hilo ikienda sambamba na kuhamasisha watu wakajiandikishe kupiga kura.
 
Kama hamtakomaa kulinda kura basi msahau, kama mlishindwa kuandamana kwa kuwaogopa polisi, basi hao mnaowaogopa watakuwepo kwenye chaguzi zenu...Watawatisha kama kawaida yao...mtaufyata kama kawaida yenu...Watapewa ushindi kwa vicheko kama 'kawaida yao'...mtalalamika na kuwaombea mabaya kwa Mungu wenu kama kawaida yenu....Tutaendelea na maisha kama kawaida yetu....

"Kura zisipotosha zitatosheshwa" by Pasco
 
Kulinda kura muhimu sana.safari hii gamba lolote likijaribu kuiba kura yatakayompata asijilaumu.
 
SAFI SANA tupo pamoja.nasi huku rock city tumejipanga kwa ushindi mnono!
 
.......Pale ambapo wapinzani watakuwa imara katika kulinda kura zao, CCM watashindwa kuiba kura na hivyo watashindwa kwenye hayo maeneo kama kawaida yao.....mifano, Ubungo, Arusha, Mbeya, Iringa, Mwanza etc....

Back
Top Bottom