Wamuomba rais Kikwete aruhusu wanyongwe

Status
Not open for further replies.

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
na Asha Bani

KATIKA kile kinachoonyesha kuwa maisha ya wafungwa gerezani ni mabaya sana, wafungwa wawili wamemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, wakimuomba abatilishe adhabu ya kifungo cha maisha wanayotumikia ili wanyongwe hadi kufa.

Katika waraka huo ambao Tanzania Daima imepata nakala yake, wafungwa hao wanadai kuwa, kifo ni bora kulinganisha na tabu na mateso wanayoyapata wakiwa wafungwa wa maisha.

Katika barua hiyo, wafungwa hao kutoka gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam (majina na namba zao tunazihifadhi), wanamuomba Rais Kikwete atoe amri ya wao kunyongwa ili waepukane na mateso wanayoyapata hivi sasa.

Nakala ya barua hiyo iliyopitishiwa kwa Kamishna Mkuu wa Magereza, imetumwa pia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mkuu wa Magereza Mkoa (RPO).

Mmoja wa wafungwa hao anaeleza katika barua hiyo kuwa, alikamatwa mwaka 1977 kwa kosa la mauaji na kuhukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1983.

Hata hivyo, alisema kuwa mwaka 2002 alipata msamaha wa rais na adhabu yake ikapunguzwa na kuwa ya kifungo cha maisha.

Mfungwa mwingine, anadai katika barua hiyo kuwa, alikamatwa mwaka 1984 na kuhukumiwa adhabu ya kifo Februari 15, 1989.

Anasema kuwa, mnamo Mei 15, 2005 alipata msamaha wa rais na adhabu yake ikapunguzwa na kuwa kifungo cha maisha.

Katika barua yao, wanasema tangu wabadilishiwe adhabu hiyo, maisha yao yamekuwa ya tabu na shida kubwa kutokana na mateso wanayokumbana nayo gerezani na sasa wanatamani afadhali wangenyongwa.

"Kutokana na maisha ya gerezani kuwa magumu na ya tabu sana, tumefikia uamuzi wa hiari, Mheshimiwa Rais tunaomba utubadilishie uamuzi wako wa msamaha wa kifungo cha maisha na tuhukumu tena kunyongwa kwa kuwa tumechoka na tabu za huku gerezani Ukonga," wanasema wafungwa hao katika barua yao.

Hivi karibuni, mahabusu katika gereza la segerea nao walizungumzia maisha magumu wanayoishi gerezani humo.

Waliyasema hayo kufuatia mgomo wa siku nne wa mahabusu kugoma kusikiliza kesi zao mahakamani, uliowalazimisha mawaziri wanne kutembelea gereza la Keko na kuzungumza na mahabusu hao.

Mgomo wao ulichochewa na kuachiwa haraka kwa dhamana kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, anayekabiliwa na mashitaka ya mauaji bila kukusudia.


Source: Habari Tanzania
 
Sometym m2 unakata tamaa ya kuishi eti,sa m2 tangu mwaka 1977 yuko gerezan,kuna matumain kwel hapo?
 
KATIKA kile kinachoonyesha kuwa maisha ya wafungwa gerezani ni mabaya sana, wafungwa wawili wamemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete, wakimuomba abatilishe adhabu ya kifungo cha maisha wanayotumikia ili wanyongwe hadi kufa.

Mgomo wao ulichochewa na kuachiwa haraka kwa dhamana kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, anayekabiliwa na mashitaka ya mauaji bila kukusudia.

Mkuu,
Hii habari ni ya Zamani, miaka ile 1947!
Huyu Ditopile amerudi mbinguni & kwa udongo tayari au?
 
Kumbe Ditopile Mzuzuri, kafufuka tunashukuru mkuu kwa latest news
 
Ukweli ni kuwa Tanzania hatuna magereza ila tuna torture chambers. Ukweli unauma lakini that is the fact na huo ni ushahidi.

Malazi ni duni, chakula ni kama hakuna, maji ni luxury na bahati mbaya hawana mtu wa kuwasemea. Wizara ya mabo ya ndani wako busy na mradi wa vitambulisho na masuala ya polisi ili kuwadidimiza wapinzani.

Wizara ya sheria ambayo ingeziba pengo la udhaifu wa mambo ya ndani ndio usiseme.
 
Hawa jamaa wa kusubiri kifo si wale wanaokula na kulala tu? Sasa wamepelekwa 'uraiani' wanaona hapatoshi wanataka kurudi kule kwenye starehe. Na watanyongwa kweli safari hii. Imejin mtu kahukumiwa kifo 83 hadi 2002 hajatundikwa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom