Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huu uliopita.

Makamu huyo nguli wa sheria na siasa bora Tanzania ametumia nafasi hiyo kuwapongeza watanzania waliokiunga mkono chama hicho kikiwa katika hali ngumu ya kifedha.

"Wanachama wetu na wafuasi waliendelea kufanya kazi za chama bure kabisa bila malipo, na hii inaonesha kuwa Chama chetu ni chama cha watu."

===

1678082736261.png

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku waliogoma kuichukua baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Uthibitisho huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu leo Jumapili, Machi 05, 2023 wakati akijibu maswali kwenye hadhara iliyofanyika kwenye mtandao wa Clubhouse.

“Chama (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku mwezi huu (Machi) ambayo hatukuichukua tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa 2020

“Tumepokea sehemu tu ya pesa hizo na kiasi kilichosalia tutapewa siku za usoni. Tumeamua kuichukua kwasababu ya ahadi ya maridhiano yanayoendelea,” alisema Lissu

Hata hivyo mwanasiasa huyo alisema hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika au Mwenyekiti, Freeman Mbowe atatoa taarifa rasmi.

Chadema iligoma kuchukua ruzuku hiyo inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya sh. Milioni 110 baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi waliyodai haukuwa uchaguzi bali ulikuwa ni uchafuzi.

Kwenye kauli za chama hicho walisikika wakisema kuwa wanaukataa uchaguzi na mazao yake.

Ikumbukwe chama hicho pia kilikataa kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni kwa sababu ya kutoutambua uchaguzi huo.

Hii ni hatua nyingine ya matunda ya maridhiano yanayoendelea baina ya chama hicho na Serikali.
 
Tundu Lissu ameongeza kuwa tangua Mwenyekiti Mbowe aachiwe Feburary 2022 Rais Samia amefanya mambo makubwa sana.

Pia amefanya na kutatua mambo muhimu ya kitaifa na hivyo yanatia matumaini kwamba huenda matatizo ya kisiasa, kitaifa, kikatiba yanaweza kupatiwa ufumbuzi.

Ameongeza kuwa katika kipindi hiki kifupi watu woote waliofunguliwa kesi na kufungwa kisiasa zote zimefutwa na watuhumiwa kuachiwa bila masharti. Hata hivyo amesema bado kuna kesi mbili tu ya Shinyanga na nyanda za kusini ambazo nazo ziko kqenye mchakato.

Tundu Lissu amesema amepata bahati ya kushiriki kikao cha Maridhiano aliporudi Tanzania na anasema mambo yamayojadiliwa humo hayajawahi kutokea tangua ameanza siasa za Tanzania.

hivyo anasema kuna dalili njema ikiwemo swala la Katiba Mpya.

mwisho ana hoji kwa kusema je ktk mazingira haya bado tunaweza kuendelea na msimamo ule ule wa wakatiule mambo hayajabadilika? Hapana. Tubaki na mambo makubwa zaidi haya madogo
chane nayo.
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuw Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huuuliopita...
 
IMG_1168.jpg

====

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku waliogoma kuichukua baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Uthibitisho huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu leo Jumapili, Machi 05, 2023 wakati akijibu maswali kwenye hadhara iliyofanyika kwenye mtandao wa Clubhouse.

“Chama (Chadema) kimeanza kupokea ruzuku mwezi huu (Machi) ambayo hatukuichukua tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa 2020.

“Tumepokea sehemu tu ya pesa hizo na kiasi kilichosalia tutapewa siku za usoni. Tumeamua kuichukua kwasababu ya ahadi ya maridhiano yanayoendelea,” alisema Lissu

Hata hivyo mwanasiasa huyo alisema hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika au Mwenyekiti, Freeman Mbowe atatoa taarifa rasmi.

Chadema iligoma kuchukua ruzuku hiyo inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya sh. Milioni 110 baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi waliyodai haukuwa uchaguzi bali ulikuwa ni uchafuzi.

Kwenye kauli za chama hicho walisikika wakisema kuwa wanaukataa uchaguzi na mazao yake.

Ikumbukwe chama hicho pia kilikataa kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni kwa sababu ya kutoutambua uchaguzi huo.

Hii ni hatua nyingine ya matunda ya maridhiano yanayoendelea baina ya chama hicho na serikali.
 
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huuuliopita...
Unadhani Vyama vingine wafuasi wameendelea kufanya kazi na hela? Chama gani hicho?
 
Back
Top Bottom